Video: Malasusa aelezea sababu ya kutofungua Jeneza la Lowassa

Papa John Paul wa Pili mwenyewe aliagwa kwa watu kumtazama, Nyerere hata Magufuli. Malasusa aseme tu kuwa huo ni utashi wa kifamilia, ila kutafuta sababu za kidini hapana. Kawaida kuna open na closed casket service. Ni utashi wa familia kuchagua aina ya utaratibu wa kuaga (ama kwa nchi za wenzetu marehemu wengine husema kabisa kabla hajafariki atapenda iweje wazi ama afunikwe)
 
Ni kweli sioni mantiki ya kuaga marehemu, kwa suala la mazishi nawapongeza waislamu, mtu akishakufa siku ya mazishi hakuna kupoteza muda kama sisi wakristo.
Safi, njoo huku kwetu Mkuu! Taqbir....
 
Kama ndivyo si wazike tu?????

Au jeneza limejazwa mipesa yake ya reach at Monduli???!
 
Sasa kwanini hamsemi hilo?
miaka yote watu wanahangika na kipengele ambacho si cha lazima kumbe kunako 'protokali' ya kuwahifadhi jamaa zetu, mambo mengine yanachosha aisee.
 
Analeta siasa kwenye mazishi!
Kwa nini huo utaratibu ulivyoanza tu haukuzuiliwa? Kama jambo hilo alilolisema ni la kibiblia, mbona hatusaidii mistari?! Halafu anavyoongea ni kama familia ndio walioamua jeneza lisifuguliwe, kama wangefungua, je angeruhusu?
 
Naona picha kubwa hapo kama ya Yesu au ya Maria... namsikia salamu yake akisena tumsifu yesu Kristu..... hiyo ni madhabahu ya kanisa gani?
 
Mambo mengi ni mindset tu
Kuaga mara ya mwisho sielewagi hata maana yake nn maana hata kabla ya kufariki unakuta mlishaonana kwa mara ya mwisho
Kwa wale ambao hawajaonana nae kwa mara ya mwisho, mfano, wewe uko Kenya, ndugu yako akafariki na ukaja kumzika, hamjaonana muda hata miaka 2 ama 3, nafasi ya kuonana nae mara ya mwisho hukuipata, hapo una maoni gani mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…