Wewe unafikiri wakati Mandela apipokua kifungoni alikua anatamka maneno ya kuwapenda makaburu ?
Hebu tutumie akili zetu vizuri ili hata watakao kuja baadae wajue kuwa tulishauri mambo mazuri.
Mandela amewasamehe Makaburu baada ya kutoka Gerezani na kuwa Rais.
Makaburu walikuwa weshaweka Sheria na katiba isigoruhusu tena Ubaguzi na wakaruhusu Shughuli za kisiasa ndio maana mandela aliposhinda walimtangaza.
Makaburu na unyama wao lakini hawakuvuruga uchaguzi ili waonekane kuwa wameshinda kisanii , walimpa ushindi Mandela ili amani irejee.
Kwa hiyo na usomi wako kabisa unaona kuwa Katiba ya Tanzania inaweza kuitawala Afrika Kusini hata mwaka mmoja bila kutokea vita ya makabila.? Katiba inayotoa mwanya kwa watawala waliochaguliwa kidemokrasia kuongoza nchi kijeshi haiwezi kuvumiliwa na Wazulu.
Usifikiri Serikali ya Afrika ya kusini ni wajinga kutumia nguvu ya kadiri kuwanyamazisha waandamanaji wa kule.
Wale wanawajua watu wao walivyo. AFRIKA kusini na ubabe wote wa makaburu lakini walishindwa kuzuia vurugu za kujitoa mhanga za wapigania uhuru.
Na nakuahakikishia hata tanzania kama CCM na serikali yake hawatabadilika nchi hii haina miaka 20 mbele bila watu kutoana ngeu. Vita ni ya Mungu siku zote . Wewe usije ukadhani bimadamu wote unaowaona wamezaliwa kwa ajili ya kula bata huku wenzao wakiwa wananyanyaswa . Hapana hata kidogo kuna watu wamezaliwa kwa ajili ya wengine , hao tangu enzi na enzi wapo. Hata uwaue watu kwa mabomu ya sumu kama alivhofanya Sadam lakini watapinga dhulma kwa nguvu zote.
Lisu alisema wazi kuwa kama angechaguliwa basi angeunda tume ya maridhiano ili waliofanya makosa wakiri na kuwaomba msamaha waliowakosea. Hakuwahi kusema kuwa atalipa Kisasi.
Na pakiwa na Katiba bora hata kisasi hakina maana .Waovu watajivua wenyewe kwenye uongozi.
Haiwezekani uwe na Mkurugenzi anayevuruga uchaguzi kwa wazi kabisa bila hata kificho halafu aendelee kukalia ofisi kwa sababu tu anateuliwa na amiri Jeshi mkuu na mtu anayeteua majaji wote kama apendavyo halafu unasema kuwa katiba hiyo ni nzuri.
Haijawahi kutokea kwenye historia kundi moja ndani ya jamii likawatesa wengine muda wote kwa sababu ya uimara wa Jeshi au silaha. Uimara wa jeshi ni kusimamia Haki sio kupora haki.
Unajua Osama bin Ladeni shujaa kwa Waarabu na waislam wanaoishi leo kwa amani Ulaya na Marekani . Kama sio amsha amsha ya Osama mpaka leo wasilam na Waarabu wangekua wamabaguliwa na dini yao kudharauliwa Ulaya. Kuheshimu na kumtendea mtu haki bila kujali dini yake na itikadi yake ni msingi wa amani.
Kosa la Lisu ni Lipi.?
Je, nani angefurahi kuona ndugu yake au kiongozi anayempenda anapigwa risasi bila kosa lolote?
Nani asiyejua kuwa Lisu alianza kupigania maslahi ya nchi hii kwa miaka mingi wakati hao waliokua wananugaika ndio awaliokuja kujiita wazalendo feki ili kulinda vyeo!!?
Je, kama Lisu angekua mbunge wa CCM angepigwa risasi bila mtu yeyote lukamatwa ? Yani hakuna hata mtu aliyetangaza kuwa kuna mtu anashikiliwa kwa mahojiano ?
Mungu tunayemwamini ataliweka sawa Taifa hili wala hatuna shaka na hilo. Tumechoka kutawaliwa na watu waovu ,washirikina ,wauaji,wezi, wanafiki,wazinzi,walevi,wachawi na watesaji wasiofuata sheria ama za dini au hata walizoweka wenyewe.
Ije katiba mpaya ama ya zamani Siku Kikombe cha ghadhabu ya Mungu kikijaa atajibu kwa Moto.
Ogopa mtu unayemdhulumu halafu halafu hana uwezo wa kujitetea ni bora anayepambana mana atatumia nguvu zake. Asiyepambana anamwachia Mwenyezi apambane kwa haki.
Tanzania hata wakaoloni waliondoka kwa Dua tu za Wazee wa Kiislam kwa amani na Upendo kabisa bila kuuana. Kama wageni walikaa pembeni kwa amani basi hata Wakoloni weusi wa leo wataondoka kwa amani tu mana wao ni ndugu zetu wa damu.
Katiba Mpya ni muhimu ihi hii yenye ladha ya mkoloni iondoke na viashiria vyake vyote vya kikoloni.