- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimeona video inayosambaa ikimuonesha kuku ameruka kutoka ghorofa moja hadi lingine huku watu wakisema kuwa kuku akiacha uvivu anaweza kufanya hivyo. Je, hii ni kweli?
- Tunachokijua
- Kuku ni kwa lugha ya kitaalamu hufahamika kama Gallus gallus, Kuku ni miongoni mwa ndege wafugwao majumbani kwa ajili ya nyama na mayai. Kuku wamekuwa wakiruka mara kadhaa wakikutana na hatari mbalimbali ama kwa mitetea huruka juu kupambana na kunguru wanaotaka kuchukua vifaranga.
Mdau wa JamiiCheck amehitaji kupata uhalisia wa kipande cha video kinachoonesha kuku akiruka kutoka ghorofa moja hadi lingine kama ni halisi au imehaririwa. Kipande hiko cha video kimekuwa kikiambatana na jumbe tofauti zikieleza kuwa kuku ana uwezo wa kufanya hivyo lakini amekuwa ni mvivu.
Uhalisia wa video hiyo upoje?
JamiiCheck.com imefutilia uhalisia wa video hiyo ambayo ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa mwezi wa 12,2024 huku ikiambata na jumbe mbalimbali kuonesha kuwa kuku ana uwezo wa kuruka kwa umbali mrefu kama inavyoonekana kwenye video hiyo.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imehaririwa kwa kuunganishwa vipande viwili tofauti na hivyo kupotosha uhalisia wake. Kupitia fuatiliaji wa njia ya mtandao tumebaini uwepo wa video hiyo mtandaoni katika nyakati tofutitofauti.
Kipande hiko cha video kimehaririwa kwa kuwekwa video mbili ya kwanza ikimuonesha kuku akilazimishwa kuruka na kisha kuruka hii ni kuanzia sekunde ya 00 hadi sekunde ya 08 na sekunde zilizofuatia zinamuonesha njiwa akiruka. Lakini pia namna ya urukaji wa kuku haifanani na namna ya ndege ayetua upande wa pili kwani kuku hana uwezo wa kuelea hewani na kutua kwa utulivu wa namna ile.
Kupitia ufuataliaji wa makala mbalimbali zinabainisha kuwa Kuku wana uwezo wa kuruka juu lakini si kama ilivyo kwa ndege wengine na hii ni kwa sababu hawaitaji kuruka juu ili kuyaendesha maisha yao, hawahitaji kujenga viota juu ya miti ama kuwinda mawindo ya angani kama ilivyo kwa ndege wengine.
Makala ya tovuti ya Grubbly farm inaendelea kueleza kuwa muundo wa mabawa ya kuku umebuniwa kwa ajili ya mwendo wa kasi wa muda mfupi. Hawahitaji kuruka mbali, kuelea angani, au kubaki wakining’inia wanaporuka. Sio tu kwamba mabawa ya kuku yameundwa kwa ajili ya kuruka kwa muda mfupi, bali pia misuli yao haijaimarika vya kutosha kudumu katika safari ndefu za kuruka.
Lakini pia Kuku wana uwezo wa kuruka wima kuelekea juu vizuri zaidi kuliko kudumisha mtindo wa kuruka kwa usawa wa sakafu. Hii inamaanisha kwamba wanaweza kuruka hadi kwenye viota vilivyo futi 10 au 15 kutoka ardhini, lakini huenda wasiweze kuruka usawa wa ardhi kwa zaidi ya futi moja au mbili. Ingawa Baadhi ya aina nyepesi za kuku zinaweza kuruka hadi urefu wa futi 30 juu
Kwa mujibu wa BBC wildlife rekodi ya kuku aliyeruka juu kwa muda mrefu inashikiliwa na kuku aliyetumia sekunde 13 kwa umbali wa mita 92, huo ulikuwa mruko mmoja mkubwa kwa aina ya kuku.