Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Israel inashambulia majengo marefu sio kwasababu ya Hamas kufanyia shuglizao, bali Hamas wanatumia majengo hayo marefu kufyatulia makombora yanayotua kwenye miji mikubwa ya IsraelHilo jengo limekuwa targeted kwasababu Israel inasema linatumiwa na Hamas pia.. Hamas wanafanya shughuli zao humo kwa mgongo wa media
Mashambulizi ya makombora katika eneo la Gaza yanaingia siku ya sita mfululizo, huku idadi ya vifo ikiongezeka kufikia watu 140, wakiwamo watoto 39.
Israel imeendelea kutumia makombora kushambulia majengo marefu katika eneo la Gaza, ikilenga jengo la ofisi za Shirika la Habari la Al Jazeera na Associated Press (AP) siku ya Jumamosi.
Al Jazeera ilirusha mubashara picha za wakati kombora la Israel lilipopiga ofisi zake, hii ni baada ya uongozi wa Shirika hilo kupokea simu kutoka Jeshi la Israel likiwaonya kuwa watashambulia jengo hilo. Wafanyakazi wa mashirika yote mawili waliondoka kabla ya tukio hilo.
View attachment 1786135
Shirika hilo limeripoti kuwa wafanyakazi walipewa saa moja tu kuondoka ndani ya jengo hilo la Al Jalaa, lakini mmiliki wa jengo alijaribu kuwaomba wanajeshi wa Israel wamwongezee nusu saa nyingine ili watu waweze kutoa vifaa vyao kutoka ofisini. Jeshi la Israel lilikataa kuongeza muda na baada ya saa moja jengo hilo likashambuliwa kwa kombora.
“Ni uharibifu mkubwa. Mamia ya familia zimelazimika kuondoka katika jengo hilo na majengo mengine ya pembeni, hii inamaanisha kuwa sasa familia hizo zinaongezeka kwenye idadi ya maelfu wengine ambao hawana makazi. Hakuna sehemu salama tena ndani ya Gaza,” anasema Youma al-Sayed, Mwandishi wa Habari wa Al Jazeera wa Gaza.
Mkurugenzi Mkuu wa AP, ambayo ilikuwa ikitumia jengo hilo la Al Jalaa pamoja na Al Jazeera, amesema ameshtushwa na shambulio la Israel kwenye ofisi zao.
Kitendo hicho cha Israel kimelaaniwa vikali na Rashida Tlaib, Mjumbe wa Bunge la Congress nchini Marekani mwenye asili ya Palestina akisema kitendo cha kushambulia vyombo vya habari kinafanywa makusudi na Israel ili kuifumba macho dunia isione mauaji ya watoto na wazazi wa Kipalestina yanapofanyika.
Wakati huo, maandamano yanaendelea katika maeneo mbalimbali Magharibi mwa Ukingo wa Mto Jordan kupinga mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina, huku mzozo huo ukizorotesha hali ya kibinadamu katika eneo hilo. Maelfu ya Wapalestina wamekimbia makazi yao na kutafuta hifadhi katika majengo ya shule Kaskazini mwa Gaza yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa Wapalestina 10,000 wameyakimbia makombora ya Israel yanayoanguka katika nyumba zao.
Chanzo: Al Jazeera
Ki ukweli wale jamaa ni shidaa!!yaani ilikuwa live , sikuamini kama lile jengo lingedondoka pekee yake tu bila kukugusa yale mengine ya pembeni! Ila nasema hivi hawa israel wakisema wawamalize wapestina wote ni kazi ya masaa tu! Inabakia history! Kwani wakitaka kulipua jengo wanawapa taarifa kabisa kuwa mtoke haraka! Ila HAMAS naona kama wanawapa watu mateso tu bila sababu!!High tech demolition.. jengo moja tuu ndio lina dondoka.. mengine hata hayatikisiki.
Anapitia wapi kufika Gaza?Kwaninj Iran asipeleke jeshi hapo Gaza awafundishe adabu mazayuni
Una akili sana. Ndugu zetu waafrika wanauwawa uwasikii wakilaani kabisa. Hayo ya mashariki ya kati hayatuhusuWala haizunishi kuliko Msumbiji alshabab na isis wanachinja watu na hamna tamko lolote la kulaani kutoka kwenu. Israel iendelee na huu huu msimamo. Walijitakia wenyewe.
NO MERCY
Kwa hiyo kufatulia makombora yao siyo kutumia kwa shuguli zao?.Israel inashambulia majengo marefu sio kwasababu ya Hamas kufanyia shuglizao, bali Hamas wanatumia majengo hayo marefu kufyatulia makombora yanayotua kwenye miji mikubwa ya Israel
Kama wanachagua jengo la kudondosha bila mengine kuathirika je wakiamua kuyaharibu yote si inakuwa vumbi tuKi ukweli wale jamaa ni shidaa!!yaani ilikuwa live , sikuamini kama lile jengo lingedondoka pekee yake tu bila kukugusa yale mengine ya pembeni!!!ila nasema hivi hawa israel wakisema wawamalize wapestina wote ni kazi ya masaa tu!!inabakia history!!kwani wakitaka kulipua jengo wanawapa taarifa kabisa kuwa mtoke haraka!!ila HAMAS naona kama wanawapa watu mateso tu bila sababu!!
teknolojia mpya hii usicheze na idfHigh tech demolition.. jengo moja tuu ndio lina dondoka.. mengine hata hayatikisiki.
We jamaa.muongo kinouma[emoji2][emoji2][emoji2]israel anaangusha majengo wakati hamas wanazidi kukomboa vitongoji kazaa jana marekani imetuma wanajeshi wake kadhaa huko
Hapo ndio kwao mlitaka wakau Uganda wakakataaKwanini UN iliamua kuwaleta waisrael mashariki ya kati karibu na hao wapalestina kwani hamna sehemu nyingine ?
Hawa jamaa ni shidaDah! Israel habari nyingine, yaani kombora linashusha jengo moja na kuacha mengine.
Hapo wametuma ujumbe fulani na umepokelewa na walengwa.
Kha! We jamaa huna hata aibuisrael anaangusha majengo wakati hamas wanazidi kukomboa vitongoji kazaa jana marekani imetuma wanajeshi wake kadhaa huko