Huyu hua anafikiri yeye kupigwa risasi ni ujiko kupata urais. Amegombea na kuangukia pua vibaya lakini anajidai eti alishinda ila kaibiwa kura🤣😂
Ndugu
kmbwembwe hakuna uhusiano wa u - Rais na uonevu, uhuni na mateso waliyomsababishia huyu ndugu..
Hebu wewe jaribu kuvaa viatu vyake;
√ Kwamba ushambuliwe ukiwa kwenye majukumu yako ya kazi ya mwajiri wako na watu "wasiojulikana" ili kukuua kwa risasi kama hizo za Tundu Lissu..
√ Mamlaka za uchunguzi na kutenda haki zinyamazie tukio hilo kimya kama vile hakikutokea kitu chochote....
√ Huyohuyo mwajiri wako akijua kilichokupata ukiwa kazini akunyime haki na stahili zako zote za kisheria kwa sbb tu kuna mtu pale juu na ana nguvu na mamlaka ya kuamua hivyo...
√ Huyo mwajiri ukiwa unaendelea kujiunguza kuokoa uhai wako, ukiwa huna hili wala lile anakufukuzwa kazi eti kisingizio kikiwa "mwajiri hajui uko wapi..". Really?
##Hebu niambie, ukiwa wewe au nduguyo katendewa hivi utajisikiaje?
##Likely, labda wewe huoni tatizo. Na pengine utajisikia poa tu. Lakini nikuambie tu kuwa, si mtu wa sampuli ya Tundu Lissu mtu mpigania haki, mpenda haki..
##Ukimkosea au kumtendea jambo lisilo haki Tundu Lissu, atahakikisha anafuatilia mpaka ajue ni kwanini umemfanyia hivyo. Tundu Lissu ni mfano ambao kila mtu anatakiwa kuwa, kupambania haki yako hadi tone lako la mwisho..
Inashangaza tu kuwa, wewe huoni hili na badala yake unawaza ujinga na upumbavu..!