Video: Askari Watiifu Kwa Mobutu Wakimkamata, Kumpiga na Kumtesa Patrice Lumumba 1960

and 100 others

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2023
Posts
4,515
Reaction score
14,999

Hawa askari kama baadhi wapo, najua wamezeeka sasa, hawana nguvu tena na wanajutia hadi mwisho wa maisha yao hapa duniani.

Inawezekana kutokana na tamaa za mali, kujipendekeza kwa wakubwa ilipelekea kufanya kitendo hiko cha kikatili.

Hata mwisho wa Mobutu hukuwa mzuri, ndipo utajua Mungu ni fundi..

Historia imeonyesha mara nyingi vyombo vya dola hufuata amri za watawala, lakini baadaye huonekana kama wahusika wa dhuluma, huja kuandikwa vibaya katika historia na kulaaniwa na vizazi vijavyo.

Leo hii Patrice Lumumba tunamkumbuka kama shujaa.
 
Walimkosea sana Patrice Lumumba hawa watu leo hii watakuwa ni wazee ila kwa macho yao wanaona Congo ilivyoharibika hakuna la maana Mobutu alilofanya zaidi ya kuendekeza anasa na uchawi.Hata majumba ya kifahari aliyojenga yamebaki magofu.
 
View attachment 3346586

Jamaa aliacha laana, ya milele
 
Walimkosea sana Patrice Lumumba hawa watu leo hii watakuwa ni wazee ila kwa macho yao wanaona Congo ilivyoharibika hakuna la maana Mobutu alilofanya zaidi ya kuendekeza anasa na uchawi.Hata majumba ya kifahari aliyojenga yamebaki magofu.
Cha ajabu utakuta leo wanaoteseka ni familia, wajukuu, ndugu za hao askari waliofanya huo unyama.
utakuta ndugu zao wengine wanakufa kwa magonjwa, vita na njaa kama ujuavyo yanayoendelea Congo.
 
Patrice Lumumba (1925–1961) alikuwa kiongozi wa harakati za uhuru wa Kongo na Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo baada ya kupata uhuru kutoka kwa Ubelgiji tarehe 30 Juni 1960.

Alikuwa mwenye msimamo mkali dhidi ya ukoloni na utawala wa kigeni, na hivyo akawa mwenye maadui wengi, ikiwa ni pamoja na serikali za Magharibi na makabila yaliyogawanyika ndani ya Kongo.

Baada ya miezi michache tu ya uongozi, Lumumba alikumbana na mzozo wa kisiasa na kiaskari, na hatimaye alikamatwa na jeshi la Joseph-Désiré Mobutu mnamo Desemba 1960.

Lumumba alihamishwa kwa nguvu hadi Katanga, mkoa uliokuwapo chini ya utawala wa Moïse Tshombe aliyeunga mkono wa Ubelgiji na makampuni ya kigeni.

Mnamo 17 Januari 1961, Lumumba aliuawa kwa pamoja na wafuasi wake wa karibu, Maurice Mpolo na Joseph Okito. Mauaji yalifanyika kwa siri na kushirikiana kwa vikosi vya Katanga na wafanyakazi wa kiserikali wa Ubelgiji, kama ilivyodhihirika baadaye katika uchunguzi wa kimataifa.

Kifo cha Lumumba kilisababisha ghasia kubwa duniani na kumfanya kuwa mlingwa (icon) wa harakati za ukombozi barani Afrika.

Miaka mingi baadaye, Ubelgiji ilikiri jukumu lake la kihistoria katika mauaji hayo na kuomba msamaha mwaka 2002.

Lumumba anaheshimiwa kama shujaa wa kitaifa nchini Kongo na kama mwanasiasa aliyepigania haki za Waafrika dhidi ya ukoloni.
 
Aisee kama huyo askari aliyempiga na bunduki ya mgongo sijui waliahidiwa nini mana alimpiga nayo kama kuni kwa nguvu zote mpaka Lumumba akajikuna mgongo 🥲🥲
 
Cha ajabu utakuta leo wanaoteseka ni familia, wajukuu, ndugu za hao askari waliofanya huo unyama.
utakuta ndugu zao wengine wanakufa kwa magonjwa, vita na njaa kama ujuavyo yanayoendelea Congo.
Utakuta wanalalamikia kutokulipwa madai na stahiki mbalimbali za kimaslahi kipindi wakiwa kazini.
 
Aisee kama huyo askari aliyempiga na bunduki ya mgongo sijui waliahidiwa nini mana alimpiga nayo kama kuni kwa nguvu zote mpaka Lumumba akajikuna mgongo 🥲🥲
Na bunduki ni chuma na ni nzito, hivyo ilimuumiza..
Kuna mwingine hapo akaja kwa nyuma akampiga ngumi kichwani sijui ni kofi kwa nguvu...

Inasikitisha sana, kama katika kumkamata tu walimtesa hivyo imagine walikompeleka walimtesa kiasi gani...
 
La mwisho kabisa hao askari walikufa masikini kimmbwa kabisa nao
 
kifo cha PATRICE LUMUMBA huwa kinaniuma roho kama vile nilikuwepo, ilhali kilinizidi miaka 30 na kadhaa tangu afe. huko alipo MUNGU amuweke mahali pa RAHA na STAREHE MILELE, kwakua alikua MZALENDO wa KWELI.
 
Back
Top Bottom