Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mbeya limebaini wizi mkubwa wa nishati ya umeme katika Kijiji kizima cha Kisoko, Kata ya Kinyala wilayani Rungwe, ambapo wananchi wote wanaotumia umeme kijijini hapo wamejiunganishia kinyume cha sheria kwa kutumia nguzo na nyaya za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Ubainifu huo umefikiwa kufuatia operesheni inayoendelea wilayani humo ya kusaka wezi wa miundombinu na watumiaji haramu wa nishati hiyo, ambapo Afisa Usalama wa TANESCO, Aloyce Mndolwa, pamoja na Fundi Mkuu wa TANESCO Wilaya ya Rungwe, Himid Mwanzegule, wamethibitisha kuanza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote waliohusika na hujuma hiyo.
Kwa upande wao, viongozi wa eneo hilo akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasyeto, Charles Mbeye, wamekiri kuwepo kwa wimbi la vishoka wanaolaghai wananchi, huku baadhi ya wakazi wa Kisoko wamejitetea kuwa waliunganishiwa nishati hiyo bila kufahamu kuwa wahusika walikuwa vishoka na si watumishi halali wa shirika hilo.