Video: Angalia Bodaboda alivyogongwa na Mwendokasi

Video: Angalia Bodaboda alivyogongwa na Mwendokasi

Mungu anisamehe kwa mitizamo yangu na kutokuijua kwangu kesho ila Kila nkiona abiria na boda boda wake naona ni kama watu flan hawana akili wote
Usiseme hivyo mkuu kuna emergency ...
Mfano mimi nimejenga mpiji magohe kuna muda huwa barbara ni mbovu huwezi toka na mkweche wako au panda daladala option unayobaki nayo ni bajaj or bodaboda
Kufika mbezi kwa uhakika ni Boda tu hapo unakwepaje?
 
Mwendo kasi ilikua imechanganyia hadii injini inapiga mluzi.
Shida ya Hawa madereva wa mwendokasi hawana uendeshaji wa kujihami. Kipande cha kuanzia Kivukoni mpaka Faya pale shuleni Jangwani ni kipande hatari ambacho kina pilika pilika nyingi, hivyo ni busara mwendokasi waendeshe kwa spidi ndogo na kwa umakini mkubwa.
 
mkuu hisia gani kwani ile intersection anatakiwa aiheshimu bodaboda peke ake na ndicho wanachofundisha driving school, bodaboda wana hatia kila ajali ikitokea na mbele pale uelekeo wa mwendokasi pana pundamilia kivuko cha watembea kwa miguu unataka unambie yule mwendokasi alipaheshimu, sawa mimi nimesema madereva wa mwendo kasi bila kutumia utu hadi anastaafu ashaua bodaboda 20, miundombinu yetu sio salama.
Boda wakati anaingia main road alipaswa atulie km dk 1 kucheck. Ye kanyookea.

Zebra pia wabongo mpk tuone traffic 😂
 
Boda wakati anaingia main road alipaswa atulie km dk 1 kucheck. Ye kanyookea.

Zebra pia wabongo mpk tuone traffic 😂
Hahahaa.....Ukiwa mstarabu ukasimama wale.wa nyuma yako hizo honi utapigiwa mpaka unashangaa tena Trafic light ziko- RED

Africa kuna shida kubwa sana
 
Bodaboda wangekatazwa kuingia mjini wasilete siasa watawamiza vijana yaan wanapita kwenye njia mwendo kasi kama yao
 
Madereva wote vichomi hapo.

Hao wa mwendokasi waache kujiona wanaendesha treni.
 
Boda ni watanzania Wenzetu, baadhi yao, na wenzao bajaji, sioni kama ni wakuhurumia, wao wanajari kuwahi kuliko Usalama wao na wa wenzao barabarani.
.
.Juzi nipo kwenye kigari changu, kwenye kituo cha daladala nimepungaza mwendo, akaja kukivaa kigari changu, nyuma, gari imebondeka sana bampa na shavu la kushoto, maana alipoanguka pikipiki iliilaria gari.

.Ila kwa saidiwa na boda wenzi, walinyua pikipiki chapu akakimbia, bodaboda wengine wakabaki wanacheka na kebehi, hii haina kesi hii. Nikaona uzuri wa kutotembea na silaha mda mwingine, maana shetani alishanituma vibaya pale.
.
.
Boda wanateteana ujinga aiseeee
Pole mkuu maana hapo ni ghalama umeingia kunyoosha
 
Kwenye sekta ya udereva kuna ktu kinaitwa "UDEREVA WA KUJIHAMI"....ukiangalia kwa makini apo kuna watu wawili walikuwa wanajiandaa kuvuka wakisubiri mwendokasi kwanza ipite......

Sema sku ikifika imefika
 
Back
Top Bottom