SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2



Yule Super Women aliyesema anauza Mchicha mpaka Ulaya Leo amekamatwa Oman na Kete 100 za unga.
Screenshot 2025-02-24 220234.png
 
Tunachokijua
Yupo mwanamke anayetambulika kama superwoman (Pendo Open Kitchen”) ambaye amejizolea umaarufu kutokana na vipande vya video vinavyomuhusu yeye akiongelea namna alivyopata mafanikio kutokana na harakati zake ikiwemo kuuza mchicha online hadi mataifa ya nje ikiwemo Uingereza na Ujerumani. Tazama hapa

Madai

Kumekuwepo na kipande cha video kilichoambatana na taarifa kuwa superwoman amekamatwa na madawa ya kulevya Oman. Taarifa hiyo ikihusianishwa na mwanamke aliyejipatia umaarufu mitandaoni kwa kueleza kuwa pesa zake anazipata kwa kufanya biashara mbalimbali ikiwemo kuuza mchicha katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Taarifa iliyoambatana na video hiyo inajaribu kuonesha kuwa mwanamke huyo amekuwa akifanya biashara za madawa ya kulevya na hivyo amekamatwa. Tazama hapa na hapa.

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa njia ya mtandao na google reverse image search umebaini kuwa video hiyo si ya hivi karibuni. Mttu mmoja aliweka kipande hiko cha video Julai 29, 2023 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram bila kuweka maelezo yoyote yale. Tazama hapa

Ufuatiliaji zaidi umebaini tovuti kadhaa ziliripoti ikiwemo tovuti ya Legit ambayo ilichapisha taarifa Februari 5, 2021 yenye kichwa cha habari “Video inaonesha akiwa na dawa za kulevya zilizojazwa chini ya wigi, maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wapigwa na butwaa”. Katika Taarifa hiyo walieleza namna tukio hilo lilivyotokea katika uwanja mmoja wa ndege na hali iliyokuwa ikionekana katika tukio hilo ingawa hawakueleza zaidi.

Tovuti nyingine inayojulikana kama Justnaija ilichapisha taarifa iliyoambana na video hiyo tena Julai 23, 2023`ilielezea pia tukio hilo inagwa na wao pia hawakueleza tukio hilo limetokea wapi na ulikuwa ni uwanja upi wa ndege.

Hivyo video hiyo si ya hivi karibuni kama ilivyosambaa zaidi katika mitandao mbalimbali ya kuanzia Februari 21, 2025. Pia hakuna uthibitisho wa kuwa video hiyo inamuhusu Mtanzania.
Mimi tangu Shamimu Zeze 8020 Fashion mamaa wa kibubu akamatwe na NGADA siwaamini tena hawa walioanza na mtaji wa afu tatu.

Siri ya utajiri anaijua TAJIRI mwenyewe hayo anayoyaelezea nje si yaliyompa huo utajiri ,hayo ya nje unayoyaona ni camouflage.
 
Kwa waarabu kaisha huyo ,halafu ni ushamba sana yaani hapo hata zile Scanner za screening airport anashikwa.
Inaweza kuwa ilikuwa mbinu yake kupitisha na si unajua ma papa huwa yanasafisha njia kabisa sas hapo ukikuta njia haijasafishwa hahah lazim ujae mikononi kingine wakiona passport imejaa mihuri ndani ya miezi umesafir mara kadhaa kengere za masikio zinalia wanaanza kukutilia mashaka unajaa mikononi mwao hujiulizi why wengine wapite na mtu kameza kete tumboni lakin wana mpoint yeye apigwe full body scan washamtarget kitambo
 
Kakamatwa kwenye harakati.

Live for nothing, die for something
Get rich or die trying
ndio hii.

Ila usimuamini mtu aliyetoboa hata siku moja, mafanikio yana siri nyingi sana.
Haha ni kweli watu wana siri nyingi lakin pia watu wapine kabla hawajaingia kwenye hiyo career
 
Hii clip niliiona TikTok kuna watu walisema huyo mtu sio Mtanzania ni Mnigeria na clip ni ya siku nyingi
Ya miaka 4 huko hyo mama ni muwest africa naona watu wana comment kama tu 😄

Ova
 
View attachment 3245074


Yule Super Women aliyesema anauza Mchicha mpaka Ulaya Leo amekamatwa Oman na Kete 100 za unga.
Looh!

Ameumbuka vibaya sana. Njia ya mwongo ni fupi.

Hawa ndio wamekuwa wakilichafua jina la nchi ya Tanzania huko ughaibuni kiasi cha kuifanya Passport za Tanzania kuonekana kuwa ni za Watu wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Wafungwe maisha huko huko walikokamatiwa au wanyongwe kabisa ili kuwapunguza idadi yao hawa Watu. Wamekuwa wakisababisha Kero kubwa sana kwa Wasafiri wengine wenye Passport za Tanzania ambao ni raia wema kwani na wao pia wamekuwa wakihisiwa kuwa wanajihusisha na uhalifu wa namna hii.
 
Yaan hizi mbuzi, na wasanii hawa Akina Chino, Nifah ,wale Ma DJ ,wasanii wanaojificha CCM.


Unajiuliza, huyu Chino kama kudensi Kuna Akina Iyobo wameanza kitamboooo, inakuaje kuaje??.

Kama uDJ unajiuliza, mbona MaDJ ni wengi sana, inakuaje MTU ana nyumba ya B 1+, Magari ya kifahari


Kiukweli kabisaaa kabisaaaa, Hapa Bongo, Sanaa ya Muziki, Filamu, Uchekeshaji, Biashara mitandaoni , Badoo haijafikia Hadhi ya kumpa MTU Nyumba za Mabilioni Kadhaa ,Magari ya mabilioni .

Badoooo, badooooo !!!.

Manina zao, wanatupa stress tukidhan tumechelewa kumbe ndo zao
Wengi wao wanafanya uhalifu nyuma ya pazia. Money laundering na madawa ya kulevya ndo sababu kuu.
 
Its about time kwa Mamlaka kuhakikisha Jamii inapata Role models na Public figures wenye elimu, vipaji vya maana na Kazi za kijasiriamali zenye tija. Muhalifu kama huyu alipataje airtime?? hawa wadada na Wakaka huko social media ambao wana influence upuuzi wanaruhusiwaje kulisha content zao kwa jamii.. ???

Hivi kipindi cha Wasomi, Wagunduzi wa kiteknolojia, Wasanii kutamalaki kwenye vyombo vya habari kiliishia wapi??? Nakumbuka enzi zetu tunakua watu kama Philbert Bay, Tanzania Ones , Doctors, engineers etc ndo vitu vijana walikua wanafuatilia na kutamani.. ila leo Wahalifu wanaruhusiwa kujinadi wazi wazi na kujipa majina ya sijui wapambanaji, content creator, social media figures na takataka zingine.. jaman Sera zitungwe ili kuokoa jahazi.. social media Contentz zinanguvu kubwa sana kushape direction ya Jamii nzima.. watu kama hawa wasipewe Nafasi kabisa..
Majanga ya uchawa na kujipendekeza yameharibu taswira ya Taifa na wasomi hence walio na Elimu wamekuwa sawa kama wasio na Elimu ki mtazamo, mawazo na uwasilishaji wa hoja. Vilevile media kwa sasa hatuna Tanzania. Over🙌🏻
 
maisha si mchezo
ukiona mtu ana fedha alafu kirahisi anakwambia nafanya biashara hii ni uwongo

kuna jamaa alikuwa anatuaminisha biashara ya mawese inalipa sana maana ana majumba na mali zingine
kile kipindi cha magu wanafatilia wauza pembe za ndovu jamaa kakamatwa na mzigo

tangu hapo stori za fanya kazi kwa bidiii huwa sizitaki masikioni mwangu
Ko huamini kama mawese yanalipa tena 😂😂😂
 
duuh!sasa kama kakamatwa huko,atahukumiwa huko huko au atarejeshwa bongo kuhukumiwa?
 
Fungua code bloangu ndio nani huyo,wengine hatumjui,hatakushughulikia kwani yupo chini ya ulinzi
'MUNGU Anatupenda Sote Waislam kwa Wakristo, kwa nini tugombane wakati sote ni Viumbe vyake????
Kama unatenda Matendo Mema,Dini hazina umuhimu wowote Duniani lazima PEPO utaiona tu'
Aise hii signature yako juu nimeipenda mno mungu akubariki mambo yako yawe mepesi ngoja niku inbox
 
Back
Top Bottom