Zanzibar 2020 VIDEO - KAMPENI ZANZIBAR: Tundu Lissu awapa somo muhimu Wazanzibar na Watanganyika juu ya Muungano. Je, Magufuli - CCM anaijua historia hii kweli?

Zanzibar 2020 VIDEO - KAMPENI ZANZIBAR: Tundu Lissu awapa somo muhimu Wazanzibar na Watanganyika juu ya Muungano. Je, Magufuli - CCM anaijua historia hii kweli?

..hataweza ku-prove kwasababu vyombo vya dola na mahakama ni za ccm.

..hata mauaji yaliyotokea mgodini Bulyankhulu miaka ya 90 alishindwa ku-prove kwasababu vyombo vya dola/uchunguzi vilikuwa upande wa serikali na siyo upande wa wahanga ambao TL alikuwa anawatetea.

..ccm mnapozidiwa ktk majukwaa ya kisiasa mnakimbilia kwa Polisi wenu, waendesha mashtaka wenu, na mahakama zenu.
Twende wote.

Inajulikana wazi kuwa kutojua sheria sio kigezo cha kutokuadhibiwa na kiwa sheria ikipitishwa hata Kama ni mbaya basi inahotajika movement ya kuibadilosha but until then, bado ukitenda kosa utahukumiwa kwa sheria hiyo.

Lissu yeye anajua kisheria, chochote anachokisema kinyume na kinavyoonekana basi anawajibu wa kukithibitisha. Anajua kuwa anachokisema kinahitaji proof ambayo hana huku akijua ni kinyume na sheria ni kinyume na mwenendo na utaratibu wa kampeni.

Nadhani ameshajua hawezi kushinda Sasa anaharibu ili afutwe kugombea aseme ameonewa kwasababu angeshinda.
 
Mbona wameikata video, sasa unafika wakati wa kuomba kura mleta mada unakatisha hotuba ya mgombea sio jambo zuri, unakuwa kama TBC.

Lete yote tusikilize kwa macho.
Basi nimeiona kwenye uzi wa yule DADA-VUA unasema Lisu amuombea kura Maalim Seif.
 
Ila Mungu fundi sana, hivi Magufuli, angepewa hata robo ya akili ya Lissu, na vile anapenda ajue kidhungu, na kutoa takwimu za kilomita za bara bara tungekoma.

Anachojua kwenye historia ya Tanzania ni Chato. Na maeneo mengingine yenye majina ya kiuasharati tu. Eneo la katerero na mto wake wa maji.

Kumuuliza historia ya Muungano Magufuli ni kumuonea bure.

Miaka 5 inatosha akapunzike, acheni kumsukumia huko.
Saa hizi ungekuwa umelala
 
Hili lipo wazi.
Tumepakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Malawi na Msumbiji, hakuna hatari ya usalama, hi habari ya usalama kukosekana kwa muungano wa serikali 3 inatoka wapi? Mnatujengea hofu kama ya korona! Waache wazanzibar waendeshe nchi yao! Kama shida Ni ukaribu wa Ikulu kwa mpaka wa Zanzibar, mbona tayari tuna Ikulu Dodoma?
 
Upinzani hata kama hutaki muungano ukisema huu muungano w serikali mbili naukubali imo ushinde ukishinda ndio uongelee kuvunja wakashindwa nini? Kwa nini ukomalie kitu anachojua ukichokonoa kitakufanya ashindwe?

Lisu kachokonoa ajiandae kushindwa tena vibaya kura zote za wazanzibai weusi wa unguja na Pemba hazipati sababu wao muungano ndio unawafanya waishi vizuri na hata wapemba wenye biashara zao na shughuli zao Bara na ndugu Zanzibar kura zao hawezi pata

Wazanzibari hospital yao ya rufaa ni muhimbili ndiki huja kutibiwa wakishindikana kule kwa hiyo ukisema muungano hutaki kazi unayo!!! Kupata kura Zanzibar


Tutolee propaganda zako za zama za kale hapa. Kuna Wakenya wapo mpaka Newala huku wanafanya biashara,tuna Wacomoro wengi tu,tuna warundi na Wanyarwanda wengi tu hapa wanafanya biashara. Kuna wazungu na wachina wengi tu wana biashara na viwanda.

Serikali tatu zinawazuru nini nyinyi MATAGA? Au kila mtu akibaki na nchi yake kuna shida gani mbona tuliishi hivyo wakati wa mkoloni? Mbona Burundi na Rwanda wanajitawa,mbona Comoro inajitawala na haihatrishi usalama wenu nyinyi MATAGA.

Tuotoleeni ujima wenu hapa vibuyu nyie,kama mnapenda kuwa na nchi kubwa unganeni na Rwanda na Burundi nyau nyie.
 
Kwa sababu za ulinzi hatuwezi jitenga na Zanzibar. Sehemu ya bahari pia itakayoimiliki Zanzibar baada ya kutengana inatulazimu kuhakikisha Zanzibar ni part ya Tz. Kijografia hizi hazikupaswa kuwa nchi mbili sema ndio tayari ipo hivyo.
Hizi ni stori za zamani sana. Eti kiulinzi. Basi tuungane na Msumbiji ili kuimarisha ulinzi wa mikoa ya kusini.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Twende wote.

Inajulikana wazi kuwa kutojua sheria sio kigezo cha kutokuadhibiwa na kiwa sheria ikipitishwa hata Kama ni mbaya basi inahotajika movement ya kuibadilosha but until then, bado ukitenda kosa utahukumiwa kwa sheria hiyo.

Lissu yeye anajua kisheria, chochote anachokisema kinyume na kinavyoonekana basi anawajibu wa kukithibitisha. Anajua kuwa anachokisema kinahitaji proof ambayo hana huku akijua ni kinyume na sheria ni kinyume na mwenendo na utaratibu wa kampeni.

Nadhani ameshaiua hawezi kushinda Sasa anaharibu ili afutwe kugombea aseme ameonewa kwasababu angeshinda.

..Polisi wetu wanapendelea ccm.

..Waendesha mashtaka ni vibaraka wa ccm.

..Mahakama ni kichaka cha ccm.

..Halafu mnataka watu wakathibitishe madai yao mbele ya vyombo hivyo.

..CCM mkizidiwa hoja za kisiasa mnaweka mpira kwapani.
 
Lissu anataka kuuboresha muungano kwa kuleta serikali tatu

Kuendelea na muungano wa aina hii usio na ridhaa ya Wazanzibari ipo siku wataingia mitaani kushinikiza viongozi wao wauvunje na Mtakuwa hamna jinsi ya kuwazuia maana hakuna jeshi la kuufanya muungano uwepo kama Wazaznzibar kwa umoja wao wataingia mtaani kuukataa!

Mwenye akili ni yule anayewasikiliza wazanzibar wanataka nini leo. Ukiwalazimishia aina ya muungano huu ambao unategemea tuwapandikizie wazanzibari vibaraka, kisha tuwashindishe kwa figisu kwenye sanduku la kura, kisha tuwalinde kwa kutumia majeshi huu muungano hautofika popote siku wazanzibar wakiamua kuingia mtaani kuukataa!

Lissu ndiye mzalendo wa kweli anayetaka tuunusuru Muungano kwa kutengeneza muungano uliofair, Nje ya hapo it is a matter of time kabla Wazanzibar hawajarevolt!
Inatosha kuwa ni jibu pekee kwa mataga wote pale Lumumba na kwingineko!
 
Tatizo la Mgombea WAO anaongea vitu ambavyo hakupaswa kuongea..Wazanzibar hawatakiwi kujua Historia yao. Wanatakiwa kuwepo kama walivyo sasa. Tuwaamulie nani anawafaa kuwatawala na sio wao wenyewe..Tatizo la TL anaharibu kabisaa yaani Sio vyema kwa kweli..🙁🙁
Sasa wewe ni mkoloni kwelikweli, na uaamini katika kutumia ujinga wa raia na ukandamizaji wa haki ya kupata habari ilimradi ubaki madarakani, huo ni unyama!
 
Yuko tayari avunje Muungano ili ajenge SGR na Bwawa umeme
 
Hakuna aliyeyejaribu kuvunja muungano au kuungana na wavunja muungano huu uliopo kama ulivyo sasa aliyefaniiwa kushika uraisi iwe wa muungano au wa Zanzibar awe wa CCM au upinzani

Aboud Jumbe na Seif shariff Hamad walikwama kwa sababu hiyo. AKINA warioba, Lowasa waligombea wakashindwa kwa hivyo kipengele sababu alienda kuungana kwenye UKAWA na Maalim Seif mtaka kuvunja muungano huu wa serikali mbili uliopo

Lisu kajiingiza mwenyewe kwenye mdomo wa mamba biashara imeisha .Hapewi uraisi

Muungano uliopo ni eneo sensitive ambalo mwanssiasa yeyote anayeutaka uraisi hatakiwi kuligusa negatively kuwa anavunja huu muungano wa serikali mbili uliopo
Wenye nchi yao wakiamua kwa pamoja kurejesha nchi yao mtawaua wote?
 
Akikujibu, nishtue. Hawa ndio team ya Bashiru aliwaagiza juzi wajibu mapigo. Lakini maskini hawaelewi lolote matokeo yake wanakurupuka kama ngiri shimoni.

Hawana hoja ,hawajui historia ngoja utaona wanakuja na matusi!!! Bashiru mwenyewe hiyo hotuba kwake ni somo tosha kwani alipokuwa msaidizi wa marehemu Kinyondo haya mambo ndio yalipotendeka hivyo uelewa wake ulikuwa mdogo!!
 
Bara na visiwani tumeshakuwa ndugu. Tuna muingiliano wa damu na kijamii.

Muungano nao ni muhimu sana kwa usalama wa pande zote. Lissu analeta mentality za kikoloni kwani anataka turudi kwenye kifungo cha mipaka ya kikoloni kwasababu za kisiasa.

Changamoto za Muungano zishughulikiwe kwa umakini na ustaarabu wa halinya juu

Amenishangaza Sana huyu mwamba
Wapi amesema hataki Muungano!
 
Back
Top Bottom