Hii sasa ni vita kubwa na mpya between two super powers Iran na Israel maana Iran ni nchi tajiri yenye msuli mkubwa wa kijeshi na pia ina washirika kama Russia na China ambao wanaweza kutuma silaha zikajaribiwe kwa kuipiga Israel, Israel na dunia ya wazungu sasa wamepata kitisho kikubwa na msemaji wa kijeshi wa Israel anaongea kuwa baadhi ya makombora yametua na kuleta hasara na binti mdogo kuumia, Israel wanafanya vikao kujadili mbinu za kujilinda, Israel wameomba msaada wa dharura wa kulindwa kutoka Marekani ambako leo kuna kikao kizito chini ya President wao aliekatisha safari zake na kurudi Washington kuja kujadili barua ya maombi ya Israel na nini kifanyike kuilinda Israel kwa njia za kidiplomasia, kutatua mzozo mpya kwa njia za amani, yaani marekani hawataki kabisa hiyo Vita mpya, haijulikani wanahofu nini.
Wakati huo huo UN general secretary ameitaka Iran kuacha vita hiyo wakisema dunia haina tena nguvu kuhimili vita mpya ya giants and Iran na Israel
Vita sasa ni kubwa maana jana Iran imechukua kibabe baharini meli ya Israel iliyokuwa na shehena ya mzigo wa Israel na Israel hawakuweza kuzuia zaidi ya kulalamika kuomba Iran iwekewe vikwazo na EU.
Raia wa Iran Leo wanakusanyika mitaani na kusherehekea kuanza vita na Israel kwa mara ya kwanza katika historia yao. Kiongozi wa Iran amesema Israel imeingia cha kike kushambulia ubalozi wao wa Syria ambako ni mshirika wao watakoma na wameionya US kuingilia Vita hiyo na kuwa tayari kuadhibiwa na wao washirika wote wanaoisaidia Israel.
Israel imeomba kufanyike kikao leo cha baraza la usalama la umoja wa mataifa kujadili mashambulizi ya Iran huko Israel na kukitaka kikao kilaani mashambulizi hayo. Iran imejibu hoja na kusema kikao kikikaa kilaani mashambulizi ya Israel kwenye ubalozi wao huko Syria ambako kuna maofisa wakubwa wa Iran walikufa.
Kwasasa duniani kuna kususiwa bidhaa za Israel ambako makampuni ya Israel yanafunga biashara na watu kuachishwa kazi, hii ni hatari sana kwa ustawi wa Israel.
Hivi sasa ndio vita kubwa imeanza maana baada ya baadhi ya drones na missiles kutunguliwa na zingine kutua kama Iran inavyodai, Israel ikijibu kama ambavyo wameahidi kulipiza, Iran itatuma ndege zisizo na rubani, sasa ndo kumekucha, Iran inapenda sana vita, iliwahi kupigana na Iraq ya Saddam kwa miaka 8 hadi pale makombora yenye hewa ya sumu yalipotumika na watu kufa kwa wingi huko Iran.
Kitu kizuri Israel inazuia uchukuaji wa picha za athari ya vita na ina iron Dome inayotungua baadhi ya makombora mengine yanapenya.
Wakati huo huo kuna makombora yanatumwa Israel toka Lebanon
Source: Al Jazeera TV mda huu kila kitu kinaongelewa.
Sisi bongo ni nyasi zitakazoumia kwenye vita ya tembo baada ya bei ya mafuta kupanda bei