Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Kila anapokwenda Na kutua katika ardhi ya Nchi hii Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Amekuwa akilakiwa na kupokelewa kwa mafuriko makubwa sana ya watu ambao hujitokeza na kumiminika kwa wingi sana kama mchanga wa baharini.
Hii ni kutokana na kupendwa , kukubalika na kuishi katika mioyo ya mamilioni ya watanzania ambao wanaendelea kumuunga mkono Mama kwa nguvu zao zote. Kutokana na kazi kubwa aliyoifanya katika kuwainua watanzania na kuwaletea maendeleo ya haraka zaidi kuliko ilivyo tazamiwa na kutarajiwa.
Embu fikiria ndani ya muda mfupi amekamilisha ujenzi wa Bwawa la mwalimu Nyerere lenye kuzalisha megawati 2115, ujenzi wa reli ya kisasa na kuanza kutumika kusafirishia abiria ,kuongeza mapato kwa mwezi kufikia zaidi ya trilioni mbili, kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja,kujenga na kusogeza huduma za kijamii karibu kabisa ya wananchi.
Kutoa Elimu Bure hadi kidato cha sita ambapo serikali inatoa zaidi ya Billion 33 kila mwezi kugharamia au kubeba mzigo wa kuwasomesha watoto wa watanzania ili wapate Elimu na kutimiza ndoto zao,kutoa ajira kwa Maelfu kwa Malaki. Kusambaza huduma za umeme mpaka vitongojini huko, kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma.
Kujenga vituo vya afya zaidi ya 300 Nchini Kwote ,kuboresha huduma za afya kuanzia ngazi za msingi huko hii ni baada ya kutiririsha zaidi ya Trilioni sita katika secta ya afya pekee. Kudhibiti mfumuko wa bei hususani wa bei za vyakula,kuboresha mazingira ya biashara,kukuza na kuimarisha Demokrasia hapa Nchini na mengine mengi sana.
Hii ndio maana Rais wetu Mpendwa anaendelea kuiteka mioyo ya mamilioni ya watanzania na kupokewa kwa kishindo sana kila apitapo. Lakini pamoja na mapokezi makubwa ambayo RAIS wetu huyapata. Kwangu mimi Morogoro inaendelea kushikilia rekodi ya mapokezi makubwa sana ambayo Rais wetu aliyapata.
Yalikuwa ni mapokezi ya kihistoria,mapokezi ya kishindo ,heshima na kishujaa kwa shujaa wetu wa Afrika na jasiri muongoza njia Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Embu Tazama Mwenyewe hapa.
Pata burudani hii pia kuifanya wikendi yako iwe njema na kumshukuru Rais Samia kwa kufanya Taifa na watanzania kuwa wenye tabasamu katika nyuso na mioyo yao.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.