Video: Kijana afunguka alivyofanyiwa ukatili wa kutisha na mwenyekiti wa kijiji Uleling'ombe, kilosa

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
Tazama video inasikitisha sana...

Yapo baadhi ya mambo ukiyasikia unaweza kudhani pengine uko ndotoni!

Siku kadhaa zilizopita, liliripotiwa tukio la kushangaza, kustaajabisha, na kuhuzunisha kuhusu vijana wawili wanaodaiwa kufanyiwa ukatili wa kutisha na Mwenyekiti wa Kijiji cha Uleling'ombe, Kata ya Uleling'ombe, Kilosa, mkoani Morogoro, Generasko Tresfori.

Global TV imempata mmoja kati ya vijana hao wawili wanaodaiwa kufanyiwa vitendo vya kikatili na kiongozi huyo kwa kushirikiana na mgambo aliyetajwa kwa jina la Tegemea Maganza, wakituhumiwa kuiba simu ya mwenyekiti huyo.

Hapa kijana huyo anasimulia kwa uchungu jinsi alivyofanyiwa ukatili, tukio lililotokea Februari 25, mwaka huu.

Daaaa hukoo kuna serikali kwelii ?? Aibuu sanaaa...
 
Umesikia alikamatwa na migambo

Alikuwa overpowered na mtu zaidi ya mmoja pengine wenye ubavu kuliko yeye.
Muhimu asaidiwe ili mtesi wake afikishwe mahakamani.
Mkuu mada kama hizi huwezi kuta watu wanachangia kwa wingi ili kukomesha ukatili..
Ila ingekuwa mambo ya tff, simba na yanga uzi ungekuwa una flow kama kama mvua za masika
 
Ndugu wachangiaji nilifika katika kijiji kimoja na KUKAA kama mwaka mmoja nilichojua kuwa ukiwa mjini na vijijini ni MBINGU na ARDHI vijijini mwenye kiti wa kijiji amepewa nguvu na anaheshimika sana hata akipita unamfuata unamsalimia kwa HESHIMA na ukiwa ww humjui wale ndugu ulipofikia wanaenda kukutambulisha kwa style za unyenyekevu utashangaa baada ya muda unaanza kufuata taratibu zao ikitokea umepigana ukipelekwa ofisini unachapwa viboko mpaka 50 na kuendelea
 
Mpaka kufiln tena au viongozi wamebariki upuuz huu

Ova
 
Ndugu wachangiaji nilifika katika kijiji kimoja na KUKAA kama mwaka mmoja nilichojua kuwa ukiwa mjini na vijijini ni MBINGU na ARDHI vijijini mwenye kiti wa kijiji amepewa nguvu na anaheshimika sana hata akipita unamfuata unamsalimia kwa HESHIMA na ukiwa ww humjui wale ndugu ulipofikia wanaenda kukutambulisha kwa style za unyenyekevu utashangaa baada ya muda unaanza kufuata taratibu zao ikitokea umepigana ukipelekwa ofisini unachapwa viboko mpaka 50 na kuendelea
Wapi huko?
 
Back
Top Bottom