Video: Je, hiki ndio kimesababisha Kemikimba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji kutenguliwa?

Video: Je, hiki ndio kimesababisha Kemikimba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji kutenguliwa?

Changamoto iliyopo hatujui hicho ki note kiliandikwa nini mpaka Katibu akaghafirika! Lakini bado Katibu angekuwa Mvumilivu.
 
Huyu hastahili kuwa kiongozi. Mbona kuletewa ki note wakati unazungumza ni jambo la kawaida sana? Wanaletewa vi note hati kina Bidden, Trump na Obama? sembuse yeye? Yeye nani?
Ukisikia miungu watu ndiyo hao mkuu yupo mwingine pale Elimu
 
The issue is not about the content or context of the memo but the place and reaction after receiving it!

No matter kimemo kilikuwa na habari za kukera kwa kiwango gani; hakutakiwa ku-behave vile, pale, wakati ule, mbele ya wale!

Right things, at the right time, and right place! Amekwama kwenye Hilo.
Kwanza ili awe kwenye mood yake kile kimemo.angekiweka.kwa.mfuko baadae akisome wakat akiwa ametulia,lazima ucheze na akili za watesi wako,today angekuwa safe na watesi wanalia
 
Uongozi ni mgumu kama hutambui madhaifu ya wafuasi,, zipo njia za kiongozi kudili na changamoto binafsi kama kiongoz hususan kwanye changamoto ambazo zitamtoa nje ya maadili ya kiutendaji! Yawezekana alikwazwa kulingana na mapokeleo yake Kwa wkt huo lkn ilimpasa kustahimili hrf angefuata taratibu za uongozi Kulingana na taratibu zao za kuonya watumishi! Hii ni hatriiii swala la maadili ni bado ni mtambuka!
 
Ukute kile ki-noti kilikuwa kimeandikwa "usisumbuke umeshatenguliwa" sasa hata kama ungekuwa ww ungeendelea kubwabwaja? Haaa haaa ila hatujajua kwenye note kulikuwa na ujumbe gani?
 
Anaweza hata kuwa Ras Mkoani ila salary ni hiyo hiyo ya Katibu Mkuu.

Serikali ilitaka ilete Mapendekezo ukitenguliwa na stahiki zako ikiwemo salary vinashushwa kulingana na kazi Yako ya kimuundo ya awali Watumishi na Wanasiasa walipinga sana hii Bungeni,ikawa imeisha kimya kimya.
Uko sahihi sana mkuu nakumbuka Mh. Jumanne Sagini kwa sasa mbunge wa Butiama alitenguliwa kuwa Katibu Mkuu Tamisemi na Magufuli akapelekwa kuwa RAS simiyu na salary yake ikiwa ileile🙏🙏.
 
Usikimbilie kuhukumu bro! Ki note kilikuwa kinasemaje?
Je aliyekipereka ana cheo gani? Alitumwa na nani?
Mfano wewe kama mfanyakazi wa kawaida kwenye kampuni, huwezi kukurupuka ukapeleka ki note wakati CEO anaongea, wapo viongozi wa karibu na CEO, MD, HR,CFO, kama una ishu pitisha kwako!
Hata kwenye kampuni zetu ndogo za bongo, sio kila MTU anaweza kujiingilia kwenye ofc ya mkurugenzi, hata kama hayupo,
Mipaka lazima iwepo,
Sasa wewe boss wako anaongea, unakurupuka kumpelekea ki note!
Kwenye taasisi zetu hz, kuna wafanyakszi wana vieleele Sana,
Katibu mkuu, ni msomi, technocrat, sio politicians,
And technocrats, takes no shit from anybody
Mnapenda ufalme wa kipumbavu tu, kama aliyeleta note alitumwa na akaandika lazima note itaanza mathalani, "...samahani mkuu, bosi anaomba ufupishe mazungumzo.." hapa unamkasirikia mjumbe au bosi wako?

Au kama kiliandikwa na bosi "...sorry katibu fupisha twende na muda.." kisha akatuma kijana apeleke unamkasirikia nani?

Kwa vyovyote hiyo note ilikuwa katika namna hizo mbili ndio maana waziri aliona kafokewa yeye na 'akaomba radhi' kusafisha hewa. Haikuwa radhi kama radhi ni sawa na kusema Eeh mama samahani kama hupokei maelekezo utatafuta unapoona panakufaa kuelekezwa.

Yaani bosi akuombe radhi wewe? Kilichofuata ITV....?[emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watu wenye kiburi na dharau kama hizi hawastahili kuwepo kwenye uongozi.
 
Kwanza kabisa jinsi anavyoongea nina wasiwasi kama ni MTANZANIA halisi.

Utamkaji wa maneno ni kama wa kenya.

Mbili hana heshima mbele za watu na naomba sana Mwenyezi Mungu amuadabishe zaidi.
 
Huenda ana tatizo la "inferiority complex".

Hata kama kakosewa kupelekwa kimemo, asingeonesha hasira zake hadharani kwa kuitupa. Angekaa nayo na baada ya huo mkusanyiko angefuatilia kwa mujibu wa miongozo stahiki.
Nachompendeaga Mhe. Makongoro Nyerere hivyo vimemo uwa anapewa sana akiwa jukwaani hata mbele ya Rais. Utamsikia "naona hapa nimeambiwa muda umekwisha sasa namalizia la mwisho kabisa" then watu wanacheka....anaendelea Ha ha ha!

Busara tu hutumika. Kimemo siyo dharau ni kwamba kila kitu kinakwenda kwa muda. Hata Rais upewa vimemo kujulishwa iwe muda au nini. Na utii. Kuwa na cheo kikubwa si wewe kuwa juu ya kila kitu. Ni vizuri kuwasikiliza hata ulowaamini walio chini yako.

Pole Katibu Mkuu, hasira hasara!
 
Back
Top Bottom