Vichekesho Azam Tv Live

Vichekesho Azam Tv Live

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
3,541
Reaction score
2,187
Nipo Naangalia vichekesho Azam Tv live,
Kiukweli wachekeshaji wa Tanzania bado tupo nyuma sana aisee, ingawa wametangulia watangulizi,
Bado kuchekesha sisi wabongo hatujaweza, ngoja tuone wale waliotangazwa wiki nzima,

Bado tuna safari ndefu,

MC nae bado aendani na comedy yenyewe

Kwa kifupi,
Vichekesho vilipendeza, MC pili pili alifunika, Ticha Mpamile alitendea aki jukwaa, alifanya alichoitiwa, Mau Fundi nae alifanya vzr tatizo muda aliopewa ulikuwa mfupi, Katharina wa Karatu aliogopa jukwaa hata kutembea alishindwa, kama alitumia dk nyingi hata NNE hazikuzidi, alijitahidi kidogo.

Huyu sasa mkenya tuliomsubiria kwa hamu! Mh mh mh mm namwachia Mungu, zaidi ya kumsifia diamond na lulu hakuna la maana alilofanya! Labda kwenye kakipengele ka kila mtu kuwa MC kwenye Harusi zao! Zaidi ya Hapo hakuna cha ajabu alichofanya.

Hii ni kwa mtazamo wangu
 
Dah bado sana, ila Mau amejitahidi, huu n mwanza Mgumu, mbeleni watatoboa tu
 
Kumchekesha mtu n ngumu sana aisee, Dah jamaa wanajitahidi
 
Ila wakipata exposure wataweza
Tatizo lao hawakijui vizuri kiswahili. Matumizi sahihi ya lugha kwenye kuchekesha ni muhimu sana. kama hujui kutumia lugha kwa wakati muafaka basi inakuwa ngumu kuchekesha.

Ila pia lugha yao ya mwili haichekeshi!
 
Bongo watu wana stress, we mtu anadaiwa kodi, mwingine cheti feki + kutumbuliwa ataanzaje kucheka
 
Ila wakipata nafasi zaidi watakuwa wazuri sana...
 
Back
Top Bottom