VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

Wanaonekana hawapo sawa kabisa...

Wapo sawa na wame act hao....believe me or not hao walishikiliwaa kwa 2 days na wamepatikana unadhani wale waliowashilikia na kuwateka wangewaachia??ni mchezonambao umefanyika hapa
 
Alafu police wanasema watafanya upepelezi wa nini hasaaa si hao wakina roma wasema walipokuwepo ili wale watu wakamatwe kwanza ndio upepelezi uendeleee ila wanafanyiwa kwanza interview kabla ya kuwakamata wahusika wakiondoka??
 
Nimeomwona roma akiwa natembeakama kaumizwa mguu na mkono , je kuna report yoyote ya daktari ,nini hasa chanzo cha kuumia ?je alipelelkwa hospitali mara baaada ya kupatikana maana taarifa ilitolewa kuwa amaepatina na yupo kituo cha polisi
Atakuwa kapigwa magongo ya chini ya nyayo ili afunguke zaidi,,,,kesho unaweza ukasikia anasema wapinzani ndio walimteka,, nchi hii
 
Kwanza nimpe pole sana mshikaji wangu Roma na wenzake kwa madhila waliyoyapata, kwa hakika mashetani haya yameshindwa na yataendelea kushindwa tu.Nayaita maharamia haya mashitani kwa sababu kitendo cha kutekwa na koptezwa kwa msanii huyo kilikua cha kishetani na kiharamia.Niende mbali zaidi kwa kusema kua huenda yalikua magaidi kama walivyo Alshababu.


Baada ya kutoka kule kituo cha polisi ambapo walienda kutoa ushahida,msanii Roma na wenzake waliotoka kuelekea majumbani kuonana na familia zao ingawa waliokua dhoofu bin hali.
Alipoulizwa na waandishi wa habari waliokua wapi?alishikiliwa na nani?amefanyiwa nini?ameona nini na anasemaje? Amesema hawezi kuongea chochote kulingana na masharti ya kuachiwa kwao ispokua mengi atayasema siku ya jumatatu.


SWALI,

1.Hivi ni kweli Roma ataweza kua na ujasiri wa kusema lolote juu ya masharti aliyopewa zaidi ya kuwapgopa watesaji hao? je, kama watesaji walikua ni maharamia tu na sio vyombo vyetu vya dola atapgopa nini kuwataja au kufunguka wazi?

2.Au atasingizia kua anapisha uchunguzi na upelelezi wa kipolisi hivyo hawezi kusema chochote juu ya yaliyompata?

3.Sio ataogopa kupotezwa mazima?Maana juzi hata baada ya msanii Nay wa Mitego kuachiwa tu akasema kua yeye hana chama ilihali umma unaijua kadi yake.


4.Tuna vyombo vyenye dhamana ya kulinda usalama wa raia, Roma awe muwazi tu kuuambia umma tu alikua wapi maana kwa sasa yuko salama na anatambua kua lazima kuanzia sasa awe na tahadhari kubwa.

5.Ujasiri wa Roma Mkatoliki tuujuavyo utakuwepo tena? Au alikua akiongea na kuimba kwa vile hayajawahi kumkuta?Rejea wimbo wake wa "Mkanitupe Segerea"
alikuwa wapi alikuwa na wanaume wa kazi kazi!ajifunze nyimbo za kutunga na kuimba akiinba asiwaseme wasanii wenzake vibaya na kutukana watu,akuna m babe aliye juu ya m babe mwenzie,

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Roma usipotuambia ukweli basi ukitekwa tena hakuna atakayekutetea,Umetoka kwenye gari unachechemea,mikono na miguu umechubuka halafu unatuambia kwamba upo safi kabisa,Ongea ukweli,Tunajua ulitekwa na Kikundi cha BASHITE na usipoongea ukweli basi na wewe tutakuweka kwenye mkakati alioufanya bwana bashite na BabuTale/WCB.
 
Nawashauri hivyo maana kutekwa na kuachiwa lazima ujiulize zaid ya mara 10 maana ninini hasa malengo ya watekaji na je wamefanikiwa walicho hitaji?na kama wamefanikiwa kwa mbinu gani?nina mashaka kabisa nanhawa watekaji wasije fanya kama walivyo mfanya huyu waziri wa habari mpya miaka ile.
 
Roma anaonekana kuteswa sana!amevimba pia,anachechemea japo kasema yeye ni mzima
Inaniumiza sana!
Millard ayo amepost insta na cloudfm pia wamepost clip ya video alipokuwa anashuka kwenye gari,,kweli siyo mzima japo anajaribu kutuaminisha hivyo!
Huenda hataki kuumiza hisia za mashabiki zake,ama amekatazwa kusema kuwa ni mgonjwa!
Kilichomuokoa ni kelele zenu , lakini ilielekezwa amalizwe .
 
Roma asiposema ukweli atajiju mwenyewe.
 
Wasiwasi wangu ni marinda yamesalimika?
Dr Ulimboka ndiye aliyepata mateso makubwa sana kati ya waliopona kwa bahati.

1.Kutolewa kucha.
2.Kutolewa Meno.
3.Kupasuliwa Balls na Kutiwa uhanisi.
 
Namshukuru Mungu kwa kuonekana kwao maaana huku mitaani maneno ya yalikuwa yamesha kuwa mengi kwa serikali. Mungu anaipenda serikali yetu. Hongera JPM kwa kuwa na wapelelezi walio bobea Mungu akubariki aminaa
Shukrani za dhati zimfikie Bashite popote alipo.
 
RIPOTI YA KUTEKWA KWA ROMA - WILLYD HABARI
Baada ya usiku wa jana Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wenzao wawili kuachiwa salama baada ya kutekwa na watu wasiojulikana alhamisi iliyopita wakiwa studio za Tongwe Record Masaki jijini Dar es salaam, Bongo5 imekukusanyia matukio yote pamoja na kauli mbalimbali ambazo zilitolewa na viongozi pamoja na wadau mbalimbali katika harakati za kupatika kwa Roma na wenzake.



Jiunge bongo193.blogspot.com
 
Mbona anachechemea? Wamemfanya nini jamani????
 
Sijui una elewa nini kuhusu haki na sheria.
Sheria pia inatambua haki na hukumu stahiki kwa wapuuzi.
Sheria inayotambua haki zako kama raia huru pia inatambua na kuweka mipaka ya dhidi dhuruma.
Mpuuzi pia anataratibu zake za kushughulikiwa.
Jifunze kwanza kujua katiba,haki na sheria.
Ni sawa kumfanya mtu chochote kwa kuwa tu mpuuzi?!
Unamkumbuka mwanafunzi wa IFM aliyeuwawa pale Posta baada ya kuitiwa kuwa na mwizi na watu wakajichukulia sheria mkononi kana kwamba hii nchi haielekezi namna ya kushughulika na mhalifu?
Unamkumbuka baba wa watoto Wawili aliyeuwawa msimbazi kwa kudhaniwa kuwa ni mwizi?
Yote hii ni kwa sababu tunashindwa kuheshimu sheria na haki.
Ni sawa kwa mwalimu kumpiga mwanafunzi kama mwizi kwa kuwa amemkosea?
Ustaarabu ni kuishi within agreed guidelines

"...With law man is noble being, without it he is lower than anything..."


hakuana Taifa linalofata haki duniani kwa kuvumilia upuuzi.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom