Video: Hizi drones Bayraktar TB2 za Uturuki ni shida, Waafrika tutafika lini huku?

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Jamaa wameketi ofisini kazi yao kubonyeza bonyeza na kuondosha vifaru utadhani video game, Waafrika tumejiandaaje kwenye utaalam kama huu au bora liende tu.

Halafu tatizo hizi drone sio rahisi kuzigundua kwa radar, jamaa anachagua kifaru kipi amekichukia kwenye msafara wa Warusi anabonyeza na kukiondosha.

Haya mambo husababisha nihisi huruma kwa ajili ya bara letu Afrika, huku hakuna taifa hata moja lenye manowari/sub-marine, aina ya utaalam wa enzi za akina Hitler hatujaufikia, kazi yetu ni wajeda kupasua matofali kwa kichwa siku za maonyesho tunashangilia na kujiona wababe.

 
shida muendelezo wa hizo drone itakua ngumu maana walikua na makubaliano ya kununua engine zake kutoka ukraine..........sasa nchi ya supplier wa engine ndo ametandikwa..........................
 
Russia aliingia kichwakichwa na vifaru vyake ameona moto wa Ukraine &allies🤔

Halafu mabango ya barabarani yamepotoshwa, hivyo hajui hata pakutokea...
 
Hivi ndivyo wajuvi wa mambo hayo walivyoichambua video clip hiyo inayodai hiyo drone imeharibu mamia ya vifaa vya Russia.

View attachment 2152684


Mbona sijaona tatizo lolote kwenye huo uchambuzi, vita vyenyewe vimeendelea wiki kadhaa sasa, kwa hivyo huo uwezekano upo.
Au unaongea kuhusu huyo aliyejibu hapo anaitwa "Tarski", jina lake tayari limemsaliti.
 
Mbona sijaona tatizo lolote kwenye huo uchambuzi, vita vyenyewe vimeendelea wiki kadhaa sasa, kwa hivyo huo uwezekano upo.
Au unaongea kuhusu huyo aliyejibu hapo anaitwa "Tarski", jina lake tayari limemsaliti.
Huweziona tatizo kwa kuwa hushirikishi ubongo.

Unaambiwa kwanza footage sio Ukraine, pia hata kama ingekuwa Ukraine, ingehitajika drones takriban 50 kufanya mashambulizi hayo (kuharibu mamia ya vifaa vya Russia). Wakati drones hizo walizokuwanazo ni takriban 20. Na nyingine jana zimeharibiwa na Russia.

Sasa kama kweli zinawasaidia, mbona Ukraine yoote hakuna sehemu salama?! Popote pale Russia akitaka kufanya mashambulizi anashambulia. Na haya ni maelezo ya serikali ya Ukraine.

 

Wapi huyo mchambuzi amesema hiyo sio Ukraine, wewe nawe unalazimisha na kumlisha maneno, pili yeye hapo alikua anaongea kuhusu shughuli ya siku mbili, ila wote tunafahamu hii shughuli imechukua wiki kadhaa sasa.....
 
Hapa ndio imedhihirisha nini haswa, hamna mtu aliyetaja idadi kamili ya vifaru vilivyoliwa shaba, Ukraine wanaendelea kuviondosha moja baada ya kingine, pia wakitumia na zile javelin....
ushapata githeri na avocado baada ya kazi nzito ya kutikisa mbuyu??????????au ndo hata mahindi umeishiwa
 
Wapi huyo mchambuzi amesema hiyo sio Ukraine, wewe nawe unalazimisha na kumlisha maneno, pili yeye hapo alikua anaongea kuhusu shughuli ya siku mbili, ila wote tunafahamu hii shughuli imechukua wiki kadhaa sasa.....
Kasome tena screen shot, acha wenge...

Alfred kasema: Footage mostly not from Ukraine at all. USELESS CLIP
 
Kasome tena screen shot, acha wenge...

Alfred kasema: Footage mostly not from Ukraine at all. USELESS CLIP

Huyo Alfred ametoa comment kwa mwenzake, hajachambua, hivyo kwako wewe one sentence comments zimekua uchambuzi, mpo very desperate ila ndio hivyo, Mrusi amewaingiza kwenye aibu sana mliokua mnamtegemea, hata Waarabu wale wamiliki wa dini ya "amani" raundi hii wapo kimya maana nguvu na jeuri yao siku zote ilikua Urusi na ndiye huyo ameonyesha udhaifu mkubwa sana, mumebaki maustadhi wa Bongo ndo mnabwatuka na kutukana kwenye mitandao.
 
Alfred anaijua vema Ukraine, kama ambavyo mie ninavyoijua Tanzania. Ukiniletea video clip ya Sudan ukanambia ni Tanzania nitakushangaa, na kukwambia 'hiyo (mazingira hayo) siyo Tanzania, video clip hiyo ni UPUUZI'. Sentensi moja tu lakini nimeshamaliza kila kitu.

We upo zako hapo Uthiru wapiga sukuma wiki, wala Ukraine huijui, halafu wajitia kubishana na wanaoyajua mandhari ya Ukraine.
 
Asikupotezee muda huyo mkenya njaa inamsumbua.......hapo kapewa kibarua cha kumtetea bwana wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…