Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Sasa kama tunaendelea na uzalishaji katika sekta zingine shida iko wapi? Kama utalii unakwama basi huu ndio muda wetu wa kujiimarisha katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi, na bahati nzuri mvua zimekuja za kutosha wakati muafaka, maana hizo ni bidhaa ambazo kwa siku za usoni zitakuwa na demand kubwa sana, hata hao waliokwenye lockdown watahitaji products za sekta hizo, huu si muda wa kukaa na kuombea Magufuli ashindwe ili mumzodoe, ni nchi yetu sote hii, nakuona jinsi ulivyo na shauku ya kuona tunaumbuka, wiki 2 mlizosema mnaona hazitoshi, sasa mnaanza tena miezi 6, haya ngoja tuone..
Ngoja nikufafanulie mambo mawili matatu, yatakusaidia.
Unasema tutaongeza uzalishaji wa kilimo, uvuvi na ufugaji ili kufidia utalii. Halafu unategemea uende kuuzia wale wale unaosema hawana nia njema na sisi, unaona unavyozidi kujikanyaga?
Pili sijataja jina la Magufuli hapa usijishuku. Nyakati zikiwa ngumu ndiyo mnakumbuka hili ni taifa letu sote.
Unajua kwa nini Magufuli ameona ulazima wa kuomba msamaha wa madeni? Ni kwa sababu miezi 3 kuanzia sasa kama hali hii itaendelea, kutaanza kuwa na uhaba wa fedha za kigeni, bei za vitu zitaanza kupanda kwa kasi kwa sababu importation itapungua, serikali itaanza kushindwa kulipa mishahara.....mengine utajazia mwenyewe.
Haya ninayokwambia ni kanuni za kimahesabu na kiuchumi, siyo mapenzi yangu au habari za kutunga.
Unavyowasema hao unaoita wazungu utadhani waafrika ni watakatifu.