SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2



Yule Super Women aliyesema anauza Mchicha mpaka Ulaya Leo amekamatwa Oman na Kete 100 za unga.
Screenshot 2025-02-24 220234.png
 
Tunachokijua
Yupo mwanamke anayetambulika kama superwoman (Pendo Open Kitchen”) ambaye amejizolea umaarufu kutokana na vipande vya video vinavyomuhusu yeye akiongelea namna alivyopata mafanikio kutokana na harakati zake ikiwemo kuuza mchicha online hadi mataifa ya nje ikiwemo Uingereza na Ujerumani. Tazama hapa

Madai

Kumekuwepo na kipande cha video kilichoambatana na taarifa kuwa superwoman amekamatwa na madawa ya kulevya Oman. Taarifa hiyo ikihusianishwa na mwanamke aliyejipatia umaarufu mitandaoni kwa kueleza kuwa pesa zake anazipata kwa kufanya biashara mbalimbali ikiwemo kuuza mchicha katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Taarifa iliyoambatana na video hiyo inajaribu kuonesha kuwa mwanamke huyo amekuwa akifanya biashara za madawa ya kulevya na hivyo amekamatwa. Tazama hapa na hapa.

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa njia ya mtandao na google reverse image search umebaini kuwa video hiyo si ya hivi karibuni. Mttu mmoja aliweka kipande hiko cha video Julai 29, 2023 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram bila kuweka maelezo yoyote yale. Tazama hapa

Ufuatiliaji zaidi umebaini tovuti kadhaa ziliripoti ikiwemo tovuti ya Legit ambayo ilichapisha taarifa Februari 5, 2021 yenye kichwa cha habari “Video inaonesha akiwa na dawa za kulevya zilizojazwa chini ya wigi, maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wapigwa na butwaa”. Katika Taarifa hiyo walieleza namna tukio hilo lilivyotokea katika uwanja mmoja wa ndege na hali iliyokuwa ikionekana katika tukio hilo ingawa hawakueleza zaidi.

Tovuti nyingine inayojulikana kama Justnaija ilichapisha taarifa iliyoambana na video hiyo tena Julai 23, 2023`ilielezea pia tukio hilo inagwa na wao pia hawakueleza tukio hilo limetokea wapi na ulikuwa ni uwanja upi wa ndege.

Hivyo video hiyo si ya hivi karibuni kama ilivyosambaa zaidi katika mitandao mbalimbali ya kuanzia Februari 21, 2025. Pia hakuna uthibitisho wa kuwa video hiyo inamuhusu Mtanzania.
Stori za mafanikio huwa zinasimuliwa kwa sauti ya chini na kwa upole sana.

Ukiona mtu anasimulia kwa kupayuka jua hamna kitu hapo
Huyu asingekamatwa, siku moja angedanganya watu kuwa alianzia biashara na fungu moja la mchicha wa jero, na sasa ni milionea.
 
Its about time kwa Mamlaka kuhakikisha Jamii inapata Role models na Public figures wenye elimu, vipaji vya maana na Kazi za kijasiriamali zenye tija. Muhalifu kama huyu alipataje airtime?? hawa wadada na Wakaka huko social media ambao wana influence upuuzi wanaruhusiwaje kulisha content zao kwa jamii.. ???

Hivi kipindi cha Wasomi, Wagunduzi wa kiteknolojia, Wasanii kutamalaki kwenye vyombo vya habari kiliishia wapi??? Nakumbuka enzi zetu tunakua watu kama Philbert Bay, Tanzania Ones , Doctors, engineers etc ndo vitu vijana walikua wanafuatilia na kutamani.. ila leo Wahalifu wanaruhusiwa kujinadi wazi wazi na kujipa majina ya sijui wapambanaji, content creator, social media figures na takataka zingine.. jaman Sera zitungwe ili kuokoa jahazi.. social media Contentz zinanguvu kubwa sana kushape direction ya Jamii nzima.. watu kama hawa wasipewe Nafasi kabisa..
Mwanangu umeongea point kubwa sana.
 
Yaan hizi mbuzi, na wasanii hawa Akina Chino, Nifah ,wale Ma DJ ,wasanii wanaojificha CCM.


Unajiuliza, huyu Chino kama kudensi Kuna Akina Iyobo wameanza kitamboooo, inakuaje kuaje??.

Kama uDJ unajiuliza, mbona MaDJ ni wengi sana, inakuaje MTU ana nyumba ya B 1+, Magari ya kifahari


Kiukweli kabisaaa kabisaaaa, Hapa Bongo, Sanaa ya Muziki, Filamu, Uchekeshaji, Biashara mitandaoni , Badoo haijafikia Hadhi ya kumpa MTU Nyumba za Mabilioni Kadhaa ,Magari ya mabilioni .

Badoooo, badooooo !!!.

Manina zao, wanatupa stress tukidhan tumechelewa kumbe ndo zao
Noma sana🚨🚨🚨🚨
 
Back
Top Bottom