Vicky Kamata asema marehemu mume wake "Alikuwa na vinyumba vya kawaida na msururu wa watoto!"

Vicky Kamata asema marehemu mume wake "Alikuwa na vinyumba vya kawaida na msururu wa watoto!"

Nakuomba msamaha mume wangu kwa kuwa mimi ni Mkatoliki na Imani yangu inaniambia unaona na unajua kila kitu kinachoendelea kati yangu na wanao.

Najua muda utaongea lakini kwa kuwa nami ni binadamu naomba niseme yafuatayo! Ni kweli mimi ni kiumbe dhaifu na mwenye dhambi nyingi tu kama wengine.

Lakini wanangu kwanini mnapindisha ukweli? Nimedhulumu mali gani? Nimemfukuza nani? Nyumba ipi? Wanangu hata kama ni chuki iwe na kiasi basii.

Sitaki kumuaibisha mume wangu lakini mnanichochea na kunisukuma wanangu! Niambie Dunia ukweli wa maisha yangu na Baba yenu? Alikuwa na pesa kunizidi yes! Lakini alikuwa na asset gani ya maana kunizidi mimi?

Baba yenu alikuwa na vinyumba vya kawaida na msululu wa watoto! Kwanini alipokuwa na Mama zenu hakufanya maendeleo? Leo mnanichafua na kunipaka matope kwa jasho langu? Mungu mnamjua nyie watoto?

Nimetoka familia masikini sana, na nimefika hapa kwa jasho la damu. Naomba sana mshangilie ushindi wenu kwa heshima! Sijafukuza mtu! Sijadhulumu na sintakuja kudhulumu maishani kwangu.

Nafanya kazi usiku na mchana kwa kuwa najua sina wa kunipa cha bure. Baba yenu hata swimming pool ameikuta kwangu. Na baadae nikachimba kwa pesa zangu ili nifurahie uzee wangu mimi na yeye. Bahati Mbaya Mungu kamuita mapema ange enjoy na alikuwa anaenjoy. Najua mnamuumiza sana. Tulieni sihitaji hata kijiko ambacho siyo cha jasho langu. Jasho la mama zenu mtalifaidi na mimi jasho langu hayupo wa kunidhulumu.

Maisha ni hadhithi tu. [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Pia, soma=> Vicky Kamata aangukia pua kesi ya mirathi ya Dkt. Servacius Likwelile
Alikuwa na pesa kunizidi yes! Lakini alikuwa na asset gani ya maana kunizidi mimi?[emoji848][emoji2827]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu aliekuwa kitengo nyeti BOT mtaalamu wa Uchumi anatambiwa na kilaza
Sema wabongo hatuna exposure kabisa hata uwe tajiri vipi.

Kwa hizo Hela ninaenda zangu hapo Caribbean countries Jamaica, Bahama, Saint Lucia, Dominica, Puntacana.

Kuna watoto safi wamenyooka Tena unaweza kupata mtoto decent au mtu mzima very decent. Huwa nashangaa sana mtu ana mapewa tele na ana uwezo wa kusafiri nchi yoyote ila Bado anahangaika na malaya vichwa maji wa kitanzania wasio kuwa na akili kichwani.

Kama una vihela vya hapa na pale karibu kutembelea hizo nchi. Kwanza ukiwa black na vihela Huwa wanajua wewe ni black American utagandwa Hadi ukome[emoji2]

Wabongo exposure ni zero
 
Halafu msimpaishe Vicky kiiivyo, mzee wa msoga alishaga muacha way back yaani kama jamaa ana mtu, basi ana mtu mwenye akili zake sio Vicky alishindwa hata kuficha siri mpaka mama mjengo alijua. Vicky alikuwa anapenda ndoa sana matokeo yake hajawahi kuipata. Mnakumbuka yule jamaa hakuonekana kanisani sinza siku ya ndoa yake na Vicky? Yule alipangwa na mama mjengo kumkomoa Vicky. Likewise likwelile alijua ndoa ni Batili lakini kwa kuwa Vicky alikuwa desperate na ndoa akamkubalia tu ili ajifurahishe nafsi. Kuhusu exposure jamaa aliishi nchi nyingi na watoto wake wengine wana Uraia wa UK.
 
Huyu ana mali zake mbili tatu si haba, sijui kwanini alitaka adhulumu watoto, kweli hakuna kitu kibaya kama greed, shame on you Vick.

Halafu huwa ni mihemko au nini? Hii mitandao hii, eti nakuomba msamaha mume wangu, wapi? Insta? Unamuomba msamaha marehenu Halafu insta!!!
 
Halafu msimpaishe Vicky kiiivyo, mzee wa msoga alishaga muacha way back yaani kama jamaa ana mtu, basi ana mtu mwenye akili zake sio Vicky alishindwa hata kuficha siri mpaka mama mjengo alijua. Vicky alikuwa anapenda ndoa sana matokeo yake hajawahi kuipata. Mnakumbuka yule jamaa hakuonekana kanisani sinza siku ya ndoa yake na Vicky? Yule alipangwa na mama mjengo kumkomoa Vicky. Likewise likwelile alijua ndoa ni Batili lakini kwa kuwa Vicky alikuwa desperate na ndoa akamkubalia tu ili ajifurahishe nafsi. Kuhusu exposure jamaa aliishi nchi nyingi na watoto wake wengine wana Uraia wa UK.
Halafu ni vile tu hajui, hii case kuna wazito behind the scene waliokuwa wanaangalia haki itendeke, Vick kudhani angeweza kumuhonga kila mtu ni kujitafutia kutumika bila sababu.

Vick vita yake ni ngumu cause mama mjengo hata kaa amsamehe abadani asilani na yuko naye sambamba kwenye kila vita.

Kijana alijazwa mihela akapita kushoto.
 
Sheria za Tanzania sizielewi mimi.

Mfano Dada akizaa na Jamaa pasipo ndoa na huku jamaa bado hajaoa yani hakuwa na mke.
Jamaa akifaliki na kuaacha baadhi ya mali huyo dada aliyezaa nae hawezi kuchukua mali kwa kisingizio cha mtoto mali zinabaki kwa ndugu wa ME.

Ila mwanamke akizaa na Mume wa mtu ambaye anafamilia yake kabisa na mke wake wa ndoa. Mume akifariki akaacha mali alizochuma na mume wake , huyo dada aliyevamia ndoa ya watu anaweza kuchukua mali 😬😬😳 kwa kisingizo cha mtoto why??? Wakati hakuwa mume wake??
Huku sheria za Tanzania zinasema kutembea na mke wa mtu au mume wa mtu ni kosa kisheria.
 
Halafu msimpaishe Vicky kiiivyo, mzee wa msoga alishaga muacha way back yaani kama jamaa ana mtu, basi ana mtu mwenye akili zake sio Vicky alishindwa hata kuficha siri mpaka mama mjengo alijua. Vicky alikuwa anapenda ndoa sana matokeo yake hajawahi kuipata. Mnakumbuka yule jamaa hakuonekana kanisani sinza siku ya ndoa yake na Vicky? Yule alipangwa na mama mjengo kumkomoa Vicky. Likewise likwelile alijua ndoa ni Batili lakini kwa kuwa Vicky alikuwa desperate na ndoa akamkubalia tu ili ajifurahishe nafsi. Kuhusu exposure jamaa aliishi nchi nyingi na watoto wake wengine wana Uraia wa UK.
Ndoa alifunga mbili, moja Rita wakasema cheti feki, kingine kanisani Arusha nacho feki, nabiii kaulizwa kasema hakuna kitu Kama hicho, na kaambiwa ndoa kikristu ni moja tu, Tena Ana bahati vyeti vya kufoji angekuwa mwenzangu na Mimi si ingikuwa lupango Sasa hivi.
 
Disco limeingia mmasai... Uswazi wanasema shoes limepata subwoofer[emoji23]

BILA HURUMA MANGE KIMAMBI AMVAA VICKY KAMATA

"Wee embu tutolee mapepo yako sisi, hao watoto walishaongea na walijibu maswali yoote uliyowauliza hapo, na walipoongea kuhusu kuwafukuza kwenye nyumba ya baba yao uliwajibu kwa jeuri kuwa haki haidaiwi mtandaoni waende Mahakamani, sasa Mahakamani watoto wamekutoa knockout unakuja kujitilisha huruma

Eti mali zilikuwa zako, kwahiyo Mahakama haina akili kuweka hizo mali kwenye mirathi? Kwahiyo Mahakama imechukua mali ambazo ni zako wakaziweka kwenye mirathi? Kwahiyo wewe ndo una akili kuliko Mahakama? Yaani leo ndio ume-proove ulikuwa na plan kubwa ya kuwadhulumu hao watoto kila kitu, eti baba yao hakuwa na asset yoyote, nyo**** Katibu Mkuu Wizara ya fedha hakuwa na asset yoyote? Dadrekiii kweli dada ulijipanga kuondoka na kila kitu.

Eti hukuwafukuza watoto, so watoto ambao wengine ni underage, wengine walikuwa chuo waliamua tu kuondoka kwenye nyumba ya baba yao wakahangaike na dunia? Unawaambia Watanzania watoto wa Likwelile waliondoka tu kwa matakwa yao wakaamua kwenda kuteseka na dunia? Embu kaa kimya wewe, Vicky ulibadili mpaka vitasa vya nyumba, walinzi ukawapa Order hakuna kuwafungulia geti watoto, au unataka zipostiwe video za watoto wa Likwelile wakiwa getini walinzi wakawa wanagoma kuwafungulia geti? Mpaka ulimuitia Polisi mtoto wa kiume wa Marehemu ukadai ni jambazi, leo unataka kujifanya mwema huku kwenye mitandao?

Alafu koma kumwita Uncle wangu Likwelile mume wako, Mahakama ishasema hujawahi kuwa mke wake. Vicky huna maana wewe hata mwaka hukukaa toka Likwelile afariki ukaanza kulea Vibenteni mpaka hapo ulipo uko na kitoto kidogo kinakukaz* ndani ya nyumba ya Likwelile. Vicky nakwambia hivi!! Bado hujasema, mpaka useme"- ameandika Kimambi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom