VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

Kwanza nimpe pole sana mshikaji wangu Roma na wenzake kwa madhila waliyoyapata, kwa hakika mashetani haya yameshindwa na yataendelea kushindwa tu.Nayaita maharamia haya mashitani kwa sababu kitendo cha kutekwa na koptezwa kwa msanii huyo kilikua cha kishetani na kiharamia.Niende mbali zaidi kwa kusema kua huenda yalikua magaidi kama walivyo Alshababu.


Baada ya kutoka kule kituo cha polisi ambapo walienda kutoa ushahida,msanii Roma na wenzake waliotoka kuelekea majumbani kuonana na familia zao ingawa waliokua dhoofu bin hali.
Alipoulizwa na waandishi wa habari waliokua wapi?alishikiliwa na nani?amefanyiwa nini?ameona nini na anasemaje? Amesema hawezi kuongea chochote kulingana na masharti ya kuachiwa kwao ispokua mengi atayasema siku ya jumatatu.


SWALI,

1.Hivi ni kweli Roma ataweza kua na ujasiri wa kusema lolote juu ya masharti aliyopewa zaidi ya kuwapgopa watesaji hao? je, kama watesaji walikua ni maharamia tu na sio vyombo vyetu vya dola atapgopa nini kuwataja au kufunguka wazi?

2.Au atasingizia kua anapisha uchunguzi na upelelezi wa kipolisi hivyo hawezi kusema chochote juu ya yaliyompata?

3.Sio ataogopa kupotezwa mazima?Maana juzi hata baada ya msanii Nay wa Mitego kuachiwa tu akasema kua yeye hana chama ilihali umma unaijua kadi yake.


4.Tuna vyombo vyenye dhamana ya kulinda usalama wa raia, Roma awe muwazi tu kuuambia umma tu alikua wapi maana kwa sasa yuko salama na anatambua kua lazima kuanzia sasa awe na tahadhari kubwa.

5.Ujasiri wa Roma Mkatoliki tuujuavyo utakuwepo tena? Au alikua akiongea na kuimba kwa vile hayajawahi kumkuta?Rejea wimbo wake wa "Mkanitupe Segerea"

Labda kuna movie inapangwa! Nasisitiza LABDA kwani sina uhakika. Labda ni mpango uliopagwa na kina Bashite na watasema walitekwa na kundi la watu wasiowajua. Nia ni ili ionekane kuwa kuna kikundi cha kuteka watu hapa Bongo. Ni ikishaonekana kuna kikundi kama hicho itakuwa rahisi kuwalisha watu uongo kuwa Ben Saanane alitekwa na kundi kama hilo. ( NB: nimefikiria hivyo kwani tangu Clouds Media ivamiwe na Nape kuonyeshwa silaha hadharani watu wengi wameanza kufunguka macho na kuhisi kuwa hata Ben Saanane yalimpata mambo kama hayo kutoka kwa hao hao watu)
 
Hawezi sema lolote
Na anaweza akahama kabisaa nchini tusimuone...
 
Hawataongea chochote cha maana jumatatu

Kama alikuwa anachechemea alafu anasema wao ni wazima kabisa,what do u expect "in Darasa's voice"

Bashite atakuwa kawatisha vya kutosha, na kama watakuwa wametishiwa kuuwawa basi Roma ataanza kuimba kwaya
 
Nimeomwona roma akiwa natembeakama kaumizwa mguu na mkono , je kuna report yoyote ya daktari ,nini hasa chanzo cha kuumia ?je alipelelkwa hospitali mara baaada ya kupatikana maana taarifa ilitolewa kuwa amaepatina na yupo kituo cha polisi
 
Hapo kaambiwa cha kuongea. Please Roma sema ukweli ulipelekwa wapi na nani alikupeleka? Bila kusema ukweli kilio cha wengi kitakuwa juu yako maana kuna watu wamelia usiku na mchana na wengine walishindwa hata kutimiza haja ya ndoa zao juu yako na wengine hadi sasa wanashinikizo la damu juu yako na wengine wamekosana na jamii nzima juu yako. No! u need to be frankly Roma plz. U will be cursed if u can speech wrong.
 
VIVA ROMA MIE NAKUOMBEA AFYA ITENGAMAE.SIJUI HUKO ULIPEWA UJI WENYE CHUMVI AU PANADOL.NAHISI KULIA.MUNGU NDO MJUZI.
 
Ingekuwa mimi jumatatu ni mbali sana ukweli wote ungekuwa nje!
Mkuu mambo mengine hayawezi kueleweka mpaka yakukute. Hapa iko namna.
Katika hali ya kawaida haiwezekani nchi iwe na vyombo vyote vya usalama kisha mtekaji wa kawaida tu akuachie kwa makubaliano maalum wakati wewe si mhalifu.
Kwa maana nyingine nyingine huyo mtekaji atakuwa yuko juu ya sheria.
 
Nimeomwona roma akiwa natembeakama kaumizwa mguu na mkono , je kuna report yoyote ya daktari ,nini hasa chanzo cha kuumia ?je alipelelkwa hospitali mara baaada ya kupatikana maana taarifa ilitolewa kuwa amaepatina na yupo kituo cha polisi
Sisi ndio tumeona hilo ila yeye anasema wao ni wazima kabisa
 
kwa n ninavyofaham watanzania walivyokuwa waoga, Roma hata sema jambo la msingi zaid ya kumung'unya maneno na kuacha ukwel! roma hapaswi kuficha ukwel wa jambo lililompata! mchawi mpe mtoto akulele,lait kama ningekuwa mm hyo kesho ningesema yote na kuitangazia dunia jins Tanzania ya leo ilivyo! Roma we2 n jasir na kama unapitia hum jf soma mchango wangu wa kimawazo,unapaswa kusema kile kilichokupata na ikiwezekana anika watu wote waliotaka kuhujum uhai wako kwan familia,wazaz na jamii inayopenda aman ktk nch h imesikitishwa sana na tukio lililokupata na we2 ukikaa kimya kama alivyokaa kimya Dr Ulimboka h hal itaendelea hasj ktk utawala huu wa Maguful! Binafs nimeguswa na hupasw kuficha ukwel kwa 2kio hl na mengne yaliyopta! Roma unapaswa kuwa jasir ktk jambo hl la sivyo utamung'unya 2 maneno na kuuficha ukwel,nape jana kasema ukwel na mwenye akil ametambua nn kinachojir ktk utawala huu!
 
Hapo kaambiwa cha kuongea. Please Roma sema ukweli ulipelekwa wapi na nani alikupeleka? Bila kusema ukweli kilio cha wengi kitakuwa juu yako maana kuna watu wamelia usiku na mchana na wengine walishindwa hata kutimiza haja ya ndoa zao juu yako na wengine hadi sasa wanashinikizo la damu juu yako na wengine wamekosana na jamii nzima juu yako. No! u need to be frankly Roma plz. U will be cursed if u can speech wrong.
Labda akubali kujitoa muhanga kama alivyoimba kwenye wimbo wake

Aseme ukweli na kuwa tayari kwa lolote

Ingawa ninahisi hatasema ukweli, watakuwa wamepewa vitisho vya kutosha, si kwa kuchechemea kule
 
Na ole wake awe anatumika, ntamtoa kwenye ubongo wangu
Haya maneno angeyaongea mke wake ambaye alikuwa analia kwa uchungu ningwez nikaelewa. Lakini wewe shabiki wake tu ambaye sio ajabu hata kazi zake hununui unataka kumtoa kwenye ubongo kisa unataka afanye yanayokufurahisha bila kujali madhila anayopitia.

Huu muziki sio wa kitoto, ni mapambano ya uhai na kifo, Roma ndiye anayejua acheze kete ipi ili ltokee nini kwa maslahi ya maisha yake na familia yake. Ben yuko wapi!

Ni lazima tukumbuke 'Adhabu ya kaburi aijuaye ni maiti' Uliye hai kaa kimya.
 
Mhhh Ruge againa aiseee huyu jamaa ameishika vibaya aanaa Industry ya mziki maana wasanii wote wa bongo amewaweka chini mpaka anaitwa boss no wonder lady jaydee hamfagilii kabisaaa
 
Mungu aniepushe sijui lini nitakuja kumtamkia binadamu mwenzangu boss au kumuita boss......
 
Hakuna jipya watu wanacheza na Akili za Watanzania,
Watanzania fanyeni kaz umli unakwenda
 
Back
Top Bottom