Vicky Kamata afunga Ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Likwelile

sasa bro umezungumza sawa, lakini huyo katibu wenu mkuu hakusoma hizo habari za ajabuajabu za huyo dada? kujihusisha nae ndio kusema naye anahusika na habari za ajabuajabu vilevile ndio wakakutana....
Watu wengine wana mioyo ya chuma. My God, Dr. kweli nimeamini halua haina makombo!
 
Hakufunga ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango; amefunga ndoa na Dk. Servacius Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
Soma tena ulichoandika ukiweza edit ueleweke mkuu unaheshima sana hapa jukwaani
 
image.jpeg
.................
 
Maisha yalivyo magumu nayeye ni mtetez wetu vijana si angenichagua ata mimi tujiinjoy jameni. Niache pulitebo nijiajir kwake.Pesa ya ubunge ingetutosha,akienda bungeni nikonaye beneti naivi amenoga yuko lainiiii,Ila poa tu dr faidi menyewe but usiwebize saana yeye geita-dom wewe busy dar.
 
According to Robert Mugabe " if you bear a girl child who is cute, but lacking enough intelligence, her private parts will be over ulized when she will be struggling to get better life". Ngoja niishie hapo bahari imeshachafuka moods wasije wakaanza na Mimi.
 
Vicky Kamata Afunga Ndoa na Dk. Likwelile

View attachment 331018 View attachment 331019

Dk Servacius Likwelile.

Dar es Salaam, Geita-Tanzania. Mbunge wa Viti Maalamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vicky Kamata amefunga ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile.

Dk Likwelile amefunga ndoa hiyo baada ya mkewe wa awali kufariki dunia Mei mwaka 2014.

Kwa hatua hiyo, Dk Likwelile amemfuta machozi mbunge huyo kijana baada ya ndoa yake ya awali aliyotarajia kuifunga na Charles Pai kukwama dakika za mwisho wakati wa maandalizi yote ya msingi kukamilika.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata, zilieleza kwamba mbunge huyo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya , alifunga ndoa hiyo Septemba mwaka jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Habari zinaeleza kuwa wawili hao baada ya kufunga ndoa, hawakuwa na sherehe kubwa bali walikuwa na ‘pati mchapalo’ iliyofanyika nyumbani kwa Dk Likwelile na kuwashirikisha baadhi ya wana ndugu na marafiki wa pande zote mbili.

“Wamefunga ndoa bomani, hakukuwa na sherehe bali kulikuwa na hafla ndogo iliyofanyika nyumbani na wanafamilia wachache ndio walioshiriki,” alisema mtoa habari wetu ambaye alikuwa mmoja wa watu wachache walioshuhudia ndoa hiyo.

Alipotafutwa kwa njia ya simu kuthibitisha taarifa hizi, Kamata alikiri kufunga ndoa hiyo, lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi.

“Umepata wapi hizi taarifa? Ila ni kweli nimefunga ndoa, ninachojua ni kwamba Dokta Likwelile ni mume wangu halali, namshukuru Mungu kwa hilo,” alisema kwa kifupi Vick na kukata simu.

Mei 24 mwaka 2014, Vick Kamata alikwama kufunga ndoa na Charles Pai baada ya kubainika kuwapo kwa kasoro kwenye nyaraka za mwanaume.

Hali hiyo ilisababisha mbunge kuugua ghafla kutokana na mshituko alioupata na kulazimika kulazwa katika Hospitali ya Tabata Genaral iliyopo Segerea. Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilikuwa zimesambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.

Kamata ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha “ Wanawake na Maendeleo” na pia ni mtetezi wa haki za wanawake.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima (Jumamosi Machi 19, 2016)
Vipi ile ndoa iliyoshindikana mwaka jana?
 
Hivyo huyu mama haoni aibu kwani tendo la kupata ndoa ni sawa na kupanda daladala?
 
Back
Top Bottom