Parody
Member
- Sep 13, 2020
- 24
- 69
Tazama jengo la shule lililojengwa zaidi ya miaka 85 iliyopita likihamishwa zima zima kama lilivyo katika mji wa Shanghai, China, kwa kutumia teknolojia iliyopewa jina "Mashine Inayotembea"
Jengo hilo lililopo katika eneo la Wilaya ya Huangpou lilijengwa mwaka 1935 kwa ajili ya Shule ya Msingi Lagena, na limeondolewa ili kupisha ujenzi wa majengo mapya ya ofisi, ujenzi unaotarajiwa kukamilika mwaka 2023.
Kuhamishwa kwa jengo hilo kulifanikiwa baada ya Wahandisi kuchimba kuzunguka jengo hilo kisha kuweka mashine (robots) zaidi ya 198, hasa katika nguzo zinazoshikilia jengo hilo, na kufanikiwa kulibeba na kulisogeza umbali wa mita 62 kutoka eneo lililokuwepo awali ndani ya muda wa siku 18!
Hatua hiyo ni sehemu ya serikali ya China kuhifadhi majengo ya asili yenye historia ya nchi hiyo.
Chanzo: CNN