SI KWELI Video inayomuonesha mwanaume akichapwa Zanzibar ni ya Ramadhani ya mwaka huu 2024

SI KWELI Video inayomuonesha mwanaume akichapwa Zanzibar ni ya Ramadhani ya mwaka huu 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam ndugu zangu,

Nimekutana na video ya kusikitisha ikimuonesha raia anayesemekana kuwa ni raia wa Tanzania Bara akichapwa viboko na Raia wa Zanzibar kwa kosa la kula mchana wa Ramadhani. Je video hiyo ni ya mwaka huu?



1711716685283.png
 
Tunachokijua
Leo tarehe 29/03/2024 kumesambaa video (hii) ikimuonesha raia anayedhaniwa kuwa ni mtu wa Tanzania Bara alionekana anatandikwa bakora na raia wanaodhaniwa kuwa ni Wazanzibar kwa kosa la kula hadharani wakati wa mchana wa mfungo wa Ramadhani Zanzibar.

Video hii imezua taharuki ambayo imekuja siku Moja baada ya kuwapo kutoka taarifa ya Polisi Zanzibar(hii) iliyoeleza kuwakamata raia 12 siku ya 28/03/2024 kwa kosa la kula mchana wa Ramadhani.

1711715762164-png.2948161

Picha: Sehemu ya taarifa ya kukmatwa kwa watu 12
Video hii ililalamikiwa pia na Mwanachama JamiiForums Mawele aliyeleta uzi (huu) akihoji namna Zanzibar wanavyowachukulia watu wa Bara. Katika andiko hilo Mawele anahoji uhalali wa watu wa Zanzibar kuwapiha watu wasiofungwa.

Je, video hiyo ni ya mwaka 2024
Kama Mdau wa alivyoomba kujua tarehe ya video hii, JamiiCheck imefatilia video hii katika vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa video hii iliyombaa leo 29/03/2024 sio ya Mwaka huu. Taarifa yenye video hii (Soma hapa) Iliwahi kuletwa ndani ya Jukwaa la JamiiForums.com Juni 11, 2017 na Mwananchama Waziri Kivuli aliyekuwa akilalamikia kitendo kilichofanywa na wahusika walioonekana ndani ya video hiyo. Waziri Kivuli aliandika:

Huu si uungwana, mambo haya ndio huchochea hasira na visasi! Waliofanya kitendo hicho sidhani kama hata funga yao ina maana zaidi ya kujitesa kushinda njaa bure!

Aidha, JamiiCheck imebaini video hii imewekwa katika mitandao mbalimbali tangu (Juni 11 na 12, 2017). Mathalani, video hii iliwekwa katika mtandano wa YouTube kupitia Channel hii, hii na hii. Tazama kwenye picha hapa chini:
1711715928574-jpeg.2948167

Picha inayoonesha tarehe ya video hii kuwekwa YouTube​


Hivyo, licha kuwa video hii kuonesha tukio lililotokea kweli lakini kutokana na vyanzo hivyo hapo Juu JamiiCheck imejiridhisha kuwa si tukio la mwaka huu na halihusiani na habari (hii) ya 28/03/2024 inayoelezea watu waliokamtwa kwa kula mchana wa Ramadhani Zanzibar.
Huyu si ndo aliyeamru wamasai watandikwe bakora kisa wanatembea na sime zao?

Huyu ni wa kupuuza' na aache kubeza Imani za wengine
 
Yani siku hizi watu wakiwa na safari ya kwenda Zenji hawaagi wala kujulisha. Wanaogopa wakirudi wataulizwa kamamarinda yako salama?
Wanaume wa visiwani wakiona dume kutoka bara wanaanza kujipitisha wakiwa na UROJO maana yake hakuna marinda
 

Ukiona umefunga ila wanaokula wanakusumbua ujue wewe ni mlafi na mroho wa chakula, hujui ni kwanini umefunga na unajilazimisha tu kufunga.

Acha mara moja kufunga na uendelee kula machakula yako, usijitese, baada ya kufa hatujui tunapokwenda ukiachana na hizi hadithi za dini.
 

Ukiona umefunga ila wanaokula wanakusumbua ujue wewe ni mlafi na mroho wa chakula, hujui ni kwanini umefunga na unajilazimisha tu kufunga.

Acha mara moja kufunga na uendelee kula machakula yako, usijitese, baada ya kufa hatujui tunapokwenda ukiachana na hizi hadithi za dini.
Fact
 
Alafu huyo Dc anaonekana kihere here yeye kila tukio yumo, na kauli zake tata tata hizi mpaka mishipq ya shingo inamtoka na kama ukimfuatilia ni mtu fulani ambaye ana chuki kali sana na jamii ya watu wa bara
 
Mkuu wa wilaya ya Mjini Zanzibar mh Rashid Msaraka amesema clip inayotembea mitandaoni Juu ya Kijana aliyechapwa kwa kulewa mchana Mwezi wa Ramadan ni ya zamani 2017

Source: Kitenge Tv
Hata kama ni ya zamani, je ni sahihi?
 
Jamii check mbona siwaelewi, yaani hii video sio ya kweli kwamba jamaa hajachapwa ama vipi?
 
Mkuu wa wilaya ya Mjini Zanzibar mh Rashid Msaraka amesema clip inayotembea mitandaoni Juu ya Kijana aliyechapwa kwa kulewa mchana Mwezi wa Ramadan ni ya zamani 2017

Source: Kitenge Tv
kama ni ya mwaka huo, hao makatili walichukuliwa hatua gani? na jinai huwa haifi.
 
kama ni ya mwaka huo, hao makatili walichukuliwa hatua gani? na jinai huwa haifi.


TUHESHIMU MILA ZA WATU

Kukamatwa watu kula Mchana Zanzibar ~ Watanganyika wasio Waislamu wamezusha Mjadala.

Ni vyema tukafahamu ya kuwa MILA, DESTURI, SILKA na UTAMADUNI ni mfumo wa maisha kamili ya kila jamii. Zanzibar kwa karne nyingi imekuwa ikitajika na kusifika ikafikia kubandikwa jina Tolerance Country. Kwa miongo kadhaa iliyopita zimeanza kuja hizi nganu zenye sura ya udini kwa lengo lile lile kama unataka kumuua mbwa mpe jina baya. Hayo yamekuja kutoka kwenye kundi fulani la kisiasa na kudhani ni mtaji kwao kumbe ni kuizamisha Zanzibar.

Sina hakika kama katazo la kula HADHARI mchana wa RAMADHANI lipo kisheria au la. La muhimu, kuna watu wanadhani katazo la kula hadharani mchana wa mwenzi mtukufu wa ramadhani ni katazo makhsusi kwa Watanganyika na Wakiristo. Wasichotaka kukifahamu katazo linamlenga kila binaadamu wakiwemo Wazanzibari na Waislamu wenyewe.

Kwa faida ya anaetaka kufaidika mwanamke wa Kiisilamu hawezi kufunga mwezi mzima (29/30) kutokana na sababu za kimaumbile hivyo mwanamke huyu ndani ya nyumba yetu tumezaliwa, tumelelewa na kukua pamoja mimi huwa siijui ni lini yupo ndani ya siku zake (hedhi). Nakusudia kusema ndani ya myumba yetu wakati yeye anaudhuru wa kisheria anaruhusiwa kula siku hizo (baada ya ramadhani anakuja kuzilipa) basi pia huwa anakula kwa kujificha. Huwa hali mbele yetu tukimuona.

Kuna wagonjwa nao wanaruhusiwa kula kisheria (wakipona wanakuja kulipa na wasipopona wanatolewa fidia). Wakiwa ndani ya nyumba lakini mfumo wao wa kula unakuwa ni tofauti na miezi mengine yote.
Kuna watoto ambao hawajatimia umri wanaruhusiwa kula basi hawa watoto pia huwa hawali ovyo ovyo majiani wana utaratibu wameekewa wao wenyewe wanaifahamu na kuiheshimu ramadhani kupita kiasi.

Mfano ulio hai watoto wangu mimi binafsi wanakwenda skuli na chuoni huwa wanapewa fursa warudi myumbani kula kisha warudi tena skuli au chuoni kuendelea na vipindi, mwanangu mmoja anakwenda nyumbani kula na kurudi skuli mtoto mmoja haendi anaona aibu kuwa ataitwa KOBE (jina la utani kwa mtoto asiyefunga) jaribu kufikiria mtoto wa miaka 7 anaona aibu kugundulika kuwa hakufunga anahiyari abakie skuli asirudi nyumbani kula kwa kuchelea asijulikane kuwa ni kobe!

Tulio zaliwa na kukulia Zanzibar kwa miongo kadhaa tumewashuhudia wageni kutoka mabara ya mbali wakiuheshimu utamaduni huu. Ajabu iliyoje majirani zetu na ndugu zetu wa karibu tulitegemea wao ndio wawe sehemu kutoa elimu hii badala kuhoji kwani Zanzibar na Tanganyika ni nchi tofauti? Tanganyika kuna baadhi ya MILA na TAMADUNI hakuna Zanzibar. Kadhalika Zanzibar kuna baadhi MILA na TAMADUNI hazifanani kabisa na Tanganyika si ajabu.

Zanzibar wapo Wakiristo tumezaliwa nao na kucheza nao tumekuwa wote hakuna hata siku moja Mkiristo wa Zanzibar anaweza kufanya upuuzi wa kula hadharani mchana wa ramadhani.

Siungi mkono watu kujichukulia sheria mikononi lakini vile vile sikubaliani na watu ambao hawana tolerance ya kuheshimu utamaduni wa wengine na kudhani wao pekee wana haki ya kuingia kwenye nyumba ya mtu na kufanya anachoona yeye ni sawa kwake. Heshima ni kitu cha bure kwani mtu akichukuwa chakula chake na kuenda kula ndani kwake kuna tatizo gani? Karaha ya kula mchana wa mwezi mtukufu wa ramadhani watu wanadhani inawahusu Watanganyika na Wakiristo tu, haya yashawafika hata Wazanzibari na Waislamu. Kosa linalofanyika ni kule kujichukulia sheria mikononi na kupelekea kuumiza watu.

Sisi tulipo nchi za wamagharibi kuna mambo mengi tumezuiwa tusifanye na tunaheshimu hizo taratibu. Mfano sisi tuna msikiti lakini ni marufuku kuadhini kwa bomba (spiker) kwa hiyo tunaadhini kimya kimya na kusali kimya kimya tumepungukiwa nini kwenye imani yetu?

Assallam aleykum.
 
Mkuu wa wilaya ya Mjini Zanzibar mh Rashid Msaraka amesema clip inayotembea mitandaoni Juu ya Kijana aliyechapwa kwa kulewa mchana Mwezi wa Ramadan ni ya zamani 2017

Source: Kitenge Tv
SAWA KWAMBA ZAMANI NI RUKSA KUPIGA WASIO FUNGA?
 
jemshid mbali ya kuwa ni Mzanzibari yeye si sawa na Sultani wa Mkuranga
Okello alikuwa ni Mganda alikuja kuwakomboa Ndugu zake kwahiyo usiangalie sana asili ya Mtu.
 
Back
Top Bottom