VIDEO: Lori laanguka Morogoro, wananchi wakimbilia kuchota mafuta

VIDEO: Lori laanguka Morogoro, wananchi wakimbilia kuchota mafuta

Hakuna aijuaye kesho yake, acha watu/walalahoi wenzangu wajizolee rizki, chochote kikitokea potelea pote tunasema ajali kazini
 
Yaani wanaenda kuchukua mali ya mtu mwingine. Maana yake ni wezi na yawapasa kushughulikiwa na mamlaka husika
 
Mkuu unaujua msoto wa mlo mmoja wewe?
Uliona waliolipukiwa na mafuta wakati ule? Unafikiri hata huo mlo waliula? Kuna fursa ila hiyo ya ajali ya magari ya mafuta ni fursana, ni mawili kuishi na majeraha ya kuungua na kifo.
 
Naskia moto ukiwaka unafatilia mafuta pale yalipokuwa yanadondoka
 
Lori la mafuta (ambayo bado hayajathibitishwa kuwa ya aina gani) ambalo limeelezwa kuwa lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro limepinduka eneo la kijiji cha Mwidu mkoani Morogoro huku wananchi wakionekana kubebelea madumu kwa ajili ya kuchota mafuta hayo.

Tena?!
Njaa mbaya sana sana sana!
 
Lori la mafuta (ambayo bado hayajathibitishwa kuwa ya aina gani) ambalo limeelezwa kuwa lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro limepinduka eneo la kijiji cha Mwidu mkoani Morogoro huku wananchi wakionekana kubebelea madumu kwa ajili ya kuchota mafuta hayo.

..YAMESHASAHAU MSAMVU-MORO 2019, zaidi ya watu 100 waliteketea kwa moto
 
Hawa wamekubaliana hakuna kuchomoa betri 😀😀😀
 
Back
Top Bottom