Uko sahihi kwa kiasi. Ukifungamana nafsi na walio kwenye giza maana yake wewe ndio umenaswa. Ndio maana Biblia inasema;
2 Wakorintho 6
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
¹⁵ Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
¹⁶ Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
¹⁷ Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
¹⁸ Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,
Yesu Kristo ni Mungu, alikuja kuwatoa watu utumwani ikiwemo soul tie. Hakuja kuwaambia watu wajifungue wenyewe, bali wamwamini Yeye ili awafungue. Kwetu sisi imetupasa kuwahubiria watu habari hii njema, kuwa Yesu anao uwezo kuwatoa kwenye mahusiano ya kipepo. Tunawaonyesha ni jinsi gani yalivyo hayo mahusiano na jinsi gani yanakiuka sheria ya Bwana. Kisha tunawapa tumaini kuwa yuko awezaye kuwarejesha upya kabisa. Hiyo ndio Injili.