POTOSHI Video hii ni maandamano ya wananchi Kenya wakimuonya Rais Ruto kuongeza muda wa uongozi

POTOSHI Video hii ni maandamano ya wananchi Kenya wakimuonya Rais Ruto kuongeza muda wa uongozi

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

1758612610390.png
 
Tunachokijua
William Ruto ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amekuwa Rais wa tano wa taifa hilo kuanzia tarehe 15 Septemba, 2022. kumekuwepo na madai yanayomuhusisha Rais Ruto juu ya kutaka kuongeza ukomo wa muda wa uongozi. Kwa mujibu katiba ya Kenya Rais anaruhusiwa kuchaguliwa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Awali kilisambazwa kipande cha video mtandaoni kikimuonesha Rais Ruto akisema "As the President i will be at the front to change term limit." (“Kama Rais nitakuwa mstari wa mbele kubadilisha ukomo wa muhula.”) huku zikisikika sauti za watu wakishangilia kwa kupiga makofi. Lakini baada ya ufuatiliaji wa JamiiCheck ilibainika video hiyo ilipotoshwa uhalisia kwa kukata na kuunganisha vipande visivyo husiana.

Katika video halisi Akizungumza Ikulu ya Kenya Novemba 16, 2022 Rais Ruto alisisitiza kuwa atakuwa mstari wa mbele katika kuzuia mabadiliko yoyote ya kikatiba kubadili ukomo wa mihula ili kunufaisha watu binafsi.

Sasa kumekuwepo na kipande cha video kilichochapishwa katika mtandao wa TikTok na kudaiwa kuwa ni maandamano ya wananchi jijini Nairobi nchini Kenya wakimuonya Rais Ruto kuongeza ukomo wa muda wa uongozi.


Je, ni upi uhalisia wa kipande hicho?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaini kuwa video hiyo iliwahi kuchapishwa mtandaoni tangu mwezi Juni 2025. Pia katika video hiyo linaonekana jengo lenye maneno "NAKURU SALES AND SERVICE CENTRE" jambo linaloashiria uwepo wa jengo hilo katika mji wa Nakuru na si Nairobi.

Aidha kupitia Google Earth imebainika kuwa eneo la video ni kutoka kaunti ya Nakuru, barabara ya Mburu Gichua. Hivyo matumizi ya video hiyo na kudai kuwa ni maandamano jijini Nairobi ni kupotosha uhalisia.
​
1758615756889-png.3477681
Back
Top Bottom