- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran, huku shambulio la kwanza likiripotiwa kutokea karibu na ofisi za Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei. Vyombo vya habari vya Iran viliripoti mashambulizi katika maeneo mbalimbali nchini humo, huku moshi ukionekana ukifuka kutoka katika mji mkuu, Tehran.
Madai
Kumewepo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikiambatana na ujumbe ambao unasema 'Majasusi wa Israel walipuliwa wakijiandaaa kutekeleza Ugaidi nchini Iran'
Uhalisia
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck, umejiridhisha kuwa video hiyo haihusiani na vita vinavyoendelea kati ya Iran na Israel kwani kupitia Google Reverse Image Search imebainika kuwa video iliwahi kuchapishwa katika mtandao wa Instagram Mei 07, 2020 na ukurasa wa lorestan_todayy ambapo iliambatanishwa na ujumbe uliosema "
"Video inaonyesha shambulio la mizinga lililofanywa na kundi la Hashid al-Sha'abi dhidi ya mkusanyiko wa wapiganaji wa kundi la kigaidi Islamic State of Iraq and the Levant, pamoja na wakati ambapo kombora la mortar lilipiga shabaha moja kwa moja. Inaripotiwa kuwa angalau wanachama 20 wa ISIS waliuawa katika shambulio hilo."