SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2



Yule Super Women aliyesema anauza Mchicha mpaka Ulaya Leo amekamatwa Oman na Kete 100 za unga.
Screenshot 2025-02-24 220234.png
 
Tunachokijua
Yupo mwanamke anayetambulika kama superwoman (Pendo Open Kitchen”) ambaye amejizolea umaarufu kutokana na vipande vya video vinavyomuhusu yeye akiongelea namna alivyopata mafanikio kutokana na harakati zake ikiwemo kuuza mchicha online hadi mataifa ya nje ikiwemo Uingereza na Ujerumani. Tazama hapa

Madai

Kumekuwepo na kipande cha video kilichoambatana na taarifa kuwa superwoman amekamatwa na madawa ya kulevya Oman. Taarifa hiyo ikihusianishwa na mwanamke aliyejipatia umaarufu mitandaoni kwa kueleza kuwa pesa zake anazipata kwa kufanya biashara mbalimbali ikiwemo kuuza mchicha katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Taarifa iliyoambatana na video hiyo inajaribu kuonesha kuwa mwanamke huyo amekuwa akifanya biashara za madawa ya kulevya na hivyo amekamatwa. Tazama hapa na hapa.

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa njia ya mtandao na google reverse image search umebaini kuwa video hiyo si ya hivi karibuni. Mttu mmoja aliweka kipande hiko cha video Julai 29, 2023 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram bila kuweka maelezo yoyote yale. Tazama hapa

Ufuatiliaji zaidi umebaini tovuti kadhaa ziliripoti ikiwemo tovuti ya Legit ambayo ilichapisha taarifa Februari 5, 2021 yenye kichwa cha habari “Video inaonesha akiwa na dawa za kulevya zilizojazwa chini ya wigi, maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wapigwa na butwaa”. Katika Taarifa hiyo walieleza namna tukio hilo lilivyotokea katika uwanja mmoja wa ndege na hali iliyokuwa ikionekana katika tukio hilo ingawa hawakueleza zaidi.

Tovuti nyingine inayojulikana kama Justnaija ilichapisha taarifa iliyoambana na video hiyo tena Julai 23, 2023`ilielezea pia tukio hilo inagwa na wao pia hawakueleza tukio hilo limetokea wapi na ulikuwa ni uwanja upi wa ndege.

Hivyo video hiyo si ya hivi karibuni kama ilivyosambaa zaidi katika mitandao mbalimbali ya kuanzia Februari 21, 2025. Pia hakuna uthibitisho wa kuwa video hiyo inamuhusu Mtanzania.
Unaweza kushangaa hawa watu wasioleweka hata biashara zao hazieleweki ndio wanapata airtime ..Kuna yule chief wa Mbeya yaani hovyo kabisa.
Wachungaji wa mwendokasi pia wanaobadilisha magari kila siku.
 
Sio mwamba naunga mkono kuuza unga, mie niko kati kwa kati..
Wakati mwingine hawa wala unga wanajiingiza wenyewe, sidhani kama kuna mtu amemshikia mtu bunduki ale unga.
Hapana sometimes Hawa jamaa huwa wanatengeneza wateja kama vile marketing ya bidhaa nyingine mfano anaweza tumwa mtu mmoja akaenda kuwaasha masela wa vijiweni wa mtaa mzima ndo maana unakuta wengi walichanganyiwa kwenye sigara au bangi mpaka wakawa wateja mazima hiyo nishaishuhudia
 
Uwanja wa ndege Dar aliwezane kutoka na madawa yote hayo ambayo hata ukaguzi wa bila kutumia vifaa unayagundua.Tanzania imekuwa salama Kwa biashara za madawa chini ya wamu ya sita
Brother madawa yote hayatoki Tanzania hao wana connection kubwa kuliko unavyodhania muda mwingine anaenda kuyapokea kwa mtu aliyetoka nayo Brazil na akashuka Msumbiji au SA hata huko huko huko Uarabuni yaani makontena wanabadilishana mzigo..
 
Sio mwamba naunga mkono kuuza unga, mie niko kati kwa kati..
Wakati mwingine hawa wala unga wanajiingiza wenyewe, sidhani kama kuna mtu amemshikia mtu bunduki ale unga.
Unatakiwa upinge dawa za kulevya, usiwe katikati.
Hakuna anayemshikia mla unga bunduki ale ila wala wauza unga wanawashikia bunduki watu wanaopambana kuhakikisha watu hawali unga.
 
Yaan hizi mbuzi, na wasanii hawa Akina Chino, Nifah ,wale Ma DJ ,wasanii wanaojificha CCM.


Unajiuliza, huyu Chino kama kudensi Kuna Akina Iyobo wameanza kitamboooo, inakuaje kuaje??.

Kama uDJ unajiuliza, mbona MaDJ ni wengi sana, inakuaje MTU ana nyumba ya B 1+, Magari ya kifahari


Kiukweli kabisaaa kabisaaaa, Hapa Bongo, Sanaa ya Muziki, Filamu, Uchekeshaji, Biashara mitandaoni , Badoo haijafikia Hadhi ya kumpa MTU Nyumba za Mabilioni Kadhaa ,Magari ya mabilioni .

Badoooo, badooooo !!!.

Manina zao, wanatupa stress tukidhan tumechelewa kumbe ndo zao
Usiwasahau wachungaji wenu wa mwendokasi pia.
 
Yaan hizi mbuzi, na wasanii hawa Akina Chino, Nifah ,wale Ma DJ ,wasanii wanaojificha CCM.


Unajiuliza, huyu Chino kama kudensi Kuna Akina Iyobo wameanza kitamboooo, inakuaje kuaje??.

Kama uDJ unajiuliza, mbona MaDJ ni wengi sana, inakuaje MTU ana nyumba ya B 1+, Magari ya kifahari


Kiukweli kabisaaa kabisaaaa, Hapa Bongo, Sanaa ya Muziki, Filamu, Uchekeshaji, Biashara mitandaoni , Badoo haijafikia Hadhi ya kumpa MTU Nyumba za Mabilioni Kadhaa ,Magari ya mabilioni .

Badoooo, badooooo !!!.

Manina zao, wanatupa stress tukidhan tumechelewa kumbe ndo zao
Wanakupa stress ukiwafatilia maisha yao. Wewe ishi maisha yako huku ukipambana bila kusahau kumwomba Mungu afya njema na mafanikio
 
Nadhani bongo ukishakua maarufu kuna namna serikali inakulinda.

Wasanii wengi wabapush hizo zaga ila kwakua ni maarufu na wana pesa basi mamlaka zinawaacha tu.

Ila kajamba nani ukidakwa na kete mbili za kaya unasukumwa 30 yrs kama dogo wa mbeya.
 
Majuto ni mkukuu hao jamaa mtu akipita na sumu mara moja wanamfanyia uchunguzi sana kwa safari zingine akirudia tu hiyo njia hawasumbuki maana wanakua washamkagua kabla hajafika ndio maana hawatumii nguvu...
Ukisikia mtu anakwambia anauza Mchicha Ulaya jua ni sumu.
Oman hawanyongi kama China?
 
Lazima tu watu wakuchunguze na ukamatwe huwezi kuwaambia watu unapesa nyingi halaf unadai ni kuuza mchicha then utegemee watu wakuache😂
 
Back
Top Bottom