VIDEO: Lori laanguka Morogoro, wananchi wakimbilia kuchota mafuta

Lori la mafuta (ambayo bado hayajathibitishwa kuwa ya aina gani) ambalo limeelezwa kuwa lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro limepinduka eneo la kijiji cha Mwidu mkoani Morogoro huku wananchi wakionekana kubebelea madumu kwa ajili ya kuchota mafuta hayo.

Hapo Moro hawakomi??
Hawakujifunza kwa iliyopita???
 
black gold hiyo...jamaa kaondoka na dumu 6 sawa na lita 120 za petrol

120x2700 =324000 chap...akirudi mara tatu ana milioni yake
 
Akirudi hiyo mara ya tatu sasa mana hapo ziraili anapenda watu wajae jae , anaenda baba anarudi na mzigo hapo akirudi tena anakuja na wanae watatu wanabeba wakifikisha mzigo home mama nae anaona yanini nijikalie nna marejesho mama nae huyoo anaunga trela hapo familia nzima inatia maguu hapo ndo muda wa wachomoa betri kwa hisani ya ziraili sasa inaonekana shwaaaaaaah kama kilio kijacho cha LBL
 
Lori la mafuta (ambayo bado hayajathibitishwa kuwa ya aina gani) ambalo limeelezwa kuwa lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro limepinduka eneo la kijiji cha Mwidu mkoani Morogoro huku wananchi wakionekana kubebelea madumu kwa ajili ya kuchota mafuta hayo.

Washasahau ule msala wa moto uliotokea hapohapo moro miaka michache iliyopita sababu ya wizi wa mafuta baada ya Lori kupinduka
 
black gold hiyo...jamaa kaondoka na dumu 6 sawa na lita 120 za petrol

120x2700 =324000 chap...akirudi mara tatu ana milioni yake
Milioni si kitu mbele ya kifo na akizoea hvo atkuja kufa huko huko
 
Back
Top Bottom