and 100 others
JF-Expert Member
- Feb 3, 2023
- 4,515
- 14,999
Hawa askari kama baadhi wapo, najua wamezeeka sasa, hawana nguvu tena na wanajutia hadi mwisho wa maisha yao hapa duniani.
Inawezekana kutokana na tamaa za mali, kujipendekeza kwa wakubwa ilipelekea kufanya kitendo hiko cha kikatili.
Hata mwisho wa Mobutu hukuwa mzuri, ndipo utajua Mungu ni fundi..
Historia imeonyesha mara nyingi vyombo vya dola hufuata amri za watawala, lakini baadaye huonekana kama wahusika wa dhuluma, huja kuandikwa vibaya katika historia na kulaaniwa na vizazi vijavyo.
Leo hii Patrice Lumumba tunamkumbuka kama shujaa.