PreGE2025 Video: Jeshi la Polisi lazuia mkutano wa John Heche Wilayani Mbarali, Mbeya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia ukurasa wake wa X kimedokeza kwamba Jeshi la Polisi limezuia mkutano wa Makamu Mwenyekiti wake, John Heche, uliopangwa kufanyika katika Jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya.

Chadema imelaani vikali hatua hiyo, ikitafsiri kama matumizi mabaya ya vyombo vya dola katika kudhoofisha shughuli za kisiasa.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa polisi wamesambazwa kutoka mikoa jirani, huku magari ya washawasha yakiwa tayari kudhibiti hali yoyote. Viongozi wa jeshi la polisi, akiwemo RPC na OCD, wanaripotiwa kuwa kwenye eneo hilo.

Aidha, polisi wameripotiwa kumkamata Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), Grace Vaaye na kisha kumuachiwa muda mchache baadaye

Kisha utawasikia malaya wakisifia ujinga wa 4R
 
Chadema itatawala kwa haki,hivyo ccm wataruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa.
Watakufa kifo cha kawaida kama KANU ya Kenya.

Chama chochote ambacho msingi wake ni wizi wa kura huwa hakina popularity ya raia.

Kwa hiyo kikidondoshwa kwenye uchaguzi huwa hakiwezi kuhimili kwenye upinzani, kinakufa.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia ukurasa wake wa X kimedokeza kwamba Jeshi la Polisi limezuia mkutano wa Makamu Mwenyekiti wake, John Heche, uliopangwa kufanyika katika Jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya.

Chadema imelaani vikali hatua hiyo, ikitafsiri kama matumizi mabaya ya vyombo vya dola katika kudhoofisha shughuli za kisiasa.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa polisi wamesambazwa kutoka mikoa jirani, huku magari ya washawasha yakiwa tayari kudhibiti hali yoyote. Viongozi wa jeshi la polisi, akiwemo RPC na OCD, wanaripotiwa kuwa kwenye eneo hilo.

Aidha, polisi wameripotiwa kumkamata Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), Grace Vaaye na kisha kumuachiwa muda mchache baadaye

ni muhimu sana viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyopangwa na vibaka wa siasa na magenge ya khalifu kwa mgongo wa uhuru na haki za kufanya mikutano ya hadhara, vikadhibitiwa na kusambaratishwa kwa haraka sana na bila kucheleweshwa kabla ya kuleta madhara kwa wananchi

well done jeshi imara la police mkoa wa mbeya 💪👊
 
Taarifa za Kiintelijensia labda zinaonyesha usalama wa CHADEMA uko hatarini au hawajapewa kibali ili polisi wasimamie usalama katika mkutano wao.
 
Kumeanza kunogaa... Sasa... Tulia tuone usianze zegwe...
 
Nimemkumbuka yule polisi aliyestaafu na kuambiwa atoke kwenye ya serikali haraka ile hali hata pakwenda hana. Wajinga kama hawa huwapiga virungu masikini wenzao.
 
ni muhimu sana viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyopangwa na vibaka wa siasa na magenge ya khalifu kwa mgongo wa uhuru na haki za kufanya mikutano ya hadhara, vikadhibitiwa na kusambaratishwa kwa haraka sana na bila kucheleweshwa kabla ya kuleta madhara kwa wananchi

well done jeshi imara la police mkoa wa mbeya 💪👊
Tatizo lako unajifanya mjuaji sana na wala mwanamme hatakikani awe na akili mbovu kama hizo.
 
Back
Top Bottom