The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
View: https://youtu.be/Gl_enK_qbVg?si=XGMbUj8hTJxGpgyp
➡Hatimaye matunda ya kilichofanyika Dodoma tarehe 19/01/2025 kwa Bi Samia Suluhu Hassan kujiteua mgombea u - Rais huku akimwingiza kwenye mkumbo huo Dr Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza wake, yaanza kujidhihirisha na kupingwa waziwazi..
➡Mzee Malisa (mwanachama mtiifu na mwaminifu wa CCM) ktk video hii, hajajificha bali kajitokeza waziwazi na kusema Samia na wenzake walikosea, walivunja katiba ya CCM na ya nchi kwa kujiteua kuwa wagombea u - Rais huko Dodoma na kutumia "mamlaka yake ya U - Rais" kuu - blackmail mkutano kinyume cha taratibu na kanuni za chama kujilazimisha kuwa wagombea u - Rais...
➡Mwisho kwa sbb ya kusimamia uvunjaji wa katiba na kanuni za CCM pamoja na katiba ya nchi, amemtaka Bi Samia Suluhu Hassan kujiuzuru mara moja nafasi ya uenyekiti wa CCM taifa kwa sababu hafai tena kuendelea kukiongoza chama hicho...
Tazama na sikiliza mwenyewe video hiyo..
=================================================
UPDATES
View: https://youtu.be/cdJ4Q93Z8fs?si=SJVuJalArjU24R0N
☝🏻☝🏻☝🏻AMEFUKUZWA UANACHAMA WA CCM kwa madai ya kupinga maamuzi ya mkutano mkuu!!
Yametimia. Kumbe huyu mzee ni mchungaji wa kanisa huko mkoani Kilimanjaro na aliwahi kugombea nafasi ya uenyekiti CCM Taifa...
Tayari ameshafukuzwa uanachama wa CCM na sababu eti ni kukosoa maamuzi ya mkutano mkuu wa CCM uliompitisha Bi Samia Suluhu Hassan na Dr Emmanuel Nchimbi kuwa wagombea u - Rais mwaka huu 2025..
Yajayo yanafurahisha