Mzee Nyerere
JF-Expert Member
- Jun 24, 2024
- 219
- 279
Tunaweza kubishana juu ya mambo mengi ila hatuwezi kubishana juu ya utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo unaofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mtakubaliana na Mimi kuwa Mradi huu uliwashinda akina Mzee Julius Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete hata John Pombe Magufuli wakati anafariki akiwa madarakani kwa miaka zaidi ya mitano aliutekeleza kwa 35% tu,
Maajabu ni haya, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka mitatu tu kazi IMEKWISHA mnadhani kwanini Watanzania tusimpongeze Mama na kumtia moyo kuelekea 2030?