Sasa huyu mchaga anasema nini?
Mchaga amekufa, kakutana na malaika
mtoa roho;
ISRAEL: mangi hapa kuna njia mbili, kulia mbinguni, kushoto jehanamu. Unataka kwenda wapi?
MANGI: aisee! Mi siendi popote! Nabaki hapahapa!
ISRAEL: kwanini?
MANGI: bwashee! We hauoni nikikaa hapa nitatengeneza pesa? itakuwa senta moja ya hatari! Kutakuwa na supu, bia kwa sana. Nitapiga pesa ile mbaya! Kwanza hata wewe utafaidi, utakuwa ukienda kutoa roho, unaniletea stock ya nyama. Nakupa hela yako cash kabisa! Halafu utakuwa unapiga supu ya ulimi na beer, halafu unaingia mbinguni! Kwanza nashangaa kwanini shirima alipitaje hapa bila kushika plot? Au alikufa amelewa?
Israel hoi!