- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Yule Super Women aliyesema anauza Mchicha mpaka Ulaya Leo amekamatwa Oman na Kete 100 za unga.
- Tunachokijua
- Yupo mwanamke anayetambulika kama superwoman (Pendo “Open Kitchen”) ambaye amejizolea umaarufu kutokana na vipande vya video vinavyomuhusu yeye akiongelea namna alivyopata mafanikio kutokana na harakati zake ikiwemo kuuza mchicha online hadi mataifa ya nje ikiwemo Uingereza na Ujerumani. Tazama hapa
Madai
Kumekuwepo na kipande cha video kilichoambatana na taarifa kuwa superwoman amekamatwa na madawa ya kulevya Oman. Taarifa hiyo ikihusianishwa na mwanamke aliyejipatia umaarufu mitandaoni kwa kueleza kuwa pesa zake anazipata kwa kufanya biashara mbalimbali ikiwemo kuuza mchicha katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Taarifa iliyoambatana na video hiyo inajaribu kuonesha kuwa mwanamke huyo amekuwa akifanya biashara za madawa ya kulevya na hivyo amekamatwa. Tazama hapa na hapa.
Uhalisia wa video hiyo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa njia ya mtandao na google reverse image search umebaini kuwa video hiyo si ya hivi karibuni. Mttu mmoja aliweka kipande hiko cha video Julai 29, 2023 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram bila kuweka maelezo yoyote yale. Tazama hapa
Ufuatiliaji zaidi umebaini tovuti kadhaa ziliripoti ikiwemo tovuti ya Legit ambayo ilichapisha taarifa Februari 5, 2021 yenye kichwa cha habari “Video inaonesha akiwa na dawa za kulevya zilizojazwa chini ya wigi, maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wapigwa na butwaa”. Katika Taarifa hiyo walieleza namna tukio hilo lilivyotokea katika uwanja mmoja wa ndege na hali iliyokuwa ikionekana katika tukio hilo ingawa hawakueleza zaidi.
Tovuti nyingine inayojulikana kama Justnaija ilichapisha taarifa iliyoambana na video hiyo tena Julai 23, 2023`ilielezea pia tukio hilo inagwa na wao pia hawakueleza tukio hilo limetokea wapi na ulikuwa ni uwanja upi wa ndege.
Hivyo video hiyo si ya hivi karibuni kama ilivyosambaa zaidi katika mitandao mbalimbali ya kuanzia Februari 21, 2025. Pia hakuna uthibitisho wa kuwa video hiyo inamuhusu Mtanzania.