Video: Huyu kama ni mkeo utamfanyaje?

Huyo mume hela Hana hapo hata sofa wala godoro hajanunua.
Kuna ndoa zinakufa kwa kuiga vitu kutoka nje. Na hata kama unaomba ushauri hakikisha unayemuomba ushauri ana ndoa kama yako na ana maisha kama yako. Kuna jamaa mke alikuwa anamsumbua kaka yake akamshauri awe anamshtua akili(anampiga makofi) mara moja moja. Hajui kuwa kaka yake ni tajiri na mkewe ni mama wa nyumbani. Yeye ana biashara ya duka na mkewe ni mtoto wa Jaji. Ile jamaa kumpiga mke kofi moja tu ndoa ikaisha. Jamaa amehangaika mpaka kwa maaskofu kusuluhisha. Mke washaondoka na watoto. Tusiige, ukikaa na mtu anakunywa naye bia unaona ni mwenzako kumbe mpo tofauti sana. Na pia mnaweza kuwa sawa kama marafiki lakini mkawa na ndoa tofauti.
 
Aaaah wapi wewe! Yule wa kwangu akijaribu huo upuuzi anajua kitakachomkuta. Kila siku nampaga risala na tahadhari.

Nyie mnaoweza kushare hongereni, mi hapana.
Ni kuachana tu kila mtu ashike hamsini zake. Unashare ila hujui.
 
Wanaume acheni haya mambo jamani yanaumiza sana!

Mwanaume kazingua mno, kumbe alimleta mchepuko wakafanya ushenzi mbele ya watoto?

Ila nimechekaaaa! Anayoyaongea huyo mwanamke kwa hasira yamenivunja mbavu.
Hasira hasara, sasa hayo makochi yamekosa nini??
 
Daah! Huyo dada apewe maua yake aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…