Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Chadema imelaani vikali hatua hiyo, ikitafsiri kama matumizi mabaya ya vyombo vya dola katika kudhoofisha shughuli za kisiasa.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa polisi wamesambazwa kutoka mikoa jirani, huku magari ya washawasha yakiwa tayari kudhibiti hali yoyote. Viongozi wa jeshi la polisi, akiwemo RPC na OCD, wanaripotiwa kuwa kwenye eneo hilo.
Aidha, polisi wameripotiwa kumkamata Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), Grace Vaaye na kisha kumuachiwa muda mchache baadaye