VIDEO: Diamond na Nandy waitwa TCRA, hivi ndivyo ilivyokuwa

VIDEO: Diamond na Nandy waitwa TCRA, hivi ndivyo ilivyokuwa

MumbaZ

Senior Member
Joined
Jan 28, 2018
Posts
133
Reaction score
124
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz na Faustina Charles maarufu kama Nandy, mapema leo hii wamewasili katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kufuatia kusambaa mitandaoni kwa video zao wakiwa faragha zilizodaiwa kukosa maadili.

Hata hivyo hivi karibuni Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Harrison Mwakyembe aliagiza kukamatwa kwa wasanii hao kwa ajili ya upelelezi kisha kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili ya kukiuka maadili na kusambaza video hizo chafu.

Tazama Video hapa chini ikionesha Diamond na Nandy wakiwasili TCRA.

Diamond akijitetea na Kuomba msamaha

======

Wasanii wa bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’na Faustina Charles ‘Nandy’ wamewasili katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Wasanii hao wanaitikia wito wa TCRA ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa kwa video zao zinazokiuka maadili.

Nandy aliwasili TCRA saa 5:48 asubuhi leo Aprili 19 na Diamond aliwasili saa 6:15 mchana. Diamond alisindikizwa na menejimenti yake ikiongozwa na Said Fella.

Hivi karibuni, Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe alizungumza bungeni kuwa wasanii hao walikamatwa na kuhojiwa kuhusu kusambaa kwa video zinazokiuka maadili.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kuwahoji wasanii hao.
 
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz na Faustina Charles maarufu kama Nandy, mapema leo hii wamewasili katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kufuatia kusambaa mitandaoni kwa video zao wakiwa faragha zilizodaiwa kukosa maadili.

Hata hivyo hivi karibuni Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Harrison Mwakyembe aliagiza kukamatwa kwa wasanii hao kwa ajili ya upelelezi kisha kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili ya kukiuka maadili na kusambaza video hizo chafu.

Tazama Video hapa chini ikionesha Diamond na Nandy wakiwasili TCRA.

Sasa TCRA ndio Mahakamani...au kuna wanaopelekwa Mahakani na wanaopelekwa TCRA kwa kosa hilo hilo!!
 
Dar es Salaam. Wasanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Faustina Charles ‘Nandy’ wamehojiwa kwa saa mbili na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Wakizungumza mara baada ya kumaliza mahojiano hayo yaliyofanyika leo Aprili 19, wasanii hao wamesema wamejifunza mengi kuhusiana na masuala ya mitandao.

Diamond amesema: “Ujana ni maji ya moto tumeelimishwa, hatutarudia tena, nitakuwa balozi kwa vijana wenzangu kuhusu masuala ya mitandao.”

Nandy amesema: “Nisameheni kwa yaliyotokea. Hapa TCRA nimepata somo kuhusu mitandao, tukio lile halitajirudia tena.”

Chanzo: MCL
 
Kweli Wabongo tunapenda umbea kuliko vitu vya maana!
Sio kwa wingi wa kamera hizo;
 
Massa mawili kuongelea upuuzi!
Sasa sheria zina kazi gani?
 
Bqhqti yao sio wa lile kundi jingine. Walitakiwa wapimwe mkojo na kuonesha vyeti vya kuzaliwa vya kwao, vya wazazi wao, na vya babu na bibi zao. Kudadadeki.
 
Wamefanya vizuri kuomba samahani. Binadamu wote tunakosea muhimu ni kukubali na kujirekebisha.
 
Diamond kweli star sio kwa macamera hayo. Umaarufu kweli mbaya kitu kidogo kinakuuzwa.

Diamond usirudie tena jaman
 
Diamond kweli star sio kwa macamera hayo. Umaarufu kweli mbaya kitu kidogo kinakuuzwa.

Diamond usirudie tena jaman
mkuu siku hizi habari hakuna ..umeona makamera yaliyokuwepo kwenye press ya young killer wakati anatambulishwa kuingia mkataba na kampuni ya wanene""??
binafsi nilichoka
 
Back
Top Bottom