Video kamili ya hili suala
ipo hapa naomba tuiangalie hii video bila kuwa na upendeleo.Mbunge aliyetoa mfano wa msaliti vitani ni Mheshimiwa Bulembo aliongea muda wa dakika ya 13:44-14:56 (1min 12sec).Ukimsikiliza hapo utagundua amesema "mkiwa vitani pale kagera Tanzania inapigana na Uganda,akitoka mtu mmoja akapeleka habari zetu,hatakiwi kuvuka kurudi anatakiwa auwawe kulekule".
Mheshimiwa amesema mkiwa Kagera mnapigana na Uganda.Sasa huu ulikuwa ni mfano,sasa kwa nini watu wanang'ang'ania mfano kwamba ndicho kilichokusudiwa kifanyike?Na utaona mfano huu aliutoa kama utangulizi,ndiyo maana baada ya kumaliza mfano huo akasisitiza "usaliti".
Nakubali wabunge wengi wamesema Zitto amesaliti lakini je walipendekeza auawe?Angalia video hiyo natoa summary ya kila alicyechangia na alichpendekeza mwishoni.Mimi binafsi sijamsikia mbuge yeyote akisema Zitto auawe,kwa hiyo mnaosambaza taarifa kwamba wabunge wataka Zitto auawe hamko sahihi na mnaposema mama Rwakatale kashangilia kuuawa kwa Zitto bado ni uongo juu ya uongo,huyo mama alipiga meza kussupport msaliti vitani auawe.
Summary
1.Bulembo 13:44-14:56 (1min 12sec)
"Huyu mtu kazoea anatakiwa apate kiboko kizuri sana"
2.Mhesh: Kessy: huyu ni mtu hatari,unaenda kusaliti nchi nchi za nje unafaa?hufai hata kidogo (time 13:15-13:42)
3.Mhe:Janeth Mbene ;"Zitto amepotosha kwa makusudi kwa ajenda yake binafsi ya kuleta fujo nchini kwetu"(muda 15:03-17:28)
4.Mhesh.Mary Chatanda :muda 17:30-18:13
"Ametusaliti kutumia nembo ya Bunge kinyume na sharia,"
ni vizuri akapatiwa adhabu anayostahili ( 18:08-18:13)
5.Mhesh.Stanslaus Mabula: Amepotosha(19:45-20:17),”Bunge lako kama lina namna ya kuchukua hatua ni lazima tufanye kazi ya kuijenga nchi na siyo kuibomoa”
6.Mhesh:Juma Nkamia:muda 20:20-22:58
"Tufike hatua watu wa namna hii wanayoiyumbisha nchi wachukuliwe hatua(muda 22:50-22:58)"
7.Mhesh Dr.Godwin Moleli: kwa kufuata taratibu za Bunge,kwa kufuata kanuni za nchi na sheria za nchi ninakuomba hili jambo liende kwenye mfumo ambao utatuletea watu wa aina hiyo ambao wanasaliti taifa hili wanatakiwa kufanywa nini,na isiishie hapo……..”(muda 23:50- 24:15)
Hata speaker wa Bunge alivyomalizia lilipeleka kwa mwana sheria mkuu wa serikali aliangalie.Kwa hiyo mimi binafsi sijaona popote ambapo kuna mbuge ameshauri Zitto auawe.Ushauri:Tuwe makini,matatizo au mafanikio ya mwanadamu huanza kama wazo na baadaye hutekelezwa katika mwili.Tusitumie nafasi zet vibaya au influence tuliyo nayo kwenye jamii vibaya.
peaker alitoa dakika 3 kwa kila mtu,video hii ina sec 16 tu, 3min=3x60=180sec
Je 16sec ni asilimia ngapi ya muda wote=16/180=0.0889=8.89% asilimia zaidi ya 90 ya maongezi ya Mhesh.Bulembo haijawekwa kwenye hii clip chochezi.