Uchaguzi 2020 Video: John Heche akishangiliwa na wananchi wa kata ya Nyanshicha kijiji cha Nyantira kwenye kampeni, CCM kwaherini

Uchaguzi 2020 Video: John Heche akishangiliwa na wananchi wa kata ya Nyanshicha kijiji cha Nyantira kwenye kampeni, CCM kwaherini

Watu wamebadirika sana brother,hata mimi nilidhani hivyo mwanzo kwa jinsi mlivyokuwa mmejiandaa,miaka mitano ya kampeini + wakurugenzi wote mkaweka makada + tume ya uchaguzi mkaweka makada, lakini si shwali bado kulikoni?
Tulia dawa ikuingie vizuri, usifurukute.
 
Kumbuka kwamba Magufuli na mgombea wake walizomewa huko kwao kanda ya ziwa hadi akakasirika na kuwatisha
Lissu ndiyo alizomewa, Magufuli hajawahi kuzomewa kama una ushahidi weka hapa.
 
Yaliyosemwa na kigogo yametimia ya kushambuliwa kwa Heche na lema kuvunjiwa vyombo vyake. Hapo ni kuwajenga
 
Hebu thibitisha kwa ushahidi tuone.
Aii kwanini nihangaike na ushaidi?! Hiyo namba uliyoweka, 10, ukibadilisha useme tu mwenyewe kwamba sasa naongeza tena! Nakuombea kwa Mungu usipatwe na Magonjwa Mtambuka yoyote, ikiwa matarajio yako ya CHADEMA kushindwa, yatashindwa!
 
Heche anapoteza muda wake. Kwanza upinzani wanamkera sana raisi na ndo mana amewanunua ili muishe. Mana mnamchanganya kwenye utendaji. Uelewe awamu hii wapinzani hawana kazi mana hakuna safari za nje,ufisadi hakuna.

Na ndo mana mnaongea na kiongozi wa nchi mmeweka mikono mfukoni. Hata baba yenu mnakuwaga ivyo ivyo? Ama ni kuburi cha kikurya kuwa ni murisha.

Chadema awamu hii hampiti tarime. Tuchague upinzani afu tutengwe kuletewa Huduma za kijamii. Na sema kwa no kubwa sana. Tena no mana jpm hataki wapinzani hammsikilizi raisi kazi ni kupinga tu.

Pia awamu hii uongozi unaenda kwa Uko wa akina weitara. Hata huyu sijui ni wa wapi hajui unabii ulivyonenwa hapo zamani za kale yaani za kale. Jimbo likiwa LA wapinzani mnatengwa pia mkiomba Huduma hampewi na serikali mana muwakilishi wenu ni wa cdm na huku raisi ni wa chama Kingine kazi inabaki kuvutana tu.

Angalia hata KISHIRI tu ilishabikia chadema mpaka Leo hii hakuna umeme wala maji mpaka barabara
Hapa tatizo ni management ya JF kuruhusu kila mpuuzi kujiunga!
 
Pamoja na hujuma zote toka kwa waitara kutumia Hadi police kuhujumu mikutano ya Heche ikiwemo kuchana mabango kuharibu vyombo vyake, hawezi shinda,
Kwanza amesusiwa kampeni na maccm wenzake wanamuona kiraka
 
Hapa tatizo ni management ya JF kuruhusu kila mpuuzi kujiunga!
Mkuu Sera zote za upinzani jpm kazifanyia kazi saivi wamebakia kuwa fly over inamsaidiaje bibi Yangu huko Kijijini hawana jipya tena wameishiwa Sera. Wameanza kuponda huyu tena hasafiri kupata exposure.
Tupo hapa tunza komenti hii ndugu Weitara anaichukua Tarime Vijijini
 
Serikali ya Chama Cha Mafisadi (CCM) ni muasisi na kinara wa ufisadi hapa nchini Tanzania. Hiki chama na serikali yake hawawezi kupambana na ufisadi kamwe. Mapambano dhidi ya ufisadi kwa CCM ni sawa na mkosaji kujiadhibu mwenyewe, jambo ambalo katika hali halisi, haliwezekani katu. Uliona wapi nyani anajizuia kula mahindi ya mkulima? Nyani wamezoea kula mahindi ya mkulima kiasi kwamba mkulima akiwafukuza au kuwaua wasimalize mahindi yake, watamuona kama anawaonea bure! Wanadhani kula mahindi wasiyoyalima ni haki yao ya msingi au ya kuzaliwa.

Jinsi ambavyo wanakula mahindi ya mkulima, vivyo hivyo CCM na serikali yake wamezoea kufisidi mali za umma kiasi kwamba inakuwa vigumu kwao kuwasikiliza wale wazalendo wanaowakataza au kuwashauri waachane na ufisadi. Wanadhani kwamba kufisidi mali za umma ama ni haki yao ya msingi au ni haki yao ya kuzaliwa! Hapo ndipo serikali ya kifisadi ya chama cha mapinduzi ilipotufikisha.

Na kama ambavyo ili mkulima ajiepusha na nyani anapaswa kuwaua au kuwafukuzilia mbali nyani, vivyo hivyo kwa chama cha mafisadi na serikali yake, ili kuepukana na ufisadi wao, hatuna budi kuwapiga chini mwaka huu wa 2020. Hii ndiyo njia rahisi na sahihi ya kupambana dhidi ya ufisadi. Huwezi kuitenganisha CCM na ufisadi. UFISADI na CCM ni kama kuku na yai. Ili upate yai sharti ufuge kuku; na ili upate kuku sharti uwe na mayai ya kutotolea vifaranga ambao wakishakomaa huwa kuku. Hivyo basi, ili kuepuka mayai (yanayotoa kuku), huna budi kuwachinja kuku wote na kuwafanya kitoweo. Vivyo hivyo, huwezi kupambana na ufisadi kikamilifu bila kuwang’oa CCM kutoka madarakani. Tukifanikiwa kuwang’oa CCM madarakani tutakuwa tumeumaliza ufisadi nchini.

Ndugu watanzania tukicheka na nyani (CCM) tutavuna mabua (umasikini). Hima wananchi tujitambue ili tusiendelee kunyonywa na kupe hawa wasioshiba kamwe. Tuwaulie mbali. Vinginevyo, itakula kwetu na hatutakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa kutofanya maamuzi sahihi ya kuwafutilia mbali CCM kutoka kwenye utawala wa chi hii. Wazungu wana msemo mmoja usemao, “If a peron decieves you once, shame on him; if twice, shame on you”. Tafsiri isiyo rasimi ya maneno haya ni kuwa. “Ikiwa mtu atakudanganya mara moja, aibu iwe kwake; lakini ikiwa mtu huyo huyo atakudanganya mara ya pili, aibu na iwe kwako”. Ikiwa utakubali kudanganyika mara ya pili, basi akili zako hazina akili!

Ndugu wananchi wapenda maendeleo, Chama Cha Majambazi (CCM) wamekuwa wakitudanganya miaka nenda miaka rudi lakini hatujifunzi kutokana na makosa yetu ya nyuma; matokeo yake tumekuwa tukiwarejesha madarakani kila Uchaguzi Mkuu uitishwapo. Ndugu zangu tutajifunza lini? Mbona tunakuwa na akili kama za kuku wa kienyeji au punda?

Kuku wa kienyeji hupenda kuchakura mwenyewe vichakani kutafuta chakula bila kuhitaji uangalizi wa mfugaji. Ukiwafungia kuku wa kienyeji bandani, ukawaweka kwenye mazingira tulivu chini ya kivuli, na ukawapa chakula na maji tele, watakudharau sana. Watakuona kama unawaonea kwa kuwafungia ndani na kuwapa chakula chenye virutubisho vyote, badala ya kuwaachia wajitafutie wenyewe chakula duni walichokizoea huko kwenye vichaka.

Punda daima hupenda kubeba mizigo mizito. Ikitokea Bwana (master) akambebesha punda mzigo mwepesi, humdharau sana na kumuona kama hampendi. Anadhani kubebeshwa mizigo mizito ni haki yake ya kuzaliwa. Ukimbebesha punda mzigo mwepesi halafu ukakatiza karibu yake, hakawii kukupiga mateke ili kuashiria kwamba hajaipenda tabia yako mbaya ya kumbembesha mzigo mwepesi. Atakuchukia na kukuona humtakii mema katika harakati zake za kubeba mizigo mizito kupindukia.

Nadharia hizi mbili zinaelekea kufanana na namna ya maisha ambayo watanzania wamechagua kuishi. Watanzania wamezoea kuishi maisha ya dhiki na taabu kama ambavyo punda na kuku wa kienyeji wamezoea kuishi kwa kuchakura na kubeba mizigo mizito mtawalia (respectively). Chama Cha Magamba (CCM) kimefanikiwa kuwafukarisha watanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa! Pamoja na ufukara wote ambao chama hiki kimeusababisha, bado wananchi wamekuwa wanakiunga mkono na kukifanya kiendelee kubaki madarakani mpaka leo. Ni lini watanzania tutafunguka macho na kuzibuka masikio na hatimaye kuacha kuchagua maisha ya utumwa chini ya CCM na serikali yake?

Ndugu zangu, saa ya ukombozi ni sasa. Naomba tujitambue na tujisahihishe; tujutie na tutubu makosa kwa kuendelea kumkubatia huyu shetani, ibilisi mtoa roho (CCM). Tutafungwa nira na kubebeshwa mizigo mizito na huyu shetani mpaka lini? Hebu tuitue mizigo yetu chini tukimbilie kwa Mkombozi (CHADEMA) ili tupate kupona. Dhambi ya kukubali kufungwa nira na kuchapwa mijeledi kama punda na huyu ibilisi (CCM) itatugharimu uhai wetu na vizazi vyetu sawia. Tubadilikeni ndugu zangu. Tusikubali kufungwa nira tena mwaka 2015. Tukatae kutumiwa na CCM kama ngazi ya kuning’inia madarakani.

Nimetumia hii logic rahisi ili hata wale ambao hawakwenda shule (wanaCCM) wanielewe barabara. Kwa hiyo, wito unatolewa kwa wananchi wote kuwang’olea mbali CCM, kupitia sanduku la kura tarehe 28/10/2020. Sote tukiungana kwa pamoja bila kujali rangi, kabila, jinsia wala dini zetu, tutawafuta hawa kupe kutoka kwenye uso wa ardhi ya Tanzania. Kumbuka kwamba njia nzuri ya kupambana na kupe ni kumnyima chakula (damu) kwa kuwaweka mifugo mbali na kupe. Kuna baadhi ya kupe ambao wamekuwa sugu, hata uwapulizie dawa kali kiasi gani hawafi. Na hawa kupe (maCCM) walishakuwa sugu. Huwezi kupambana nao kwa kuwashitaki mahakamani kwa kuwa wameishakuwa sugu wa mahakama. Njia nzuri ya kupambana nao ni kuwanyima ulaji (uongozi) kama vile ambavyo kupe wakinyimwa damu hujifia kwa njaa! Kumbuka kwamba hawa kupe wamekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne (zaidi ya miaka 50) lakini tukitazama maendeleo waliyoyaleta katika nchi hii hayalingani na maendeleo waaliyoyaleta MABEBERU wa kikoloni.

Ndugu watanzania, kwa hiyo mifano michache nadhani mtakuwa mmeona kwamba serikali ya Chama Cha Mashetani (CCM) haijafanya chochote cha maana zaidi ya kujitapa na kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu”, kaulimbiu ambayo haina mashiko tena, hasa baada ya wananchi kugundua ulaghai uliojificha kwenye kaulimbiu hii. Ni maneno matupu tu ambayo hayawezi kuuvunja mfupa huku wananchi wakizidi kutopea kwenye lindi la umaskini. Hivi sasa Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mkiani mwa nchi maskini baada ya Somalia na Afghanistan. Deni la taifa limekuwa kutoka Tsh trillion 22 alizoziacha Mkapa hadi Tsh trillion 55 sawa na ukuaji wa 150%! Ndugu zangu, naomba tuukatae umasikini kwa kuiondoa serikali ya Chama Cha Mafisi (CCM) madarakani. Tusikubali kuendelea kuburuzwa tena kama maboya. Tanzania yenye neema inawezekana tu kwa kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa CCM na serikali yake dhaifu na ya kifisadi ndicho kizingiti (bottleneck/hurdle) cha maendeleo ya nchi hii. Kuikataa CCM ni kuukataa umaskini, ufisadi, udokozi, unafiki, uzandiki, nk. Ukitaka kuishi maisha bora tushirikiane kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Tuhakikishe wote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, tunajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na tuzitunze shahada zetu vema hadi siku ya uchaguzi, twende tukampigie kura Mgombea wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu ili atuondoe kinywani mwa mamba mla watu (CCM), ambaye daima amepanua domo akitaka kutumeza bila huruma. Hii ndiyo hatua muhimu ya kujinasua kutoka utumwani (Serikali ya CCM) kuelekea katika nchi ya ahadi (Serikali ya CHADEMA), nchi itiririkayo maziwa na asali (maendeleo endelevu na maisha bora kwa kila mtanzania).

Miongoni mwetu kuna watu waliokata tamaa. Tuwe makini na watu hawa na daima tuwatie moyo na chachu ya mabadiliko (M4C). Hawa ‘wakata tamaa’ ni wale ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura kwa kisingizio kwamba hata kama wakipiga kura magamba wanaziiba. Msidanganyike ndugu zangu. Ukigoma kwenda kupiga kura humgomei mgombea wa gamba wala wa CHADEMA bali unajigomea mwenyewe. Usipopiga kura unawapa mwanya magamba wapite hata kama kwa tofauti ya kura chache. Kumbuka kwamba anayepata kura nyingi ndiye anyeshinda, hata kama akipigiwa kura na familia yake tu. Katika uchaguzi uliopita tumepoteza majimbo mengi kwa tofauti ya kura chache sana. Tusifanye makosa tena safari hii. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA tukawafutilie mbali magamba. Kazi ni kwako ndugu mtanzania unayeishi maisha ya utumwa huku ukitembea juu ya ardhi iliyosheheni almasi, dhahabu, tanzanite, uranium na rasilimali nyingine nyingi tulizojaaliwa na Mungu. Tafakari, chukua hatua ya kuing’oa CCM madarakani kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020!
 
Mkuu wanaujua muziki wa Chadema hao ndiyo sababu wanaikacha tume huru maana watapigwa Nchi nzima kipigo cha paka mwizi na kufutika rasmi katika anga za Siasa Tanzania.

Kuna wakayi CCM ilisema CHADEMA haitapata mbunge hata mmoja, sahizi mnasema wabunge kumi, wiki ijayo mtasema wabunge 50, mwishoni mwa mwezi sijui mtasema wangapi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wivu Hadi wamembomolea vyombo vyake na kuchana mabango yake unabii wa kigogo umetimia juu ya watu waliotumwa, sisi tunawachora tu wanavyopambana na ukuta
 
Heche anapoteza muda wake. Kwanza upinzani wanamkera sana raisi na ndo mana amewanunua ili muishe. Mana mnamchanganya kwenye utendaji. Uelewe awamu hii wapinzani hawana kazi mana hakuna safari za nje,ufisadi hakuna.

Na ndo mana mnaongea na kiongozi wa nchi mmeweka mikono mfukoni. Hata baba yenu mnakuwaga ivyo ivyo? Ama ni kuburi cha kikurya kuwa ni murisha.

Chadema awamu hii hampiti tarime. Tuchague upinzani afu tutengwe kuletewa Huduma za kijamii. Na sema kwa no kubwa sana. Tena no mana jpm hataki wapinzani hammsikilizi raisi kazi ni kupinga tu.

Pia awamu hii uongozi unaenda kwa Uko wa akina weitara. Hata huyu sijui ni wa wapi hajui unabii ulivyonenwa hapo zamani za kale yaani za kale. Jimbo likiwa LA wapinzani mnatengwa pia mkiomba Huduma hampewi na serikali mana muwakilishi wenu ni wa cdm na huku raisi ni wa chama Kingine kazi inabaki kuvutana tu.

Angalia hata KISHIRI tu ilishabikia chadema mpaka Leo hii hakuna umeme wala maji mpaka barabara
Kodi yao nayo itengwe??
 
Unaipungia Mkono Wa Kwaheri CCM simply Kwa kuwa Ndg.Heche Ameshangiliwa na WANAKIJIJI Katika KATA?!!

Yaani Wanakijiji Wa Kijiji Kimoja....Hata Ingekuwa Kata Nzimaa...

😂😂Seli Nyekundu Za Damu Banaaa....

Haya MUNGU Atupe sote Pumzi na Afya Tele Tuione Wiki ya Baada ya Oktoba 28 Aaamin.
Mkuu Heche anashinda ubunge Tarime vijijini.
 
Mkuu Sera zote za upinzani jpm kazifanyia kazi saivi wamebakia kuwa fly over inamsaidiaje bibi Yangu huko Kijijini hawana jipya tena wameishiwa Sera. Wameanza kuponda huyu tena hasafiri kupata exposure.
Tupo hapa tunza komenti hii ndugu Weitara anaichukua Tarime Vijijini
KWAMBA WAITARA ANAFAA? NADHANI HUNA UELEWA WA MAMBO WEWE. WAITARA ANAWEZA KUSHINDA KAMA WANA TARIME VIJIJINI WATARUHUSU WENYEWE KUFANYIWA UHUNI KURA ZAO ZIIBIWE, NAJUA KWA KURA HAWEZI KUSHINDA, WANA TARIME VIJIJINI SIO WAJINGA, NA NINAJUA WATU WANAOWEZA KUMPIGIA KURA WAITARA NI WALE WENYE MAHABA NA CCM YA KIJINGA, AMBAO NI WACHACHE SANA...MTU ANAYEJITAMBUA KABISA HAWEZI KUMPA KURA WAITARA!
 
Back
Top Bottom