Vichaa wanafurahia kampani yangu

Vichaa wanafurahia kampani yangu

Pyaar

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
16,078
Reaction score
77,186
Habari wakuu,

Poleni kwa majukumu ya hapa na pale.

Kuna jambo nilianza kuliona tangu mwaka 2010 na limekuwa likiendelea siku hadi siku, miaka hadi miaka. Nimetokea kupendwa sana na watu wenye magonjwa ya akili, kwa lugha iliyozoeleka "Vichaa"

Aisee hii hali imekuwa ikitokea mara kwa mara hata nihamapo mkoa mmoja na kwenda kuishi mkoa mwingine hii hali bado naendelea kuiona.

Mfano nikipita eneo nikakutana na kichaa ambaye watu wengine wakipita wanakula mboko, mimi napita bila wasiwasi kabisa, hanigusi wala kunisumbua kwa lolote. Vilevile kuna mmoja pia huwa anakuja eneo langu la kazi anakaa pale muda mrefu (Muda huo haongei chochote) na asiponikuta hawezi kukaa na aliowakuta. Anajiondokea zake.

Mpaka muda huu ninaoandika huu ujumbe kakaa hapa. Aisee kaniletea hadi maembe, sijui kayaokota wapi. Yaani huwa najiuliza sipati majibu, ni kwamba wanafurahia kampani yangu au nini?
 
Embu jipige self na huyo kichaa wako tutumie then tutoe conclusion
 
Baraka izo kua katika hali walio nayo hawakupenda pengine nj sababu za kimagonjwa au binadamu na ndani yake kuna uwepo wa Mungu, na kumbuka Mungu anamaksudi yake, watendee wema kwan nao ni binadam wanahitaj haki zao za msingi kama binadamu wengine, haki moja wapo ni upendo, waonyeshe upendo kama Mungu ameweza kukupa nafasi iyo,
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Siku zote nimekuwa nikiwakubali sana
Mara nyingi nikikutana na kichaa lazima adondoshe tabasamu
Wewe ni daktari au Nesi eee?? Basi huenda una Nyota nzuri na wao, endeleza urafiki nao na uwasaidie kadiri uwezavyo..nao ni binadamu wanahitaji faraja
 
Back
Top Bottom