SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2



Yule Super Women aliyesema anauza Mchicha mpaka Ulaya Leo amekamatwa Oman na Kete 100 za unga.
Screenshot 2025-02-24 220234.png
 
Tunachokijua
Yupo mwanamke anayetambulika kama superwoman (Pendo Open Kitchen”) ambaye amejizolea umaarufu kutokana na vipande vya video vinavyomuhusu yeye akiongelea namna alivyopata mafanikio kutokana na harakati zake ikiwemo kuuza mchicha online hadi mataifa ya nje ikiwemo Uingereza na Ujerumani. Tazama hapa

Madai

Kumekuwepo na kipande cha video kilichoambatana na taarifa kuwa superwoman amekamatwa na madawa ya kulevya Oman. Taarifa hiyo ikihusianishwa na mwanamke aliyejipatia umaarufu mitandaoni kwa kueleza kuwa pesa zake anazipata kwa kufanya biashara mbalimbali ikiwemo kuuza mchicha katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Taarifa iliyoambatana na video hiyo inajaribu kuonesha kuwa mwanamke huyo amekuwa akifanya biashara za madawa ya kulevya na hivyo amekamatwa. Tazama hapa na hapa.

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa njia ya mtandao na google reverse image search umebaini kuwa video hiyo si ya hivi karibuni. Mttu mmoja aliweka kipande hiko cha video Julai 29, 2023 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram bila kuweka maelezo yoyote yale. Tazama hapa

Ufuatiliaji zaidi umebaini tovuti kadhaa ziliripoti ikiwemo tovuti ya Legit ambayo ilichapisha taarifa Februari 5, 2021 yenye kichwa cha habari “Video inaonesha akiwa na dawa za kulevya zilizojazwa chini ya wigi, maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wapigwa na butwaa”. Katika Taarifa hiyo walieleza namna tukio hilo lilivyotokea katika uwanja mmoja wa ndege na hali iliyokuwa ikionekana katika tukio hilo ingawa hawakueleza zaidi.

Tovuti nyingine inayojulikana kama Justnaija ilichapisha taarifa iliyoambana na video hiyo tena Julai 23, 2023`ilielezea pia tukio hilo inagwa na wao pia hawakueleza tukio hilo limetokea wapi na ulikuwa ni uwanja upi wa ndege.

Hivyo video hiyo si ya hivi karibuni kama ilivyosambaa zaidi katika mitandao mbalimbali ya kuanzia Februari 21, 2025. Pia hakuna uthibitisho wa kuwa video hiyo inamuhusu Mtanzania.
maisha si mchezo
ukiona mtu ana fedha alafu kirahisi anakwambia nafanya biashara hii ni uwongo

kuna jamaa alikuwa anatuaminisha biashara ya mawese inalipa sana maana ana majumba na mali zingine
kile kipindi cha magu wanafatilia wauza pembe za ndovu jamaa kakamatwa na mzigo

tangu hapo stori za fanya kazi kwa bidiii huwa sizitaki masikioni mwangu
Wazee tusake hela za kubadilisha mboga tuu na mbususu hawa wengine story nying buree
 
Uwanja wa ndege Dar aliwezane kutoka na madawa yote hayo ambayo hata ukaguzi wa bila kutumia vifaa unayagundua.Tanzania imekuwa salama Kwa biashara za madawa ya kulevya chini ya wamu ya sita
Bro ! Inawezekana akatoka bongo akiwa hana mzigo ila akafika Dubai akatoka na mzigo kupeleka kwingine na vice versa
 
Uwanja wa ndege Dar aliwezane kutoka na madawa yote hayo ambayo hata ukaguzi wa bila kutumia vifaa unayagundua.Tanzania imekuwa salama Kwa biashara za madawa ya kulevya chini ya wamu ya sita
Je kama maafisa wa huku ndio walio mchomesha huko il kukwepa mikono ya ma PAPA wa hapa mjini?
 
Mshukuru Mungu kwa huyo uliye naye, huyo ht wewe angekuuza au kukuua, wanawake wa dizain hiyo ni makatili hayajali chochote
Nikimpata mwanamke anaye weza kuniua au kunitoa kafara ili watoto wetu waishi kitajiri HATA LEO HII HII NAMUOA
 
Back
Top Bottom