Video: Kijiji kizima kimenaswa kimeiba umeme Mbeya

Duuu ! hatari wanakijiji wote wamekuwa wataalamu wa umeme. hapo kuna namna ya watumishi wasio waadilifu kutoka TANESCO wanacheza michezo kwa kushirikiana na wasio waadilifu kutoka kijiji hicho Tukisema tunataka KATIBA MPYA tunakuwa tunamaanisha..
Wamekoleza title kujisafisha na kutafuta kiki kuwa wanawajibika, iweje kijiji kizima, ni dhahiri tatizo liko upande wa shirika
 
.
 
Attachments

  • 20260930_221723.jpg
    20260930_221723.jpg
    57.6 KB · Views: 4
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mbeya limebaini wizi mkubwa wa nishati ya umeme katika Kijiji kizima cha Kisoko, Kata ya Kinyala wilayani Rungwe, ambapo wananchi wote wanaotumia umeme kijijini hapo wamejiunganishia kinyume cha sheria kwa kutumia nguzo na nyaya za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Ubainifu huo umefikiwa kufuatia operesheni inayoendelea wilayani humo ya kusaka wezi wa miundombinu na watumiaji haramu wa nishati hiyo, ambapo Afisa Usalama wa TANESCO, Aloyce Mndolwa, pamoja na Fundi Mkuu wa TANESCO Wilaya ya Rungwe, Himid Mwanzegule, wamethibitisha kuanza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote waliohusika na hujuma hiyo.

Kwa upande wao, viongozi wa eneo hilo akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasyeto, Charles Mbeye, wamekiri kuwepo kwa wimbi la vishoka wanaolaghai wananchi, huku baadhi ya wakazi wa Kisoko wamejitetea kuwa waliunganishiwa nishati hiyo bila kufahamu kuwa wahusika walikuwa vishoka na si watumishi halali wa shirika hilo.

View attachment 3689780
Duh vishoka nao!, Kijiji kizima ni wahujumu uchumi!
 
Watu wanaomba umeme, TANESCO mnalala vishoka wanatumia fursa vizuri.
Ila utakuta hao vishoka ni watumishi wa TANESCO
 
Habari, ndugu wateje wetu.

Tafadhali fahamu kuwa TANESCO inazingatia misingi ya uadilifu na uwajibikaji katika utoaji wa huduma. Mtumishi yeyote anayebainika kukiuka maadili au taratibu za kazi anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Aidha, tunawahimiza wananchi kushirikiana nasi kwa kutoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa, uunganishaji haramu wa umeme na ukiukwaji mwingine wa taratibu. Ni muhimu kutambua kuwa hata mteja anayebainika kutumia huduma iliyounganishwa kinyume cha utaratibu atawajibishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Hivyo, tunawasihi wote kuzingatia taratibu rasmi za kupata huduma ya umeme ili kuepuka usumbufu na kuhakikisha huduma salama na za kuaminika.

Asante. ^
Mlikua wapi mpaka mnaibiwa?
 
Asante. ^MY
Je waliunganishaje kutoka kwenye chanzo kikuu cha umeme?

Je walikuwa hawanunui Luku? Na kama wananunua si pesa ilikuwa inaingia moja kwa moja?
 
Back
Top Bottom