Video: Kijiji kizima kimenaswa kimeiba umeme Mbeya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mbeya limebaini wizi mkubwa wa nishati ya umeme katika Kijiji kizima cha Kisoko, Kata ya Kinyala wilayani Rungwe, ambapo wananchi wote wanaotumia umeme kijijini hapo wamejiunganishia kinyume cha sheria kwa kutumia nguzo na nyaya za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Ubainifu huo umefikiwa kufuatia operesheni inayoendelea wilayani humo ya kusaka wezi wa miundombinu na watumiaji haramu wa nishati hiyo, ambapo Afisa Usalama wa TANESCO, Aloyce Mndolwa, pamoja na Fundi Mkuu wa TANESCO Wilaya ya Rungwe, Himid Mwanzegule, wamethibitisha kuanza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote waliohusika na hujuma hiyo.

Kwa upande wao, viongozi wa eneo hilo akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasyeto, Charles Mbeye, wamekiri kuwepo kwa wimbi la vishoka wanaolaghai wananchi, huku baadhi ya wakazi wa Kisoko wamejitetea kuwa waliunganishiwa nishati hiyo bila kufahamu kuwa wahusika walikuwa vishoka na si watumishi halali wa shirika hilo.

Your browser is not able to display this video.
 
w
walijifunza kutoka Tume ya Uchaguzi, walivyoiba uchaguzi mzima full
 
Cha kufanya wawahoji hao wanakijiji,aliewaunganishia ni nani? Na walilipa kiasi gani ? maana ukisema wanakijiji wameiba umeme unakuwa unawaonea hizo mita ambazo ni mali ya tanesco walizitoa wapi kama sio tanesco?majizi yako tanesco sio wanakijiji
 
Wanakijiji wamesingiziwa tu
 
Habari, ndugu wateje wetu.

Tafadhali fahamu kuwa TANESCO inazingatia misingi ya uadilifu na uwajibikaji katika utoaji wa huduma. Mtumishi yeyote anayebainika kukiuka maadili au taratibu za kazi anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Aidha, tunawahimiza wananchi kushirikiana nasi kwa kutoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa, uunganishaji haramu wa umeme na ukiukwaji mwingine wa taratibu. Ni muhimu kutambua kuwa hata mteja anayebainika kutumia huduma iliyounganishwa kinyume cha utaratibu atawajibishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Hivyo, tunawasihi wote kuzingatia taratibu rasmi za kupata huduma ya umeme ili kuepuka usumbufu na kuhakikisha huduma salama na za kuaminika.

Asante. ^MY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…