Video: Je, hiki ndio kimesababisha Kemikimba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji kutenguliwa?

Video: Je, hiki ndio kimesababisha Kemikimba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji kutenguliwa?

View attachment 2721390
Imbainika kuwa kuwa chanzo cha Rais Samia kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ni kitendo cha kuonesha kiburi, dharau na kutoa lugha za kejeli kwa mfanyakazi wa Wizara hiyo aliyeenda kwenye Podium wakati akiwa anazungumza na kumpa 'Kinote'.

Jambo hilo lilionekana kumkasirisha Katibu Mkuu Nadhifa Kemikimba na akaamua kukatisha hatuba yake na kwenda kukaa.

Muda mfupi baadaye Waziri wa Maji alisogea kwenye Podium na kumuomba radhi Katibu Mkuu.
Podium ndio nini
 
na hata kama boss mwanaume anakuchukia unabeba demu mkali anaemtaka ila kama unapiga kazi hufukuzwi na hakuonei na cheo utapanda
sio wote mkuu. Nimeshakutana na hivyo vitimbi chuo na kazini! Kuna maboss ni wadhaifu sana kwa hizi pisi aisee...
 
Atapangiwa kazi nyingine yenye ngazi ya mshahara sawa na aliyotolewa ndivyo mara nyingi inavyokuwa na ndo uzuri/udhaifu wa ajira za serkalini haribu bodi ya pamba utapelekwa bodi ya kahawa, ukiharibu tena ya kahawa utapelekwa bodi ya sukari🤣🤣
Acha kupotosha
 
Huyu hastahili kuwa kiongozi. Mbona kuletewa ki note wakati unazungumza ni jambo la kawaida sana? Wanaletewa vi note hati kina Bidden, Trump na Obama? sembuse yeye? Yeye nani?
Nimewaangalia Kiumakini hao akina Biden, Trump na Obama kama walishawahi nao kupewa Vikaratasi wakiwa Wanahutubia katika Podiums zao sijaona ila kama una Video ya Ushahidi wa ulichokisema tafadhali niwekee / tuwekee hapa ili tukuamini.

Nijuavyo ( kama GENTAMYCINE ) kwa Kiongozi kuletewa Kikaratasi ukiwa Unahutubia katika Podium ni uthibitisho tosha kuwa huaminiki, msahaulifu, mbabaishaji, hujui Kitu, utakosea mbele ya Safari kwa Kubwabwaja Kwako kwingi Jukwaani na huna Akili ( Popoma ), ila basi tu upo upo.
 
Kwani alikuomba kuwa katibu mkuu? Ulivyomshusha umemuondolea elimu yake? Muogope Mungu peke yake!
Bwana eeeh…atutokee hapa kwani yeye tu ndio anatakiwa kuwa KM!? Haya Katumbuliwa….kazi si zinaendelea!? Yeye ameonyesha dharau mbele ya Watumishi wenzake kwa kujiona bora zaidi…Kumbe ukweli ni kuwa yeye ni TAKATAKA tu…Haya sender kuyafokea matoto yake nyumbani uone kama tutamjadili hapa.
 
Nimewaangalia Kiumakini hao akina Biden, Trump na Obama kama walishawahi nao kupewa Vikaratasi wakiwa Wanahutubia katika Podiums zao sijaona ila kama una Video ya Ushahidi wa ulichokisema tafadhali niwekee / tuwekee hapa ili tukuamini.

Nijuavyo ( kama GENTAMYCINE ) kwa Kiongozi kuletewa Kikaratasi ukiwa Unahutubia katika Podium ni uthibitisho tosha kuwa huaminiki, msahaulifu, mbabaishaji, hujui Kitu, utakosea mbele ya Safari kwa Kubwabwaja Kwako kwingi Jukwaani na huna Akili ( Popoma ), ila basi tu upo upo.
Ki-note ni kitu cha kawaida sana. Unless wewe upo porini na hauna utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara ama ya kibishara, kidini au kiserikali.
 
Iko hivi; kwenye Itifaki kiongozi kabla ya kuongea lazima akaribishwe na mwenye shughuli..kwenye huo mkutano ni watumishi wa Wizara ya Maji/DAWASA ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Waziri wa Maji na huyo KM alikuwa anaongea ili amkaribishe Waziri.
Sasa iko hivi; kama unaongea kabla ya muongeaji Mkuu/Mgeni Rasmi hutakiwwi kuwa mzungumzaji sana maana unaweza kuongea yale yote ambayo muongeaji Mkuu anakwenda kuzungumza na kwa kufanya hivyo inakuwa hakuna maana ya Mgeni Rasmi kuongea.
Kwa maelezo hayo hapo juu kwa nilichokiona hapo kinafanana na maelezo yangu na ndiyo maana hao watu wa HR ambao kiutaratibu ndio wasimamizi wa Itifaki walikuwa wanamkumbusha Bosi/KM kwamba imetosha amkaribishe Mhe. Waziri ambae ndiye alikuwa muongeaji Mkuu.
Alichoharibu zaidi ni kushindwa kuficha hisia zake na kumkaribisha Waziri kihuni.
Yote kwa yote alijiona yuko sahihi lakini kimsingi waliokuwa wanampelekea kimemo walikuwa wanamsaidia na wakati mwingine asichokijua inawezekana vimemo hivyo alipelekewa kwa maelekezo halali ya Waziri.
Nawaza tu kwa sauti..huyu Dada kule Arusha kwenye semina elekezi sijui alienda kutalii tu.
Wasalam.
Upo sahihi 100%
 
Sisi binadamu tuna tofautiana mambo mengi, wengine kutokana na malezi na imani yake hawezi kuigiza au kuwa mnafiki..mfano mzuri ni aliyekuwa waziri mkuu hayati Sokoine..hajui kuigiza na hizo itifaki za kinafiki anaishi kiuhalisia..heshimu msimamo wa mtu wa aina hiyo pia..kwa hali ilivyo wa kuteua au kutoa vyeo kwa watu pasina kujali sifa, umri, uwezo nk ni mtihani kwa mtu anayeamini kuwa anaotakiwa kuwapa heshima kulingana na itifaki kiuhalisia hawastahili kwa sababu anawazidi kwa vitu vyote! Elimu, uwezo, umri nk mambo ya aina hii huyakuti nchi zingine ni hapa Tanzania tu kwa sabab ya ignorance na mazoea ya hovyo na kutoheshimu tofauti za kielimu, uwezo hata umri..kwa kutizama tu hivi Aweso na huyo mama Mhandisi wanarandana..kielimu, uwezo, umri nk tatizo inaweza wala si hiyo memo ni mahusiano kikazi baina yao hapo wizarani.
Unaweza kutaja kinachopungua kwenye tukio kama wasipotajwa baadhi ya watu?
Itifaki hii ni hapa Tanzania tu? Mbona sehem nyingine haya ni mambo madogo sana..
Tupunguzie pumba humu jukwaani
 
Back
Top Bottom