Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Je huyu Jaji "Y" ni nani? Na Je huyu Tapeli "Z" ndiye Alex Msama au Mushi?
Haya wataalamu wa mambo ya ARDHI tufungulieni codes.
---
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuwa ameandika barua kwenda kwa Waziri wa Katiba na Sheria kufuatia jaji mmoja wa mahakama kukiuka kanuni za taaluma.
Waziri Silaa akihitimisha hoja ya bajeti yake bungeni amesema kuwa mwaka 2015 jaji huyo alikuwa wakili, na akamsaidia tapeli mmoja kuchukua ardhi ya watu.
Amesema warithi wa aliyetapeliwa walipoenda makamani hivi karibuni, wamekuta wakili yule sasa ni jaji, bado akaamua kwa kumnufaisha tapeli.
Amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, na kwamba jambo hilo amelichukua yeye ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na haki inapatikana.
Credit: TBC