Victoria apewe Kura za Ndio
lulu mpya Umoja Wa - Vijana
" Always learning and always sharing what I have learned - purpose of acquiring knowledge for it to be beneficial to everyone " Victoria Mwanziva 2017
25 mei 2022 Baraza Kuu la Umoja Wa Vijana ( Uvccm ) Taifa lilipo mthibitisha Cde ' Victoria C . Mwanziva Kuwa Katibu Wa Uhamasishaji na chipukizi Uvccm Taifa nilijisemea moyoni Uvccm wamelamba dume
Ingizo Sahihi na Wakati Sahihi , ninamfahamu Kiongozi huyu , Kwa namna alivyo na Wivu na Mahaba Kwa CCM nikajua ana kwenda kuleta radha Tofauti pale makao Makuu Ya Uvccm , nathubutu Kusema kongole Uvccm Kwa namna mlivyo litendea haki pendekezo la Halmashauri Kuu Ya Chama Chetu Taifa na matunda tumeyaona
Kiongozi Victoria aliingia na spirit Ileile tunayoifahamu toka kwake ya kuunganisha Vijana Nchini na Kusaka Kila fursa inayojitokeza Ndani na Nje ya Nchi Kwa ajili ya Vijana Wa Tanzania ikiwamo Fursa za mafunzo ( scholarships )
Na kwa Mwaka Huu 2022 akisaidia Kundi kubwa la Vijana Kupata mafunzo ya Uongozi katika Usimamizi Wa Umma ( leadership in public management ) , uongozi Katika Biashara ( leadership in business management ) na Uongozi katika Jamii ( leadership in civic engagement ) Yanayotolewa na YALI Mandela Washington fellowship yaliyofayika Minessota Marekani , Chini Ya Usimamizi Wa Department of state of America
Kama ni kuvaa viatu Vya Muhamasa aliye tangulia Mhe. Jokate Urban Mwegelo Ambaye Sasa Ni DC Temeke Ndg Victoria anatosha ametutendea Haki Vijana Wenzie
Lengo la makala Hii si kuzungumzia Sana nafasi yake Hii ya Hamasa Msomi Huyu Wa Shahada ya Uzamili ambaye kwake kujitoa Kwa Jambo la CCM hakuna mjadala Bali ni kumuombea Kura Nyingi Za Ndio Baada ya Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Ya CCM ( CC ) kupendekeza Jina lake Kwa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa ( NEC ) ambayo pia Imempitisha Kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Wa Uvccm Taifa 2022 - 2027
Akiwa masomoni Nchini China Comrade Victoria hakuacha tabia yake ya kujifunza mambo mbalimbali Nje ya darasa ambayo pia uyaleta Mbele ya Umma ( public platforms ) Kwa manufaa ya Vijana Nchini Bila kujali gharama za nauli kwenda Katika midahalo mbali na Chuo Cha Institute of technology *Beijing China, ukiwamo Ule ulioudhuriwa na Billionea JACK MA Wa Global young leaders youth summit Uliofanyika Jimbo la Hangzhou Zhejiang chin ya Udhamini Wa Alibaba foundation na general association of Zhejiang entrepreneurs
Ni Ndugu Mwanziva aliye saidia ( connections ) Vijana Nchini Kupata Fursa za mafunzo Seoul Nchini Korea , na Fursa Nyingine Nyingi ikiwamo Ile ya Sadc Youth forum : climate change Youth envoy , amekuwa msaada Wa Kulea Vijana Wenzie na kuwapa mwelekeo ( Coaching and mentoring ) Cde Victoria atatufaa
Naomba Kura Kwa Gwiji Huyu Wa Uvccm Mwenye Uwezo Wa kuzungumza lugha Zaidi ya Tano ikiwamo Kichina , Kiingereza na Kiswahili ambaye alipokua Katika masomo ya Shahada yake ya Kwanza Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam alikua Kiongozi wa Vijana Chini Ya - Youth United Nations Association UDSM chapter Akishiriki Tafiti Nyingi Kwa Msaada Wa REDET kujua Nini ni Mahitaji Muhimu Kwa Viongozi Vijana Afrika
Victoria Anatosha Wajumbe Tunawategemea
Mwangoka Deogratius - Mwana CCM Rungwe