Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Nimeusikiliza huu mjadala, kiukweli baadhi ya wabunge wametoa kauli kali na hatarishi, ikiwemo kauli ya kifo kwa Mhe. Zitto Kabwe, ni ajabu kwa Mbunge Mlokole, Mchungaji Rwakatare, kushangilia mtu auawawe!.

Naendelea kusisitiza kuhusu kauli huumba, kauli kama hii ilitolewa kumhusu Lissu na mara ikatekelezwa, sasa ni kumhusu Zitto, bahati nzuri Zitto ni mtu wa Kigoma, mwisho wa reli, na kule kwao, kaaga!, likimtokea la kutokea, kwa mujibu wa Zitto mwenyewe, hawa waliochangia adhuriwe, kule majumbani kwao, hakuta salia hata panya alive!.

P


Msukuma mtabiri! Edelea kututabiria na kwa wengine mkuu
 
Video kamili ya hili suala ipo hapa naomba tuiangalie hii video bila kuwa na upendeleo.Mbunge aliyetoa mfano wa msaliti vitani ni Mheshimiwa Bulembo aliongea muda wa dakika ya 13:44-14:56 (1min 12sec).Ukimsikiliza hapo utagundua amesema "mkiwa vitani pale kagera Tanzania inapigana na Uganda,akitoka mtu mmoja akapeleka habari zetu,hatakiwi kuvuka kurudi anatakiwa auwawe kulekule".

Mheshimiwa amesema mkiwa Kagera mnapigana na Uganda.Sasa huu ulikuwa ni mfano,sasa kwa nini watu wanang'ang'ania mfano kwamba ndicho kilichokusudiwa kifanyike?Na utaona mfano huu aliutoa kama utangulizi,ndiyo maana baada ya kumaliza mfano huo akasisitiza "usaliti".

Nakubali wabunge wengi wamesema Zitto amesaliti lakini je walipendekeza auawe?Angalia video hiyo natoa summary ya kila alicyechangia na alichpendekeza mwishoni.Mimi binafsi sijamsikia mbuge yeyote akisema Zitto auawe,kwa hiyo mnaosambaza taarifa kwamba wabunge wataka Zitto auawe hamko sahihi na mnaposema mama Rwakatale kashangilia kuuawa kwa Zitto bado ni uongo juu ya uongo,huyo mama alipiga meza kussupport msaliti vitani auawe.
Summary

1.Bulembo 13:44-14:56 (1min 12sec)

"Huyu mtu kazoea anatakiwa apate kiboko kizuri sana"

2.Mhesh: Kessy: huyu ni mtu hatari,unaenda kusaliti nchi nchi za nje unafaa?hufai hata kidogo (time 13:15-13:42)


3.Mhe:Janeth Mbene ;"Zitto amepotosha kwa makusudi kwa ajenda yake binafsi ya kuleta fujo nchini kwetu"(muda 15:03-17:28)

4.Mhesh.Mary Chatanda :muda 17:30-18:13

"Ametusaliti kutumia nembo ya Bunge kinyume na sharia,"

ni vizuri akapatiwa adhabu anayostahili ( 18:08-18:13)

5.Mhesh.Stanslaus Mabula: Amepotosha(19:45-20:17),”Bunge lako kama lina namna ya kuchukua hatua ni lazima tufanye kazi ya kuijenga nchi na siyo kuibomoa”

6.Mhesh:Juma Nkamia:muda 20:20-22:58

"Tufike hatua watu wa namna hii wanayoiyumbisha nchi wachukuliwe hatua(muda 22:50-22:58)"

7.Mhesh Dr.Godwin Moleli: kwa kufuata taratibu za Bunge,kwa kufuata kanuni za nchi na sheria za nchi ninakuomba hili jambo liende kwenye mfumo ambao utatuletea watu wa aina hiyo ambao wanasaliti taifa hili wanatakiwa kufanywa nini,na isiishie hapo……..”(muda 23:50- 24:15)

Hata speaker wa Bunge alivyomalizia lilipeleka kwa mwana sheria mkuu wa serikali aliangalie.Kwa hiyo mimi binafsi sijaona popote ambapo kuna mbuge ameshauri Zitto auawe.Ushauri:Tuwe makini,matatizo au mafanikio ya mwanadamu huanza kama wazo na baadaye hutekelezwa katika mwili.Tusitumie nafasi zet vibaya au influence tuliyo nayo kwenye jamii vibaya.

peaker alitoa dakika 3 kwa kila mtu,video hii ina sec 16 tu, 3min=3x60=180sec

Je 16sec ni asilimia ngapi ya muda wote=16/180=0.0889=8.89% asilimia zaidi ya 90 ya maongezi ya Mhesh.Bulembo haijawekwa kwenye hii clip chochezi.
Aqua, ulitumia nguvu nyingi kutetea ujinga wako. Halafu unabishana na wabobezi kama Pascal Mayalla !! haya njoo uandike tena utumbo wako
 
Ndugali na murembo wawahi kuomba msamaha kwa zitto kabwe kabla mizimu yake haijasara kama ilivyomsalia mchungaji
 
Sikubaliani na Msimamo wa Zitto Kabwe kwa asilimia zote , ila vitisho vya kuuana hapana

Bulembo kakosea sana sana sana

Hii record inaweza kumpeleka The Hague kimasihara.masihara yakitokea madhara kwa Zitto

Angekuwa ANATAFAKARI, Bulembo angerejea mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya Kimbar Arusha


Augustine Pinochet wa Chile, Slobadan Milosovic wa Yugoslavia moja ya mambo yaliyowagharimu ni 'ndimi' zao

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmh
 
Kwa kweli inabidi kama kuna wauaji wachangiwe tu pesa na hawa wabunge wa CCM maana kujenga hoja hawawezi tena. Zitto kaandika barua katoa hoja zimeeleweka na World Bank na nyie jibuni basi mpangue hoja zake, mnashindwa nini? Mnakimbilia kuua ua tu kama mlivyotaka kumfanya Lissu

So pathetic mnadhani ni Zitto peke yake, kulikuwa na pettition online ya hilo suala na World Bank walikuwa tagged. Ili kuwa na sigantures zaidi ya 10,000 mimi mwenyewe niliandika emails, World Bank ilikuwa flooded na emails zikilalamika udikteta wa awamu ya tano.

View attachment 1346062

Endeleeni kulala tu maana mmejaza vilaza kwenye hilo chama chakavu.

Mwisho HONGERA sana mama mchungaji nimeona unakenuaaaaa uliposikia WITO WA ZITTO KABWE KUUULIWA no wonder wanasemaga ulizika makondoo hai kwenye geti la St. Mary's School na kanisani kwako FULL MAKAFARA ya damu.

View attachment 1344066
Hakuna binadamu aliyekamili, tumuachie Mungu kwenye hili.
Tushukuru kwa maisha yake hapa Duniani kuna mazuri pia amefanya tuyahubiri pia humu jamii forum
 
Kumbe mambo yalianzia huku hivi kwanza unaanzaje kuongea maneno mabaya kwa Zitto labda na wewe uwe mzito kama Zitto mwenyewe.
 
Kwa kweli inabidi kama kuna wauaji wachangiwe tu pesa na hawa wabunge wa CCM maana kujenga hoja hawawezi tena. Zitto kaandika barua katoa hoja zimeeleweka na World Bank na nyie jibuni basi mpangue hoja zake, mnashindwa nini? Mnakimbilia kuua ua tu kama mlivyotaka kumfanya Lissu

So pathetic mnadhani ni Zitto peke yake, kulikuwa na pettition online ya hilo suala na World Bank walikuwa tagged. Ili kuwa na sigantures zaidi ya 10,000 mimi mwenyewe niliandika emails, World Bank ilikuwa flooded na emails zikilalamika udikteta wa awamu ya tano.

View attachment 1346062

Endeleeni kulala tu maana mmejaza vilaza kwenye hilo chama chakavu.

Mwisho HONGERA sana mama mchungaji nimeona unakenuaaaaa uliposikia WITO WA ZITTO KABWE KUUULIWA no wonder wanasemaga ulizika makondoo hai kwenye geti la St. Mary's School na kanisani kwako FULL MAKAFARA ya damu.

View attachment 1344066
hivi huyu bulembo na zitto si mtu na mkwewe?
 
Back
Top Bottom