Video: Angalia Bodaboda alivyogongwa na Mwendokasi

Umetumia hisia hapa,ila ukweli ni kwamba dereva wa mwendokasi hapo hana makosa
mkuu hisia gani kwani ile intersection anatakiwa aiheshimu bodaboda peke ake na ndicho wanachofundisha driving school, bodaboda wana hatia kila ajali ikitokea na mbele pale uelekeo wa mwendokasi pana pundamilia kivuko cha watembea kwa miguu unataka unambie yule mwendokasi alipaheshimu, sawa mimi nimesema madereva wa mwendo kasi bila kutumia utu hadi anastaafu ashaua bodaboda 20, miundombinu yetu sio salama.
 
bosi nani kamalaumu dereva wa mwendokasi nimesema watumie busara na utu, sababu hii miundombinu ya treni za mataili ina mapungufu usiiishie kumsema bodaboda utakuta huyo boda siku nzima anafanya kazi akili inachoka msiishie kuwalaumu hawa watu ni ndugu zetu wametoka kwenye familia zetu eti pombe, nani hanywi pombe madaktari au kwani hawafanyi upasuaji.
 
Hawa ndugu zetu boda boda
🤔🤔🤔🤔🤔🤔
Boda ni watanzania Wenzetu, baadhi yao, na wenzao bajaji, sioni kama ni wakuhurumia, wao wanajari kuwahi kuliko Usalama wao na wa wenzao barabarani.
.
.Juzi nipo kwenye kigari changu, kwenye kituo cha daladala nimepungaza mwendo, akaja kukivaa kigari changu, nyuma, gari imebondeka sana bampa na shavu la kushoto, maana alipoanguka pikipiki iliilaria gari.

.Ila kwa saidiwa na boda wenzi, walinyua pikipiki chapu akakimbia, bodaboda wengine wakabaki wanacheka na kebehi, hii haina kesi hii. Nikaona uzuri wa kutotembea na silaha mda mwingine, maana shetani alishanituma vibaya pale.
.
.
 
Mungu anisamehe kwa mitizamo yangu na kutokuijua kwangu kesho ila Kila nkiona abiria na boda boda wake naona ni kama watu flan hawana akili wote
Bodaboda akiwa kwenye pikipiki akili yote inahamia matakoni. Unakatishaje barabara na spidi yote hiyo, huangalii huku wala kule we ni spidi tu. Haki yake
 
Kwanini usimwambie apunguze speed au alikupa lift ukaogopa kusema??
 
SIa
SIJAKUELEWA KOSA LA MWENDO KASI NI LIPI HAPO, HILI NENO TUAACHE WANATAFUTA MKATE, TUAACHE NI WAPIGA KURA, NDILO LINALOHARIBU MAMBO MENGI.
KUTOKANA NA TABIA HII, NDIYO MAANA WATU WANAFANYIA BIASHARA BARABARANI, BODA BODA WENYEWE NA WENZAO BAJAJI, KUNA MAENEO WANASUBIRIA ABIRIA NDANI YA BARABARA.
MFANO: UKITOKA UBUNGO KWENDA KIBAHA, STOP OVER, KIMARA SUKA. TEMBONI, OFISI ZA MKUU WILAYA UBONGO, NIMEPASAHAU JINA, KIBAMBA CHAMA.

HIVYO VITUO DALADALA ILA BODA NA HASA BAJAJI HUFANYA VITUO VYA KUANZIA KAZI.

UKIJA MBAGALA PALE ZEIKEM KIMEKUA KITUO CHA BAJAJI, MBAGARA HAPO HAPO UKITOKEA KONGOWE, PALE DARAJANI BIASHARA ZINAPANGWA BARABARANI KABISAA, NI BARABARA YA NJIA MBILI ILA INATUMIKA MOJA, NYINGINE INAPANGWA BIASHARA.
WAACHWE SABABU WANATAFUTA MKATE, WAACHWE SABABU NI WAPIGA KURA, SIKU AJALI IKITOKEA TUWALAUMU MADEREVA.
 
Mwenyewe nilikuwa naangalia hali ya usalama mbele, endapo ningeona hali ya hatari ningemshtua fast.

Pia nilitaka kufika mapema nilikokuwa naenda
Kwa scenario kama ya hiyo ajali unadhani abiria na dereva wake hawakua wanaangalia hali ya usalama??

Ajali mara nyingi huwa haionekani ni vuup chuma iko down watu mshafikia tamati ya maisha yenu.

Sasa wewe hiyo kusubiri uone hatari ndo umstue na ukimstua na yeye akubali au akate huo ushauri wao si tayari mko mochwari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…